Hatua Za Ukamilifu Katika Kristo

4/13

Sura ya Nne—KUUNGAMA DHAMBI

“Mwenye kusetiri makosa yake hatasitawi: kila aziungamaye na kuziacha atarehemiwa.” Methali 28:13 HUK 15.1

Masharti yanayompasa mtu kufanya ili apate rehema ya Mungu si magumu, ni ya haki na ya maana. Bwana Mungu hataki tufanye mambo mazito ili tusamehewe dhambi; hasemi tufanye malipo makubwa kwa ajili ya dhambi zetu; asema tu kwamba anayeungana dhambi zake na kuziacha, ndiye atakarehemiwa. HUK 15.2

Mtume Yakobo asema, “Ungameni makosa yenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpata kuponya,” Yak.5:16. Ungama dhambi zako hasa kwa Mungu, ambayo yeye tu ndiye awezaye kuzisamehe; lakini makosa ambaye umewafanyia wanadamu, basi uyaungawa mbele ya wanadamu. Hivi ikiwa umemfanyia fulani yasiyofaa na kumchukiza kwa njia yo yote, nenda kwake na kuungama kosa lile ulilomfanyia, naye amepasiwa kulisamehe kabisa. Nyuma yake imekupasa kuomba msamaha kwa Mungu, kwa sababu huyo mwenzako ni kiumbe cha Mungu, na kumfanyia mwanadamu makosa ni kufanya makosa machoni pa Mungu pia. Hivyo kwa njia ya kuomba, mambo hufika mbele ya Mwombeaji wetu, Kuhani Mkuu wetu ambaye “alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi,” naye awezaye “kuyachukua mambo yetu ya udhaifu,” huweza kutusafisha uchafu wote wa dhambi. HUK 15.3

Wale ambao hawajajishusha moyo mbele ya Mungu na kuziungama dhambi zao na kukiri kwamba wametiwa hatiani, hao nao hawajafanya bado jambo la kwamza lipasalo ili wapete kukubaliwa na Mungu. Isipokuwa tumemtubia Mungu kwa kweli, na kuchukizwa kabisa na maovu yetu, tumekuwa katika hali ya kutoomba kweli kwa kupata kusamehewa dhambi zetu; hivyo hatujapata kweli amani ya Mungu rohoni mwetu. Mtu akikiri dhambi zake, kukiri kwake lazima kuwe kwa moyoni; mtu akimtupia Mungu roho yake yote, Mungu atamhurumia kweli. “Bwana yuko karibu yao wenye moyo uliovunjika, wenye roho iliyopondeka kuwaokoa.” Zaburi 34:18.. HUK 15.4

Katika kuungama kwa kweli, imepasa kukiri dhambi au kosa hasa jinsi lilivyo. Pengine ni dhambi ambazo zimefaa kukiriwa kwa siri mbele ya Mungu tu; pengine ni tendo baya lifaalo kukiriwa kwa mtu mmoja tu, yule aliyehasiriwa kwa tendo lile; au pengine ni kosa lifaalo kukiriwa kwa wazi hadharani ya watu; hata ni dhambi au kosa la namna gani, mwenye kufanya kosa lazima kukiri kosa lile lile ambalo amelifanya. HUK 15.5

Zamani wakati wa Samweli, Waisraeli walimwasi Mungu; tena waliona taabu kwa ajili ya dhambi zao. Walikuwa hawamwamini Mungu jinsi alivyokuwa na uwezo ha akili kwa kuwatawala vizuri. Walimtupia Mfalme Mkubwa kisogo, nao walitaka kutawaliwa kwa jinsi yalivyotawaliwa mataifa mengine yaliyokuwa karibu nao. Na kabla ya kukubaliwa tena na Mungu, wakakiri hivi: “Tumeziongoza dhambi zetu kwa uovu wa kututakia mfalme. ” 1 Sam.12:19: Kosa lile lile ambalo nalo walitiwa hatiani, liliwalazimu kulikiri hasa. HUK 15.6

Kukiri kutupu hakutakubaliwa na Mungu bila kutubu kwa kweli na kugeuka moyo na matendo ya maisha; kila kitu kinachomchukiza Mungu lazima kutolewa ili mwenendo uwe safi machoni pakc. Kazi iliyo wajibu wetu imeelezwa dhahiri hivi:“Osheni, safikeni; wekeeni mbali uovu wa matendo yenu toka machoni pangu; acheni kutenda maovu; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu, msaidieni mwenye kuonewa, mhukumieni yatima, mteteeni mjani.” Isa.1:16,1. “Mwovu atakaporudisha amana, akitoa tena aliyoitwaa kwa unyang’ anyi, akiendea shoria za uzima, asipotenda maovu; kuishi ataishi, hatakufa.” Ezek. 33:15. Mtume Paulo alisema hivi juu ya kutubu: “Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naan, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa kila njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo. 2 Wakor.7:11. HUK 16.1

