Hatua Za Ukamilifu Katika Kristo
Sura ya Tatu—KUTUBU
Binadamu awezaje kuhesabiwa kuwa ni haki mbele ya Mungu ? Mwenye dhambi awezaje kusahihishwa na kuwa kama asiyo na makosa machoni pake ? Kristo ndiye njia tu ya kutupatanisha na Mungu na kutuweka katika hali ya usafi. Lakini twawezaje kufika kwake Kristo ? Watu wengi wangali wakisema kama walivyosema wengine siku ile ya Pentekota: “Tufanya je ?” Jibu la Petro lilikuwa hivi: “Tubuni.” Pengine pia alisema hivi, “Tubu-ni basi, mre jee, ili dhambi zenu zifutwe.” Matendo 2:38; 3:19. HUK 8.1
Kutubu maana yake ni hivi: kuhuzunika kwa ajili ya dhambi, tena na kujitenga nayo mbali. Katuwozi kuacha kufanya makosa mpaka tumetambua ubaya wake; tena hali yetu katika maisha yetu haitabadilika kamwe mpaka tumeitenga dhambi mbali na mioyo yotu. HUK 8.2
Kuna watu wengine ambao hawafahamu asili ya kutubu jinsi ilivyo halisi. Wengi huhuzunika kwa ajili ya makosa yao, tcna hujaribu kuongoka katika mwenendo wao mbolo ya watu, kwa kuwa wanaogopa adhabu ambayo watajipatia kwa ajili ya matendo mabaya. Lakini huku si kutubu kama Mungu anavyotaka. Wao hufikiria adhabu zaidi ya ubaya wa makosa yao. Hivyo ndiyyo alivyofanya Esau alipoona kwamba amepotewa kabisa na urithi wake. Balaam pia, alipotiwa hofu sana kwa ajili yr kumwona malaika aliyesimama mbele yake na upanga mkononi, akakubali kutiwa hatiani asije akauawa; walakini hakutubu kwa kweli, hakugouka moyo, hakuchukizwa na maovu. Yudas Iskeriota, aliponsaliti Bwana, alisema, “Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.” Matt .27:4. HUK 8.3
Alishurutishwa kukiri makosa yake alipoona moyoni mwake jinsi alivyostahili kuhukumiwa na Mungu kwa kosa lake. Lakini kitu kilichomtia hofu kilikuwa hukumu na adhabu ya Mungu; hakuhuzunika sana moyoni na kuingiwa majuto kwa kuwa amemsaliti yule mtakatifu Mwana wa Mungu, au kwa kuwa amemkana Mtakatifu wa Israeli. Farao pia, alipoona maumivu ya Mungu alikiri makosa yake ili apate kuepuka na adhabu; lakini mapigo yalipokoma, alizidi kufanya kiburi. Watu hao wote walililia mambo yaliyotokea kwao kwa ajili ya makosa yao, lakini hawakuwa wakihununika na kujuta kwa ajili ya makosa yenyewe na ubaya wake. HUK 8.4
Lakini kama mwenye dhambi anajitoa kuwa chini ya utawala wa Roho Mtakatifu, ndipo dhamiri yake itakaposafisbwa, ataona barabara jinsi alivyo katika hali ya kufanya dhambi, atafahamu maana na usafi wa amri za Mungu ambazo ndizo msingi wa utawala wake. “Kulikuwako nuru halisi, intiayo nuru kila mtu ajaye katika ulimwengu.” Ych.1:9. Nuru ile, ndiye Kristo, humtia mtu nuru moyoni, mambo ya siri hufunuliwa, na yule mwenye dhambi hujiona jinsi alivyo na hatia machoni pa Mungu mwenye haki kabisa. Pia huelewa upendo wa Mungu na uzuri wa kuwa katika hali ya usafi na utakatifu; hutamani kusafishwa na kupatana na walio mbinguni. HUK 8.5
Sala ya Daudi baada ya kuanguka kwake dhambini hutudhihirishia vizuri namna ya kweli ya kuhuzunika na kujutia maovu. Hakutaka kuli- punguza kosa lake, wala kuepuka na hukumu iliyokuwa stahili yake. Daudi aliona kosa lake jinsi lilivyokuwa kubwa mno; akaona unajisi wa moyo wake; akachukizwa sana na kosa lake. Hakuomba ili apate kuachiliwa tu, akamba pia apate kusafishwa moyoni mwake. Akatamani kuingia katika hali ya usafi na kuwa mmoja na Mungu. Akaomba hivi:- HUK 8.6
“Heri aliyesamehewa makosa, aliyestirikiwa dhambi,
Heri mwanadamu, Bwana asiyemhesabia hatia,
Rohoni mwake isipokuwa hila.” Zaburi 32:1,2.
