Tumaini Kuu

83/254

Maelfu ya Wachungaji Watimuliwa

Katika kame ya kumi na saba maelfu ya wachungaji walifukuzwa na watu walizuiliwa kuhudhuria kwenye mikutano ya kidini ambayo haikuwa imeidhinishwa na kanisa. Kwenye maficho yaliyokuwa yamesitirika msituni, wana wa Mungu waliokuwa wanateswa walikuwa wanakusanyika kuimimina mioyo yao kwa sala na sifa kwa Mungu. Wengi walikuwa wanateseka kwa sababu ya imani yao. Magereza yalikuwa yamejaa watu na familia zilikuwa zimesambaratika. Na mateso yasingenyamazisha ushuhuda wao. Wengi walifukuzwa kupitia baharini na kwenda Amerika na kule waliweka misingi ya uhum wa kiraia na kidini. TK 164.1

Kwenye gereza la chini ya ardhi lililokuwa limejaa wahalifu, John Bunyan alikuwa anadokeza mbingu ilivyo na hapa ndipo alipoandika mashairi yake ya ajabu juu ya safari ya mahujaji kutoka kwenye nchi ya uharibifu kwenda katika mji wa mbinguni. Safariya Mahujaji na Neema Tele kwa Mwenye Dhambi Mkuu ni mashairi ambayo yamewaongoza watu wengi kwenda katika njia ya uzima. TK 164.2

Katika wakati wa giza la kiroho Whitefield na jamaa ya Wesley walionekana kuwa wachukua nuru wa Mungu. Kadri kanisa lilivyokuwa linazidi kuimarika, ndivyo watu walivyokuwa wanateleza kwenda katika hali ambayo ingekuwa vigumu sana kuwatofautisha na watu wasiomcha Mungu. Watu wa daraja la juu walikuwa wanadhihaki utauwa; na watu wa daraja la chini walikuwa wameachwa waishi katika uovu. Kanisa halikuwa na ujasiri au imani kuwasaidia waliokuwa wameanguka kutoka kwenye njia ya kweli. TK 164.3