Tumaini Kuu

17/254

Wenye Dhambi Waelekezwa kwa Kristo

Wawaldensia walikuwa na shauku ya kuwafunulia watu hawa wenye njaa, ujumbe wa amani ulio katika ahadi za Mungu, na kuwaelekeza kwa Kristo kama tumaini lao la pekee la wokovu. Walikuwa wanaamini kuwa fundisho la matendo mema kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi lilikuwa limejengwa katika uongo. Stahili za Mwokozi aliyekufa na kufufuka ndizo msingi wa imani ya Kikristo. Inampasa mwanadamu kumtegemea Kristo kwa karibu kama mkono au mguu ulivyo karibu na mwili au tawi lilivyo karibu na mzabibu. TK 49.3

Mafundisho ya Mapapa na mapadre yalikuwa yanawafanya watu wamwone Mungu na hata Kristo kama mkali na wa kutisha, asiye na huruma kwa wanadamu kiasi ambacho ilikuwa inabidi mapadre na watakatifu waombwe ili kufanya upatanisho. Wale ambao akili zao zilikuwa zimepata nuru walikuwa wanatamani kuondoa vikwazo ambavyo Shetani alikuwa ameviweka, ili watu waweze kwenda moja kwa moja kwa Mungu, watubu dhambi zao, na kupata msamaha na amani. TK 50.1