HUK 9.1
“Unirehemu, Ee Mungu, kwa jinsi ulivyo mwema;
Rehema zako zilivyo kuu, ufute makosa yangu.
Unioshee kabisa hatia yangu, unitakasie dhambi zangu.
Kwani nayajua makosa yangu: na dhambi yangu mbele
yangu daima.........
Unisafishe kwa ezobu, nami nitakuwa safi;
Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji......
Uniumbie moyo safi, Ee Mungu,
Ufanye ndani yangu roho aminifu.
Usinitupe usoni pako;
Usiniondolee roho yako takatifu.
Unirudishe furaha ya wokovu wako:
Unichukue kwa roho bora……
Uniponye kwa damu, Ee Mungu, Mungu wa wokovu wangu;
Na ulimi wangu utaiimba haki yako.” Zaburi 51:1-14.
HUK 9.2
Kutubu namna ile hakuwezekani kwetu sisi kwa uwezo wetu wenyewe; kunawezekana katika Kristo tu. Hapo ndipo wengi hupotea katika kudhani kwamba hawawezi kuja kwake Kristo isipokuwa kwanza wamekwisha kutubia dhambi zao. Ni kweli mtu lazima kutubia dhambi zake kwanza, ndipo Mungu atamwachilia; kwani bila masikitiko moyoni kwa ajili ya makosa, mwenye dhambi hawezi kufahamu jinsi anavyomhita ji Mwokozi. Je, mwenye dhambi hana budi kungo ja kumfikia Kristo mpaka ametubu ? HUK 9.3
Katika Biblia, Neno la Mungu, hatusomi kwamba mwenye dhambi hana budi kutubu kabla ya kukubali mwito wa Kristo aliyesema,“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo, nami nitawapumzisha. “Matt.ll:28. Ni uwezo wa Kristo unaowezesha watu kutubu kwa kweli. Petro ameeleza mambo hayo dhahiri aliposema, “Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na masamaha ya dhambi.” Matendo 5:31. Kwa kadiri tusivyoweza kusamohewa dhambi bila Kristo, hivyo ndivyo tusivyoweza kutubu pasipo nguvu za Roho ya Kristo mioyoni mwetu. Kristo ndiyo asili ya kila fikara njoma. Yoye tu ndiyo awezaye kuutia moyo fikara ya kushindana na maovu. Kila aonaye noyoni mwake haja ya kuwa na kweli na usafi, kila asadikiye hali yake ya dhambi, huwa anashuhudia kwamba Roho Mtakatifu yumo moyoni mwake. HUK 9.4
Yesu amesema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchi nitavuta wote kwangu.” Yoh.12:32. Mwenye dhambi hana budi kumwona Yesu kama Mwokozi wetu aliyekufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu; nasi tukimwona msalabani kwa macho ya kiroho, tutazidi kufahamu mambo ya wokovu, tena wema wa Mungu utatuongoza ili tutubu. Hatuwezi kufahamu barabara upendo wa Kristo jinsi ulivyomshurutisha afe kwa ajili yetu; lakini upendo huo huivuta mioyo yetu kwake. HUK 9.5
Pengine watu huona aibu kwa ajili ya matendo mabaya yao, nao huacha kufanya mabaya mengine, kabla hawajajua kwamba Kristo Yesu ndiye anawavuta kwake. Naye akizidi kuwavuta macho ili wamwangalie msalabani na jinsi alivyopata maumivu kwa dhambi zao, wao nao huzidi kufahamu ubaya wa mwenendo wao wanyewe, na kujua namna ya haki yake Kristo. Nao huwa wanaanza kusema, “Je, dhambi ni kitu gani, ikiwa imetakiwa dhabihu kubwa namna hii kwa kumwokoa mwenye dhambi ? Je, upendo wa namna hii, maumivu haya yete, udhilifu huu, hivi vyote vilikuwa ni lazima ili sisi tusipotee mbali, bali tupewe uzima wa milele ?” HUK 10.1
