Tumaini Kuu
Maandiko Matakatifu-Mamlaka Isiyokosea
Kanuni kuu iliyokuwa inadumishwa na Wanamatengenezo hawa ilikuwa ni ileile iliyokuwa inashikiliwa na Wawaldensia, Wycliffe, Huss, Luther, Zwingli, na wale waliokuwa nao-“Maandiko Matakatifu-Mamlaka isiyokosea.” Kwa mafundisho yake, walipima mafundisho na madai yote. Imani katika Neno la Mungu iliwastahimilisha watu hawa watakatifu walipotoa uhai wao kwa kuchomwa moto. “Jipeni moyo,” alisema Latimer kwa mfia dini mwenzake wakati moto ulipokuwa unakaribia kuwanyamazisha, kwa neema ya Mungu, “katika siku kama hii, tutawasha mshumaa kama huu nchini Uingereza, na ninaamini hautazimishwa.” 160 TK 161.5
Kwa mamia ya miaka baada ya kanisa la Uingereza kusalimu amri kwa Kanisa la Roma, makanisa ya Scotland yalidumisha uhuru wao.Hata hivyo kwenye kame ya kumi na mbili utawala wa Papa ulikuwa umeimarishwa na katika kila nchi giza kuu la kiroho lilikuwa limetanda. Bado miali ya nuru ilikuwa inakuja kulipenya giza hilo. Wakitokea Uingereza wakiwa na Biblia na mafundisho ya John Wycliffe, wafuasi wa Wycliffe walikuwa wamefanya mambo makubwa ya kutunza maarifa ya ukweli wa Injili. Kuanza kwa Matengenezo kulifuatana na Maandiko ya Luther na Agano Jipya kwa lugha ya Kiingereza lililokuwa limetafsiriwa na Tyndale. Wajumbe hawa wa kimya walikwenda huku na huko milimani na mabondeni wakiwasha upya mwenge wa ukweli uliokuwa umekaribia kuzimika na kuharibu kazi ya ukandamizaji iliyokuwa imefanywa kwa kame nne. TK 161.6
Walipoishtukia hatari hiyo, viongozi wa Kanisa Katoliki waliwapeleka kwenye nguzo ya kuchomea moto baadhi ya watu waadilifu kabisa wa wana wa Sotland. Mashahidi hawa waliokuwa wanakufa katika nchi yote walikuwa wanaisisimua mioyo ya watu kwa kusudi lao lisilokoma la kuvitupilia mbali vifungo vya Kanisa la Roma. TK 162.1