Hatua Za Ukamilifu Katika Kristo

2/13

Sura ya Pili—JINSI MWENYE DHMABI ANAVYOMHITAJI KRISTO

Hapo mwanzo binadamu alipewa uwezo bora na fikara safi. Alikuwa mkanilifu katika mwili wake, nayo akawa katika hali ya umoja na Mungu. Fikara zake zilikuwa safi na makusudi yake yakawa matakatifu. Lakini kwa ajili ya kutomtii Munju, uwezo wake uligeuka ukawa mbaya, tena badala ya upendo akawa akijifikiria nafsi yake mwenyewe. Dhaniri yake ikapungua nguvu kwa sababu ya kufanya dhanbi, hata yeye mwenyewe kwa nguvu zake peke yake alikuwa hawezi kushindana na maovu. Alikuwa chini ya mamlaka ya Shetani, naye mwanadanu angalikuwa katika hali hiyo milele isingalikuwa Mungu kuingia kati. Ilikuwa nia ya mshawishi, yaani Shetani, kuyapinga maazimio mema ya Mungu katika kumwumba binadanu, na kujaza dunia ubaya na ukiwa. Na hatimaye angesema kwanba mabaya hayo yote yalitokea kwa ajili ya kazi ya Mungu katika kumwumba binadamu. HUK 5.1

Katika hali yake ya kutokuwa na dhambi mwanzoni, mwanadamu akawa na furaha katika kuzungumza na Yule “ambaye ndani yake zimo hazina zote za hokina na maarifa.” Wakol.2:3. Lakini baada ya kufanya dhambi mwanadamu hakuweza kufurahishwa na hali ya utakatifu, naye alitaka kujificha mbali na macho ya Mungu. Hata sasa hiyo ndiyo hali ya moyo usioongoka. Haupatani na Mungu, tena hakuna furaha katika maongezi naye. Mwenye dhambi asingeweza kuwa na furaha mbele ya Mungu; angewaepuka watakatifu. Kama angeweza kuruhusiwa kuingia mbinguni, asingekuwa na furaha huko. Naye asingeweza kushinikiana nao walio mbinguni katika hali ya kuwa na roho inayopatana na Mungu, yaani roho isiyofikiria nafsi yake mwenyewe, bali huwa ya kuwafikiri wengino kwa upendo. Fikara zake, mambo anayoyapenda, na maazimio yake yote, vyote hivi vingemfanya mwenye dhambi kuwa mgeni kabisa kati ya wateule wa Mungu; angekuwa hawezi kulingana nao. Angeona mbinguni kama ni mahali pabaya kwake; angetaka kujificha mbali na uso wake yeye aliye nuru na furaha ya watakatifu wa Mungu. Si amri isiyo na kanuni ambayo huwazuia wabaya wasiingie mbinguni; siyo! Watakuwa wakifungiwa wasiingie mbinguni kwa ajili ya hali yao ya kutopatana katika umoja wa hao walio mbinguni. Utukufu wa Mungu ungekuwa kama moto wa kuwateketeza, nao wangetaka kufichwa wasimwone uso wake yeye aliyekufa kuwakomboa watu. (Ufunuo 6:15-17) HUK 5.2

Sisi wenyewe kwa nguvu zetu hatuwezi kujiokoa katika shimo la uovu ambano tumeangukia. Mioyo yetu mibaya kabisa, nasi hatuwezi kuigeuza. “Awezaye nani kutoa kilicho safi katika kisicho safi ? si hata moja.” “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maar.a haitii sheria za Mungu wala haiwezi.” Ayub 14:4; Warumi 8:7. Elimu, ustaarabu, kujitawala nia, kujibidisha, hivi vyote vinafaa, lakini katika kazi hii ya kuugeuza moyo haviwezi kitu kamwe. Pengine vyaweza kumfanya mtu awe na mwenendo mzuri mbele ya watu; lakini havi-wezi kuigeuza asili yake na moyo wake. Nguvu isiyokuwa yake mwenyewe lazima kuitumike moyoni mwake ili apate uzima mpya utokao juu, hapo ndipo binadamu ataweza kugeuza hali yake ya kufanya dhambi na kuwa katika hali ya usafi. Nguvu hiyo ndiyo Kristo. Ni yeye tu ambaye anaweza kuwavuta watu kwa Mungu ili wawe safi. Mwokozi alisema,“Mtu asapozaliwa mara ya pili,” yaani kuzaliwa na Roho, “hawezi kuona ufalme wa Mungu.” Yoh.3:3. Maana yake, isipokuwa amepata moyo mpya, nie mpya, maazimio mapya, na kuishi katika uzima mpya, “hawezi kuingia ufalme wa Mungu.” Yoh.3:5. Tusifikiri kwamba inatosha kuziongsza zile tabia njema ambazo amezipata mtu tangi asili. “Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake ni mapumbavu, wala hawezi kuya jua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” “Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.” 1 Wakor.2:14-; Yoh.3:7. Imeandikwa juu ya Kristo, “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu;” tena “hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa nalo” Yoh.l:4; Matendo 4:12. HUK 5.3