Isipokuwa mtu amekataa kuvutwa kwake Kristo, Roho yake itazidi kuugeuza moyo wake mpaka ametubu na kuongoka moyo. Mambo ya kidunia hayawezi kutuliza moyo wa binadamu. Furaha ya kweli hupatikana katika kumjua Kristo tu. Kwa njia nyingi, zinazojulikana na zisizojulikana, Mwokozi hutumia sana kuwavuta watu kwake ili waitoe mioyo yao mbali na anasa ya kidunia na kujua mibaraka ya Mungu isiyo na mwisho. Wewe ambaye umetamani moyoni mwako kupata kilicho bora zaidi ya vyote vya kidunia, heri ujue kwamba kutamani huko ni ile sauti ya Mungu anayosema kwako. HUK 10.2
Pengine tumejisifu kwamba maisha yetu yamekuwa safi, dhamiri yetu imekuwa barabara, hatuna haja ya kujitweza moyo mbele ya Mungu kama wabaya wengine; lakini nuru ya Kristo ikituangaza roho zetu, tutaona hali yetu halisi, jinsi tunavyokuwa na unajisi machoni pake; ndipo tutafahamu jinsi haki yetu inavyokuwa kama vitambaa vichafu, tena ni damu yake Kristo peke yake ambayo huweza kutusafisha mioyo unajisi wa dhambi na kutengeneza mioyo yetu tena kuwa katika hali ya kufanana naye. HUK 10.3
Mwonzi mmoja wa nuru ya utukufu wa Mungu ukifikilia moyo ndani, umetosha kutudhihirishia hali yetu katika dhambi, udhaifu wetu na upungufu wetu. Hivyo twatambua tamaa zetu zisizo safi, jinsi tunavyomkana Mungu mioyoni mwetu, na jinsi midomo yetu inavyotoa maneno yasiyofaa. Roho ya Mungu ikiupenya moyo ndani, na kumjulisha mtu hali yake ya kumwasi Mungu, hapo ndipo hujichukia sana akijilinganisha na Kristo jinsi alivyo safi bila mawaa yo yote. HUK 10.4
Nabii Daniel alipouona utukufu wa mjumbe wa Mungu aliyetumwa kwake, akabaini moyoni mwake jinsi udhaifu na ukosefu wake ulivyokuwa mkubwa. Akasema, “Kazikusalia nguvu ndani yangu: kwani uzuri wangu umebadilika mwangu kuwa uharibifu, wala sikuwa na nguvu.” Daniel 10:8. Mtu akijiona hivyo kuwa si safi, ndivyo atakavyotaka kuwa na moyo safi na kuingia katika hali ya kupatana na amri za Mungu na kufanana naye Kristo. HUK 10.5
Paulo alipojichunguza aliona kwamba katika matendo ya nje alikuwa hana makosa; lekini alipotambua matakwa ya sheria kwa njia ya kiroho, alijiona kuwa ni mwenye dhambi kabisa. Kama alijipima kwa maneno ya sheria za Mungu jinsi wanavyopima binadamu kwa matendo ya nje, Paulo alijiona kwamba amekuwa katika hali ya kutofanya makosa, hakuwa na hatia; lakini alipoichunguza na kujua maana hasa ya sheria, akajiona jinsi Mungu alivyomwona yeye, kuwa ni mwenye dhambi kabisa, naye akajishusha moyo na kuungama makosa yake. Alisema, “Na mimi nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, na mimi nikafa.” Warumi 7:9. Alipoona asili ya sheria, jinsi ilivyokuwa ya kiroho, ndipo aliona dhambi jinsi ilivyokuwa ya uovu, naye hakujiona tena kuwa ni bora. HUK 10.6
