Vita Kuu

33/56

Sura Ya Kumi Na Mbili - Jukwaa Lililo Imara

*****

NALIONA kundi la watu wallolindwa vizuri na kusimama imara, waliokataa kukubaliana na wale waliotaka kutaharakisha imani ya kundi. Mungu alipendezwa na wale waliosimama imara. Nalionyeshwa hatua tatu—ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu. Malaika aliyekuwa akifuatana nami aliniambia. “Ole wake atakayeondoa au kubadili hata sehemu moja ya maneno ya wajumbe hawa watatu. Ni jambo la muhimu sana kuyafahamu maneno ya ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili, na wa tatu. Maisha ya wanadamu yanategemea sana jinsi wanavyoyapokea maneno haya.” VK 88.1

Nalionyeshwa tena mambo ya habari hizi nikaona mambo yaliyowatokea watu wa Mungu katika maisha yao, jinsi yalivyo ya thamani sana. Waliyapata kwa shida nyingi na mateso makali. Mungu alikuwa amewaongoza hatua kwa hatua, mpaka mwishowe akawaweka juu ya jukwaa lisilotikisika. Naliwaona watu wengine wakija mmoja mmoja na kulikaribia lile jukwaa kusudi wautazame msingi wake. Wengine kwa furaha wakapanda mara juu ya jukwaa lile. Wengine walianza kutafuta kasoro fulani katika msingi ule. Walitaka ili itengenezwe sehemu nyingine, ndipo jukwaa lingekuwa kamili, na watu wangefurahi zaidi. VK 88.2

Wengine walishuka chini kutoka kwa jukwaa kusudi walitazame, na wakasenia ya kwamba lilijengwa vibaya. Lakini naliona ya kwamba karibu wote walisimama imara juu ya jukwaa lile wakiwasihi wale walioshuka ili wayaache manung’uniko yao; kwa kuwa Mungu ndiye aliyekuwa Mjenzi Mkuii, tena walikuwa wakishindana naye. Waliisimulia kazi ya ajabu ya Mungu, iliyowaongoza hata jukwaa lile lililo imara, na wote wakainua macho yao mbinguni, wakaanza kumtukuza Mungu kwa sauti kuu. Jambo hili liligeuza nia za wale waliokuwa wamenung’unika na kushuka chini. na kwa unvenyekevu wakapanda tena juu ya jukwaa. VK 89.1