Tangu Sasa Hata Milele
Akahesabiwa Kifungo na Mauti
Tena zoruba ya hasira ikatokea kwa nguvu, na Jerome akapelekwa gerezani kwa haraka. Kwani kulikuwa wengine ambao maneno yake yaliwagusa na kuwapa mawazo mioyoni na walitamani kuokoa maisha yake. Alizuriwa na wakuu wenye cheo na kumuomba sana kutii baraza. Matumaini mazuri yalitolewa kama zawadi. TSHM 48.4
“Shuhudieni kwangu kwa Maandiko matakatifu kwamba niko katika makosa,” akasema, “na nitaikana kwa kiapo.” TSHM 48.5
“Maandiko matakatifu”! akapaza sauti mmoja wao wa wajaribu wake, “je, kila kitu basi ni kuhukumiwa kwa yale Maandiko? Nani anaweza kuyafahamu mpaka kanisa ameyatafsiri?” TSHM 48.6
“Je, maagizo ya watu yanakuwa na bei kuliko injili ya Mwokozi wetu?” akajibu Jerome. TSHM 48.7
“Mpunga dini!” lilikuwa jibu. “Natubu kwa kutetea wakati mrefu pamoja nanyi. Naona kwamba unashurutishwa na Shetani”. TSHM 48.8
Kwa gafula akapelekwa mahali pale pale ambapo Huss alitoa maisha yake. Alikwenda akiimba njiani mwake, uso wake ukang’aa kwa furaha na amani. Kwake mauti ilipoteza kutisha kwake. Wakati mwuaji, alipotaka kuwasha kundi, akasimama nyuma yake, mfia dini akapaza sauti, “tieni moto mbele ya uso wangu, Kama nilikuwa nikiogopa, singekuwa hapa.” TSHM 48.9
Maneno yake ya mwisho yalikuwa ni maombi: “Bwana Baba Mwenyezi, unihurumie, na unirehemu zambi zangu; kwa maana unajua kwamba nilikuwa nikipenda sikuzote Ukweli.” Majifu ya mfia dini yakakusanyiwa na, kama yale ya Huss, yakatupwa katika Rhine. Basi kwa namna hii wachukuzi wa nuru waaminifu wa Mungu waliangamizwa. TSHM 49.1
Kuuawa kwa Huss kuliwasha moto wa hasira na hofu kuu katika Bohemia. Taifa lote likamtangaza kuwa mwalimu mwaminifu wa ukweli. Baraza likawekewa mzigo wa uuaji wa mtu kwa makusudi. Mafundisho yake yakaleta mvuto mkubwa kuliko mbele, na wengi wakaongozwa kukubali imani ya Matengenezo. Papa na mfalme wakaungana kuangamiza tendo hili la dini, na majeshi ya Sigismund yakatupwa juu ya Bohemia. Kwa kushambulia wenye imani ya matengenezo. TSHM 49.2
Lakini Mwokozi akainuliwa juu. Ziska, mmojawapo wa wakuu wa waskari wa wakati wake, alikuwa mwongozi wa watu wa Bohemia. Tumaini katika usaada wa Mungu, watu wale wakashindana na majeshi ya nguvu yale yangaliweza kuletwa juu yao. Mara nyingi mfalme alikashambulia Bohemia, ila tu kwa kufukuzwa. Wafuasi wa Huss wakainuliwa juu ya hofu ya mauti, na hakukuwa kitu cha. Mshujaa Ziska akafa, lakini pahali pake pakakombolewa na Procopius, kwa heshima fulani alikuwa mwongozi wa uwezo zaidi. TSHM 49.3
Papa akatangaza pigano juu ya maovu (crusade) juu ya wafuasi wa Huss. Majeshi mengi akatumbukia juu ya Bohemia, kwa kuteswa tu na maangamizi. Pigano lingine la maovu likatangazwa. Katika inchi zote za dini ya Roma katika Ulaya, mali na vyombo vya vita vikakusanywa. Watu wengi wakaja kwa bendera ya kanisa la Roma. TSHM 49.4
Majeshi makubwa yakaingia Bohemia. Watu wakakusanyika tena kuwafukuza. Majeshi mawili wakakribiana hata mto tu ndio uliokuwa katikati yao. “Wapiga vita juu ya maovu (crusade) walikuwa katika jeshi bora kubwa na la nguvu, lakini badala ya kuharakisha ngambo ya kijito, na kumaliza vita na wafuasi wa Huss, ambao walikuja toka mbali kukutana nao, wakasimama kutazama kwa kimya wale wapingaji.” TSHM 49.5
Kwa gafula hofu kuu ya ajabu ikaangukia jeshi. Bila kupiga kishindo jeshi kubwa lile likatiishwa na likatawanyika kama kwamba lilifukuzwa na nguvu isiyoonekana. Wafuasi wa Huss wakawafuata wakimbizi, na mateka makubwa yakaanguka mikononi mwa washindi. Vita badala ya kuleta umaskini, ikawaletea wa Bohemia utajiri. TSHM 49.6
Miaka michache baadaye, chini ya Papa mpya, pigano juu ya maovu lingine likawekwa. Jeshi kubwa likaingia Bohemia. Wafuasi wa Huss wakarudi nyuma mbele yao, kuvuta maadui ndani zaidi ya inchi, kuwaongoza kuwaza ushindi ulikwisha kupatikana. TSHM 50.1
Mwishowe jeshi la askari la Procopius likasogea kuwapiganisha vita. Namna sauti ya jeshi lililo karibia iliposikiwa, hata kabla wafuasi wa Huss kuonekana mbele ya macho, hofu kubwa tena ikaanguka iuu ya wapigani wa crusade. Wafalme, wakuu, na waaskari wa kawaida, wakatupa silaha zao, wakakimbia pande zote. Maangamizo yalikuwa kamili, na tena mateka makubwa yakaanguka mikononi mwa washindi. TSHM 50.2
Kwa hiyo mara ya pili jeshi la watu hodari kwa vita, waliozoea vita, wakakimbia bila shindo mbele ya watetezi wa taifa ndogo na zaifu. Adui waliuawa na hofu kubwa isiyo ya kibinadamu. Yule aliyekimbiza majeshi ya Wamidiani mbele ya Gideoni na watu miatatu wake, alinyosha tena mkono wake. Tazama Waamuzi 7:1925; Zaburi 53:5. TSHM 50.3