Mungu hazioni dhambi zote kuwa ni sawa; zinakadirika mbalimbali machoni pa Mungu kama vile zinavyokadirika machoni pa binadamu pia. Lakini tendo baya liwalo lo lote, ingawa linaonekana kuwa ni dogo machoni pa binadamu, hakuna dhambi inayobesabiwa kuwa ni ndogo machoni pa Mungu. Hukumu ya kibinadamu si kamili, kwa kuwa huona sehemu moja tu; hawezi kujua nia ya ndani ya mtu; walakini Mungu hujua moyo tena hukadiri mambo jinsi yalivyo halisi. Mlevi hudharauliwa na wenziwe na kuambiwa kwamba dhambi yake itamwacha asiingie mbinguni; lakini mara nyingi makosa kama kufanya kiburi, kujifikiria mwenyewe bila kufikiri wengine, kuwa na choyo, na mengineyo kama hayo hayakadirikiwi na binadamu. Lakini makosa kama hayo yanachukizwa sana na Mungu; kwa kuwa yamekuwa kinyume kabisa cha sifa yake Mungu mwenyewe. Yule ambayo hufanya dhambi zinazohesabiwa na binadamu kuwa ni mbaya sana - yaani ulevi, kuiba, uzinzi na nyinginezo - mtu kama huyo huona aibu na namna anavyomhitaji Kristo; lakini mwenye kufanya kiburi haoni lazima yake, naye humfungie Kristo asiingie moyoni mwake, na kwa hivyo hukosa kupata mibaraka yake. HUK 11.1
Yule mtoza ushuru aliyeomba, “Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi,” alijiona kwamba yu mtu mbaya sana, na wengine pia wakamwona hivyo; lakini yeye alijua shida yake, naye alimletea Mungu mzigo mzito wake wa dhambi kwa haya, ili Mungu amrehemu na kumtoa katika utumwa wa dhambi. Luka 18:13. Yule Mfarisayo aliyefanya kiburi na kujifanya mwenye haki katika sala zake, akaonyesha kwamba amemfungia Roho Mtakatifu mlango wa roho yake, asiingie. Kwa hivyo. hakujiona jinsi alivyo na unajisi; hakuona jinsi anavyouhitaji msaada wa Kristo, naye hakupata kubarikiwa kamwe. HUK 11.2
Ukitambua hali yako jinsi ulivyo katika dhambi, usingojee kumwendea Kristo mpaka ume jaribu mwenyewe kujitengeneza kuwa safi. Wengi hufikiri kwamba hawawezi kumfikia Kristo kwa kuwa ni wabaya. Je, unafikiri utapata kuwa mwema kwa uwezo wako mwenyewe ? “Aweza Mkushi kubadili ngozi yake, au chui madoadoa, ndipo nanyi mtaweza kutanda moma, mliofundishwa kutenda mabaya.” Yer.13:23. Kakuna msaada kwetu ila kwa Mungu tu. Sisi wenyewe hatuwazi kitu. Imetulazimu kwenda kwake Kristo kama tulivyo. HUK 11.3
Hata hivyo tusijidanganyo katika kufikiri kwamba Mungu, kwa neeraa yake, atawaokoa hata wale wanaotupia mbali neema yake na rehema zake. Afikiriye hivyo, afadhali aitazame Kalwari. Kwa kuwa hakuna njia nyingine ya kuwaokoa watu, kwa kuwa bila dhabihu aliyoifanya Kristo katika kufa kwake msalabani. binadamu asingeweza tena kuwa katika hali ya kupatana na watakatifu wa mbinguni - kwa hivyo Kristo alichukua mwenyewe dhambi za wakosaji, akaadhibiwa kwa ajili yao. Upendo wa Mwana wa Mungu, maumivu yake, na kufa kwake, hivi vyote hushuhudia jinsi dhambi inavyokuwa kubwa mno machoni pa Mungu; pia mambo hayo yatudhihirishia kwamba hakuna njia ya kuokoka na kutoka katika utawala wa uovu, hakuna matumaini ya uzima bora wa milele, ila kwa kujiweka chini ya mamlaka yake Kristo na kumtii. Wenye mioyo migumu wasiotubu, pengine hujisingizia wakisema hivi juu yao wanaojisifu kuwa ni Wakristo, “Hata mimi ni mtu mwema kwa kadiri wanavyokuwa wema wale, Wao hawajinyimi zaidi ya