Haitoshi kujua namna ya upendo, na neema ya Mungu. Haitoshi kutambua tu namna ya amri zake, jinsi zilivyo za haki. Mtume Paulo aliyajua haya yote, akasema, “Nakiri ya kuwa sheria ile ni njema.” “Torati ni takatifu, na ile amri takatifu na ya haki na wema. Warumi 7:16,12. Naye akazidi kusema kwa uchungu wa moyo, “Mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.” Warumi 7:14. Alitamani sana kuwa na usafi na uadilifu kamili, ambavyo yeye mwenyewe kwa nguvu zake hakuweza kuvipata, naye akalia, “Ole wangu mimi binadamu! nani atakayeniokoa na mwili huu wenye kunifisha.” War.7:24. Kila anayelia hivyo hujibiwa neno moja tu, “Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” Yoh.l:29. HUK 6.1

Kwa njia nyingi na mifano mingi Roho Mtakatifu amejaribu kuwafundisha watu mambo hayo, na kuwaeleza dhahiri wale watakao kuokolewa katika dhambi. Yakobo alipokimbia baada ya kumdanganya Esau, aliona moyoni mwake kuwa ana hatia; naye akaogopa akifikiri labda makosa yake yamemtenga mbali na Mungu, naye akawa na huzuni moyoni mwake. Alipolala usingizi usiku ule, akacta ndoto; aliona ngazi iliyotoka chini mpaka mbinguni; tena malaika wa Mungu wakawa wakipanda na kushuka; tena kutoka mahali patakatifu juu akasikia sauti ya Mungu ikimwambia maneno ya kumtia moyo. Mambo hayo yakamjulisha Yakobo kwamba yuko Mwokozi, tena alimwona jinsi alivyoweza kurudishwa tena kupatana na Mungu. Ile ngazi ya ndoto ilikuwa mfano wa Yesu, ambaye ni njia peke yake ya wanadamu kuweza kumfikie Mungu. HUK 6.2

Huu ndio mfano Yesu alioutaja alipozungumza na Nathanael, akisema, “Mtaziona mbingu zimefunguka, na malaika wa Mungu wakipanda, wakishuka juu ya Mwana wa Adamu.” Yoh.l:51. Katika maasi yake, binadamu alijitenga mbali na Mungu; wanadamu walikuwa hawawezi kuzungumza na wa mbinguni kama walivyokuwa wamezoea kufanya zamani. Lakini kwa ajili ya Kristo tumepata njia ya upatanisho. Malaika waweza kuja kusema na wanadamu na kuwasaidia. Tena hata kama binadamu wamekuwa wabaya kwa ajili ya dhambi, katika Kristo waweza kupata nguvu ya kushindana na maovu. “Kila kutoa kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu,” kwa Mungu. HUK 6.3

Binadamu hawawezi kuwa na sifa njema ya kweli bila Mungu. Tena Kristo ndiye njia peke yake ya kumfikia Mungu. Asema, “Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.” Yoh.l4:6. Moyo wa Mungu huwafikiria watoto wake duniani kwa upendo mkubwa mno. Alipomtoa Mwanawe wa pekee kwa ajili yetu, alikuwa kama anatoa kwetu ubora wote wa mbinguni. Maisha ya Mwokozi hapa duniani, kufa kwake, na maombezi yake huko mbinguni, msaada wa malaika, maonbezi ya Roho Mtakatifu mioyoni mwetu - hivyo vyote hutuonyesha jinsi Baba yetu aliye nbinguni awapendavyo wanadamu, tena hutumia njia nyingi ili awakomboe HUK 7.1

Heri tufikiri sana habari za Mwokozi wetu, jinsi alivyojitoa kama dhabihu kwa ajili yetu! Ajabu sana, mambo hayo! Imetupasa kufahamu kwamba katika Kristo tumepewa thawabu kubwa kupita kiasi, ili apate kutuokoa na kuturudisha kwake Mungu. Tufikiri tena yote ambayo Mungu amewaahidia waaminfu wake! Thawabu kubwa kwa kufanya ya haki, kufurahishwa mbinguni, kukaa na malaika na kuwa na umoja nao, kuongea uso kwa uso na Mungu na Mwanawe, na kujua upendo wao hasa jinsi ulivyo, tena kuzidi kuelimishwa nilele. Je, hivyo vyote havitoshi kutuonyesha kuwa ni lazima tumtoleo Mwokozi wetu mioyc yetu kwa upendo wetu, ili tuwe watumishi wake milele ? HUK 7.2

Bali, hukumu ya Mungu inetangazwa jinsi itakavyokuwa juu ya dhambi na wenye dhambi, kupata adhabu isiyoepukika , kuwa katika hali ya udhilifu, na uharibifu wa mwisho; hivyo vyote vimetangazwa katika Neno la Mungu kutuonya tusiwe watumishi wa Shetani. HUK 7.3

Laiti tungefikiri sana rehema ya Mungu Angeweza kufanya nini tena zaidi ya hivyo vyote ? Heri tulingamane naye ambaye ame tupenda sana kwa upendo wa ajabu. Heri tufuate njia yake tena tutumie nguvu zake ili tupate kugeuka kuwa katika mfano wake, tuingie tena katika hali ya kushirikiana na malaika kama walivyokuwa wanadamu mwanzcni, hali ya umoja na Baba aliye mbinguni na Mwanawe pamoja. HUK 7.4