Kama maovu yametia giza macho ya kiroho, mwenye dhambi hawezi kutambua hali yake jinsi alivyo na upungufu, na jinsi makosa yake yanavyokuwa mabaya sana; tena isipokuwa atajitoa ili Roho Mtakatifu atumie moyoni mwake, basi atadumu kuwa na giza la kiroho. Kukiri kwake si kwa kweli wala kwa haki. Anapoungama kosa lake hujisingizia akisema kwamba laiti mambo yasingalikuwa hivi na hivi, asingalifanya hivi na hivi, na hivyo asingalipata kukaripiwa. HUK 16.2

Adamu na Hawa walipokwisha kula natunda yaliyokatazwa, waliona haya na hofu kuu. Mara ya kwanza walifikiri namna ya kujitetea kosa lao, ili waepukane na hukumu ya kifo. Mungu alipowauliza habari za kosa lao, Adam akawa kama anamlaumu Mungu, akisema, “Mwanamke uliyenipa kuwa nami, ndiye aliyenipa ya mti, nikala.” Yule mwaaamke alinshtaki nyoka akisema, “Nyoka alinidanganya, nikala.” Mwanzo 3:12,13. Inaonekana kwamba wote wawili walikuwa wanamsingizia Mungu - Adam kwa ajili Mungu alimpa mwanamke; tena Hawa kwa ajili ya kumwumba nyoka na kumwacha aingie katika bustani ya Aden. Ile roho ya kujifanya kuwa na haki ilianzishwa na yule baba wa uwongo, nayo huonekana kwa wanadamu wote. Kukiri namna hii na kujisingizia haifai kitu, wala hakukubaliwa na Mungu. Katika kutubu na kukiri kwa kweli, mtu hukubali kwamba ametiwa hatiani bila kujisingizia wala kutaka kujifanya mwenye haki Huomba kana yule mtoza ushuru alivyoomba, na kusema, “Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi;” asitake hata kuinua macho yake mbinguni. Hao nao wanaokiri makosa yao na namna walivyotiwa hatiani, watapata msamaha, kwa kuwa Yesu atawaombea kwa ajili ya damu yake iliyomwagika kwao wenye kutubu. HUK 16.3

Katika Neno la Mungu twasoma habari juu ya wengine wenye kutubu kwa kweli, na kujishusha mioyo na kuziungama dhambi, wala hawakuwa na moyo wa kujisingizia ama kujifanya wenye haki. Fikiri jinsi alivyosema Paulo, asitake kamwe kujitetea makosa yake: “Niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndeni ya magereza, nikiisha kupewa amri na makuhani wakuu; na walipouawa nalitoa idhini yangu. Na mara nyingi katika masunagogi mengi nali waadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama nina wazimu, nikawaudhi hata katika miji ya ugenini.” Matendo 26:10,11. Lakini hakuogopa kusema,“Yesu Kristo alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.” Alijiona kuwa ni mwonye dhambi zaidi ya wengine wote. 1 Tim. 1:15 HUK 16.4

Yule mnyenyckevu mwenye kupondeka moyo na kutubu kwa kweli, yeye atafahamu kidogo upendo wa Mungu, na dhabih iliyofanywa Kalwari jinsi iliyyo na thamani kubwa sana. Tena jinsi mtoto atakavyoziungama makosa yake mbele ya baba yake anayempenda, hivyo ndivyo mwenye kutubu atakavyomletea Mungu dhambi zake zote; kama ilivyoandikwa, “Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.” 1 Yoh.l:9. HUK 17.1

Ninaye Rafiki, naye alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo zake nimefungwa milele;
Aukaza moyo wangu, nisitengane naye;
Mimi wake, Yeye wangu; ndimi naye milele.

Ninayo Rafiki ndiye aliyonifilia;
Alimwaga damu yake kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena, nikiwa navyo tele;
Pia vyoto ni amana ndimi wake milele.

Ninaye Rafiki, naye yuna na moyo mwema;
Ni Mwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga na Mpenzi wa mbolo ?
Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele.
HUK 17.2