mimi; mimi najiweza jinsi wafanyavyo. Wao pia hupendezewa na anasa ya kiaunia kama nipendezewavyo mimi.” Hivyo watu kama hao hujisingizia kwa ajili ya makosa ya wengine ili wasifanye wajibu wao. Lakini kujisingizia hivyo hakufai kitu; kwa kuwa Bwana ametuwekea mfano usio wa kibinadamu, bali Mwana wa Mungu, asiye na ila wala kosa lo lote, yeye ndiye mfano wetu. Wale ambao hunung unika kwa ajili ya mwenendo mbaya wa wengine wanaojisifu kuwa ni Wakristo, imewapasa kufuatisha maisha na matendo ya Kristo, na kuwatolea wengine namna ya mfano ulio bora. Wamejua namna iwapasavyo Wakristo kufanya; hivyo wakikosa wenyewe kufanya yaliyo mema, makosa yao ni makubwa zaidi. HUK 11.4
Tuangalie tusifanye usiri. Tusichelewe kuziacha dhambi zetu na kutaka usafi wa moyo katika Yesu. Watu wengi hukosa katika jambo hilo; hukawia katika kujitoa kuwa wa Kristo; wafanyao hivyo wanachagua kuishi katika hali ya kufanya dhambi. Kitu ambacho tunakosa kukishinda, kitatushinda sisi na kutuangamiza. HUK 12.1
Adam na Hawa walijidanganya kwamba kula matunda yaliyokatazwa si kosa kubwa linaloweza kuadhibiwa kama Mungu alivyosema. Lakini katika jambo hilo dogo walihalifu amri takatifu ya Mungu, amri isiyobadilika; kwa hivyo binadamu akatengwa mbali na Mungu, tena kifo na taebu viliingia duniani mwetu. Kufa kwake Yesu katika Kalwari, kama dhabihu, kulikuwa njia ya pekee ya kufanya upatanisho tena kati ya Mungu na binadamu. Tusidhanie dhambi kwamba si kitu sana. HUK 12.2
Kila tendo baya, kila mara unapoidharau na kuitupia mbali neema ya Kristo, moyo wako huzidi kuwa ngumu, nia yako huzidi kuwa mbaya, nawe huzidi kuwa katika hali ya kutosikia maombezi ya Roho Mtakatifu moyoni mwalco. HUK 12.3
Watu wengi huwa wakijituliza dhamiri na mawazo yanayowasumbua, wakidhani kwamba wataweza kugeuza mwenendo wao mbaya wakati wo wote watakapo; wao hufikiri kwamba waweza kutupa na kutosikia wito wa Roho siku nyingine, tena watakuwa wakichomwa moyo mara kwa mara baadaye. Lakini sivyo. Hata tabia mbaya moja tu, ama namna moja ya tamani isiyofaa, ikidumu moyoni itathibitisha moyo katika kutopenda Mungu. Kwa maonyo yote katika Biblia juu ya kuchezacheza na maovu, lile la kututiisha zaidi ndilo hili, linalose, “Maovu yake yatamkamata mwovu mwenyewe, naye atashikwa kwa kamba ya dhambi yake. Methali 5:22. HUK 12.4
Kristo amekuwa tayari kutuweka huru kwa dhambi, lakini ha- lazimishi watu kwa nguvu; kama mtu amekusudia kufanya dhambi, naye hataki kupata uhuru katika Kristo, Kristo angefanya nini tena ? Mtu akifanya hivyo amejiharibu mwenyewe kwa ajili ya kukana upendo wake Kristo. Tumeambiwa, “Sasa ndio wakati uliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokovu.” “Leo, kama mtasikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.” 2 Wakor.6:2; Waeb,3:7,8. HUK 12.5
