Kutayarisha Njia
Je! Watu Wawili Waweza Kutembea Pamoja Wasipokuwa Wamepatana?
Mara zingine udhuru unatolewa kuwa huyo asiyeamini ni mtu mzuri kwa dini na kwa mambo yote yanayotakiwa kwa mchumba ila tu jambo moja si Mkristo. Ijapokuwa busara za kuchagua na mwenye kuamini zaweza kuonyesha jambo lisilofaa la umoja wa maisha na yule asiyeamini, lakini, tisa katika kila watu kumi, hushindwa na tamaa. Kupungua kwa hali ya mambo ya kiroho huanzia dakika ile ya kuahidi kwa kiapo kwenye mimbara; moyo wa bidii kwa mambo ya dini unapunguzwa, na ngome moja moja huvunjwa, mpaka wote wawili wamekuwa hali moja chini ya bendera nyeusi ya Shetani. Hata katika furaha za arusi roho ya kidunia hushinda dhamiri, imani, na kweli. Katika nyumba hiyo mpya na saa ya maombi haiheshimiwi. Bibi arusi na bwana arusi wamejichagua wenyewe na (kumfukuza kumwachilia mbali) Yesu. Kwanza yule asiyeamini pengine hataonyesha ushindani katika uhusiano huu mpya; lakini somo la Biblia linapotolewa ili kusikilizwa na kufikiriwa, uchungu utatokea mara moja: “Ulioana na mimi, ukijua kwamba nalikuwa hali hii nilivyo sasa; sitaki kusumbuliwa. Tangu sasa naijulikane kuwa mazungumzo juu ya mawazo yako mwenyewe hayana budi kupigwa marufuku.” Kama mwenye kuamini angeonyesha moyo wo wote wa bidii kwa habari za dini yake, inaweza kuwa kana kwamba hafanyi halali kwa yule asiyependezwa na maisha ya Kikristo. KN 140.3
Mwenye kuamini hufikiri kuwa katika uhusiano wake mpya hana budi kuacha mengine kwa mwenziwe aliyemchagua. Furaha, anasa za kidunia hupendelewa. Kwanza huwapo moyo usiotaka kufanya hivi, lakini upendo wa Neno la Mungu huzidi kupungua, na mashaka huwapo badala ya imani. Hakuna mtu ambaye angeshuku kuwa yule ambaye zamani alikuwa mwenye kuamini, imara na mwaminifu, na mfuasi mwaminifu wa Kristo angeweza kuwa mtu mwenye mashaka, na kusitasita alivyo sasa. Ah, mabadiliko yameletwa na ile ndoa isiyo ya busara! KN 141.1
Ni jambo la hatari kufanya ndoa ya kidunia. Shetani ajua sana kuwa saa ya ndoa ya vijana wa kiume na wa kike hufunga historia ya maisha yao ya dini na ya manufaa. Hawamo kwa Kristo. Pengine kwa muda mfupi watafanya jitihadi kuishi maisha ya Kikristo; lakini jitihadi zao zote zinakutana na mvuto wa nguvu unaozipinga. Zamani walijaliwa na kupendezwa kuzungumza juu ya imani na tumaini lao; lakini hawapendi kutaja somo hilo, wakijua kuwa mtu waliyeungana naye siku zote za maisha yao hapendezwi nalo. Kama matokeo yake, imani katika Neno la kweli la thamani kuu hufifia moyoni, na Shetani hufuma kwa werevu ili kuwazinga pande zote, utando wa mashaka. KN 141.2
“Je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wanapatana?” “Wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.” Lakini jambo hili huonekana kuwa la ajabu kama nini! Huku mmoja wa wale walioungana kabisa (katika ndoa) akishughulika na ibada, mwingine hajali; wakati mmoja wao anapoitafuta njia iendayo uzimam, mwingine yumo katika njia pana iendayo mautini. KN 141.3
Mamia wamemwacha Kristo na raha ya mbinguni kama matokeo ya kuoana na watu wasioamini. Yawezekana kwamba upendo na umoja na Kristo si mambo yenye thamani kwao tena ila kidogo tu hata wanapendelea zaidi urafiki wa maskini wenye kufa? Je, Mbinguni hapatnaminiwi ila kidogo tu hata wanapenda kuzihatarisha raha zake kwa ajili ya mtu asiyempenda Mwokozi wa ajabu? KN 141.4