Kutayarisha Njia

187/210

Uzima wa Mungu Rohoni Ndilo Tumaini la Pekee la Mwanadamu

Dini ya Biblia si kitu cha kudhuru afya ya mwili wala akili. Mvuto wa Roho wa Mungu ni dawa nzuri sana kwa maradhi. Mbingunbi pote kuna afya; na kadiri mivuto ya mbinguni inavyozidi kujulikana, ndivyo hakika wagonjwa wanaoamini watakavyozidi kupona. Mafundisho ya kweli ya dini ya Kikristo huwafunulia wote chimbuko la furaha kubwa mno. Dini ni chemchemi inayobubujika daima, ambayo Wakristo huweza kunywa humo wapendavyo, wala wasiwezi kuikausha, chemchemi hiyo. KN 244.3

Hali ya mawazoni huwa na matokeo katika afya ya mwili. Ikiwa mawazo yana furaha, bila wasiwasi, kutokana na dhamiri safi za matendo mema na kuridhika kwa kuwafurahisha wengine, huanzisha uchangamfu ambao utarudisha hali kwenye mwili mzima, ukiufanya mwendo wa damu mwilini kuwa mzun zaidi, na kuutia nguvu mwili mzima. Mbaraka wa Mungu ni uwezo uponyao, na wale ambao huwafaidia wengine kwa wingi wataufahamu mbaraka huo wa ajabu moyoni na maishani pia. KN 244.4

Watu ambao wamejifurahisha kwa mazoea mabaya na matendo ya dhambi, bila kujizuia wakijitoa kwa uwezo wa Neno la Mungu, kutumiwa kwa hivo kweli moyoni huamsha nguvu za tabia njema, ambazo zilielekea kuwa zilipooza. Mwenye kuupokea huwa na ufahamu wenye nguvu zaidi, na bora kuliko alivyokuwa kwanza kabla hajaikaza roho yake kwenye Mwamba wa milele. Hata afya yake ya mwili huzidi kuwa bora kwa kufahamu usalama wake akiwa ndani ya Kristo. 6 KN 244.5

Watu wanastahili kujifunza kwamba mibaraka ya utii kamili wanaweza kuipata kama wakiipokea neema ya Kristo. Neema yake ndiyo inayomwezesha mtu kuzitii sheria za Mungu. Hii ndiyo inayomwezesha atoke katika kifungo cha mazoea mabaya. Ni uwezo huu peke yake uwezao kumfanya mtu adumu katika njia sawa. KN 245.1

Injili ni dawa ya kuponya magonjwa ambayo asili yake ni dhambi, kama ikipokewa na usafi na uwezo wote. Jua fa Haki litawazukia, “lenye kuponya katika mbawa zake.” Vitu vyote vitokavyo ulimwengum humu sivyo viwezavyo kuuponya moyo uliovunjika, wala kuleta amani mawazoni, wala kuondoa taabu wala kufukuza magonjwa. Fahari, akili halisi, ama majaliwa-vyote haviwezi kuuchangamsha moyo wenye huzuni wala kumrudishia mtu siku za maisha zilizotumiwa ovyo. Tumaini la pekee la mtu ni uhai wa Mungu moyoni mwake. KN 245.2

Upendo ambao Kristo anaueneza katika mwili mzima una uwezo utiao uhai. Kila kiungo-ubongo, moyo, mishipa ya fahamuhuguswa na kuponywa na uwezo huo. Kwa njia yake nguvu za mtu zinaamshwa ili zitende kazi yake. Unauondolea moyo hatia na huzuni, mashaka na taabu, ambazo huvunja nguvu za uzima. Hivyo huleta weupe wa moyo na utulivu. Unatia moyoni furaha ambayo hakuna kitu cho chote duniani kiwezacho kuiharibu,-yaani, raha ya roho, itiayo afya na uzima. KN 245.3