“Wanadamu hulitazama umbo la nje, lakini Bwana hutazama moyo.” 1 Sam.l6:7. Mungu huutazama moyo wa kibinadamu jinsi ulivyo ukaidi, panapokuwa unajisi na udanganyifu. Mungu hutujua kabisa, moyo wetu, dhamiri yetu, makusudi yetu na maazimio yetu. Nenda kwake jinsi ulivyo na moyo usio safi, na mwambie, “Unitafutetafute, Ee Mungu, uni jue moyo; unijaribu, uni jue mawazo; utazame kama njia ya kukasiri sha mwangu, unichukue kwa njia ya milele.” Zaburi 139:23,24. HUK 13.1
Watu wengi hukubali dini katika akili zao tu, na kufanya matendo matupu ya nje tu, bila kugeuzwa moyo. Imekupasa kuomba hivi, “Uniumbie moyo safi, Ee Mungu; ufanye ndani yangu roho aminifu.” Zab.51:10. Heri ujitahiai ili usipotewe na uzima wa milele kwa jinsi watu wafanyavyo kujiokoa maisha ya sasa wakiwa hatarini. Heri ufanye bidii katika kusoma Neno la Mungu pamoja na kuomba. Katika Neno hilo, kwa njia ya amri za Mungu na maisha yake Kristo, tumeonyeshwa asili ya utukufu, “ambao hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao.” Waeb.12:14. Neno lile husadikisha watu kuwa ni wenye dhambi, tena huonyesha njia ya kupata wokovu. Heri ulisikilize kama sauti ya Mungu inayosema nawe moyoni mwako. HUK 13.2
Kama umefahamu dhambi jinsi ilivyo mbaya sana, na kujiona mwenyewe jinsi ulivyo katika hali ya kufanya dhambi, usikate tamaa. Kristo alikuja ili awaokoe wenye dhambi. Si juu yetu kufanya patanisho kati ya Mungu na sisi, lakini katika Kristo Mungu mwenyewe alifanya patanisho. “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” 2 Wakor.5:19. Hakuna hata mzazi wa kibinadamu ambaye angefanya saburi juu ya makosa ya mwanawe jinsi Mungu anavyofanya kwa wale atakao kuwaokoa. Ahadi zake zote, hata na maonyo yake yote, ni kwa ajili ya upendo wake tu, upendo usioelezeka hasa jinsi ulivyo. HUK 13.3
Kama Shetani anakuambia kwamba wewe ni mwenye dhambi, mwangalie Mwokozi wako na kuongea juu ya tabia na sifa zake. Ziungame dhambi zako na mwambie adui kwamba “Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi.” 1 Tim. 1:15. Yesu alimwuliza Simon swali juu ya wadeni wawili. Mmoja alikuwa anamwia bwana wake pesa kidogo, na mwingine mapesa mengi, naye bwana yule aliwaachilia wote wawili; na Kristo akamwuliza Simon ni nani atakayempenda bwana wake zaidi. Simon alimjibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa naye mengi.” Luka 7:43 HUK 13.4
Sisi tumekosa sana, lakini Kristo alikufa ili tupate kuachiliwa dhambi. Wale ambao amewaachilia zaidi, wao ndio watakaompenda zaidi na kukaa karibu naye, tena kumsifu zaidi katika ufalme wake kwa ajili ya upendo wake na dhabihu aliyoifanya kwa ajili yao. Tukifahamu sana upendo Mungu jinsi ulivyo, ndivyo tutakapozidi kufahamu dhambi jinsi ilivyo mbaya mno. Na jinsi tunavyozidi kufahamu kama Kristo alivyojinyima kwa ajili yetu, ndivyo tutakavyozidi kuchomwa moyo na kujitoa kwake kuwa watu wake kabisa. HUK 13.5
Nilikupa wewe
Damu ya moyoni,
Ili wokolewe,
Winuke ufuni:
Nimekunyimani wewe;
Umenipa nini ?
Nilikupa myaka
Yangu duniani;
Upate inuka,
Kuishi mbinguni;
Nimekunyimani wewe;
Umonipa nini ?
Nimekuletea,
Huku duniani,
Pendo na wokovu,
Zatoka mbinguni;
Nimekunyimani wewe;
Umenipa nini ?
HUK 14.1