Tumaini la Vizazi Vyote

166/307

Wanafunzi hawakutazamia juu ya kuja kwa msalaba

Wanafunzi walikuwa bado wanamtazamia kuwa Yesu atatawazwa kuwa mfalme wa nchini. Waliamini ila walitazamia wakati atakaosimamisha ufalme wake. Wazo ya kwamba, Kristo atakataliwa na watu, na kushitakiwa kama mhaini na kuuawa juu ya msalaba, wazo kama hili halikuingia katika mioyo ya wanafunzi. Basi Yesu lazima awadhihirishie wanafunzi wake mambo hayo ijapokuwa ni ya huzuni. TVV 234.3

Mpaka sasa alikuwa hajawafunulia wanafunzi wake kuhusu mateso na kifo chake. Katika maongezi yake na Nikodemo alikuwa amesema: “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa, ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Yohana 3:14. Lakini wanafunzi hawakuyasikia hayo. Sasa muda umefika, ambao pazia lililofunika mambo ya usoni litafunuliwa. “Tangu wakati huo na kuendelea Yesu alianza kuwafunulia wanafunzi wake, jinsi atakavyokwenda Yerusalemu, na kutesemka kwa mambo mengi mikononi mwa wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na halafu kufa, baadaye kufufuka katika siku ya tatu”. TVV 234.4

Wanafunzi wake walisikiliza kwa mshangao bila kusema neno. Yesu alikuwa amekubaliana na usemi wa Petro kuwa ni Mwana wa Mungu, na sasa kufuatana na maneno yake kuhusu mateso, yalionekana kutofahamika. Petro hakuweza kunyamaza, alimvuta Bwana wake kando akasema kuhusu Mambo haya yapitie mbali Bwana yasiwe karibu nawe”. TVV 235.1

Petro alampenda Bwana wake, lakini Yesu hakumsifu kwa ajili ya kumtakia mema, asipatwe na mateso. Maneno ya Petro hayakuwa na msaada wowote wala ufumbuzi wataabu inayomkabili. Maneno hayo hayakupatana na kujitoa ambako yesu alikuja kuwafundisha watu kwa kielelezo chake mwenyewe. Maneno Petro aliyosema yalikuwa kinyume cha mambo ambayo Kristo alikusudia kuwaonyesha wafuasi wake. Kwa hiyo Mwokozi alipaswa kutamka maneno makali ya kukemea ambayo yalikuwa hayajatoka kinywani mwake. “Nenda nyuma yangu, Shetani! kwani u kinyu;me changu. Maana huko upande wa Mungu, ila upande wa watu”. TVV 235.2