Kutayarisha Njia

86/210

Maonyo kwa Wale Wenye Kutazamia Ndoa

Vijana wanatumaini sana tamaa ya ghafula. Haiwapasi kujitoa kwa urahisi, wala kutekwa upesi mno na sura ya mchumba. Kadiri uchumba unavyoendeshwa katika zama hizi ni mpango wa udanganyifu na unafiki, ambao kwao adui wa roho za watu anahusiana sana nao kuliko Mungu. Busara njema yatakikana hapa, ikiwa ni hivyo; lakini ukweli ni kwamba, haitumiwi katika jambo hili ila kidogo. Wazo la upuzi, wepesi wa kuvutwa na tamaa, havina budi kuepukwa kwa hadhari kama ukoma. Vijana wengi sana wa kiume na wakike siku hizi ulimwenguni hawana adili; kwa hiyo onyo kubwa linatakikana. Wale ambao pamehifadhi tabia njema, ijapokuwa huenda wasiwe na tabia zingine nzuri zenye kutakikana, waweza kuwa wenye kustahili sifa. KN 136.1

Kuna hali hii duni ya kuvutwa kwa wepesi na tamaa iliyochangamana na mambo ya dini ya vijana wa zama hizi ulimwenguni. Dada yangu, Mungu anakutaka uongoke. Adilisha upendo wako, nakusini. Toa wakfu nguvu zako za akili na za mwili pia kwa kazi ya Mkombozi wako, aliyekununua. Yatakase mawazo na maom yako ya moyoni kusudi matendo yako yote yapate kutendwa kwa Mungu. Malaika wa Shetani wanakesha pamoja na wale wenye kutumia sehemu kubwa ya saa zao usiku katika kuposa. Kama wangefumbuliwa macho yao, wangemwona malaika akiyaandika maneno na matendo yao. Kanum za afya na adabu nzuri zinavunjwa. Ingefaa zaidi kuziacha saa zingine za uchumba kabla ya ndoa kuingia katika maisha ya ndoa. Lakini limekuwa kama jambo la kawaida ndoa kuwa mwisho wa upendo wote ulioonyeshwa katika siku za uchumba. KN 136.2

Shetani anajua mambo hasa apaswayo kushughulika nayo, naye hutumia werevu wake wa kishetani katika hila za namna mbalimbali kuzinasa roho za watu wapate kuangamia. Huangalia kila hatua inayofanywa, na kutoa mashauri mengi na mara nyingi mashauri nayo yanafuatwa badala ya shauri jema la Neno la Mungu. Wavu huu uliosokotwa vizuri, ambao ni hatari umetayarishwa kwa akili kuwatega vijana na wale wasiojihadhari. Mara nyingi huenda ukafichwa gizani; lakini wale wanaonaswa nao hujichoma wenyewe kwa huzum nyingi Kama matokeo yake, twaona mavunjiko ya utu kila mahali. KN 136.3