Tangu Sasa Hata Milele

30/257

Huss Alikufa Juu ya Mti (Mti wa kufungia Watu wa Kuchomwa na Moto wanapo kuwa Wahai)

Sasa akachukuliwa. Maandamano makubwa yakafuata. Wakati kila kitu kilikuwa tayari kwa ajili ya moto kuwashwa, mfia dini akashauriwa mioyo tena kuokoa maisha yake kwa kukana makosa yake. “Makosa gani”, akasema Huss, “nitakayokanusha? Najua mimi mwenyewe kwamba sina kosa. Namuita Mungu kushuhudia kwamba yote niliyoandika na kuhubiri ilikuwa na nia ya kuokoa myoyo kutoka zambini na kupotea milele; na, kwa hiyo, `furaha kubwa zaidi nitahakikisha kwa damu yangu ukweli ule ambayo nimeuandika na ku uhubiri.” TSHM 45.1

Wakati nyali za moto zilipowashwa kwa ajili yake, akaanza kuimba, “Yesu wewe Mwana wa Daudi, unihurumie”, na hivyo akaendelea hata sauti yake ikanyamazishwa milele. Mfuasi wa kanisa la Roma mwenye bidii, alipoelekeza mauti ao mateso ya wafia dini Huss, na Jerome, aliyekufa baadaye, akasema: “Walijitayarisha kwa moto kama kwamba walikuwa wakienda kwa karamu ya ndoa. Hawakutoa kilio cha maumivu. Wakati miako ilipopanda, wakaanza kuimba nyimbo; na mara haba ukali wa moto iliweza kukomesha kuimba kwao.” TSHM 45.2

Mwili wa Huss ilipoteketea, majifu yake yalikusanywa na kutupwa katika jito la Rhine na kupelekwa baharini ikiwa kama mbegu iliyotawanyika katika inchi zote za ulimwengu. Katika inchi zisizo julikana bado mbegu ile itazaa matunda mengi y kushuhudia ukweli. Sauti katika nyumba ya baraza la Constance likaamsha minongono ya kusikika miaka yote iliyofuata. Mfano wake utasaidia makundi ya watu wengi kusimama imara mbele ya mateso makali na kifo. Kifo chake kilionyesha wazi ubaya wa Roma. Maadui wa ukweli walikuwa wakisaidia shauri ambalo walikusudia kuangamiza! TSHM 45.3

Lakini damu ya mushuhuda mwengine ilipaswa kushuhudia ukweli. Jerome alikuwa akimshauria Huss kwa uhodari na nguvu, kutangaza kwamba kama ni lazima kwake kuanguka kwa hatari, angeruka kwa kumsaidia. Aliposikia habari ya kufungwa kwa Mtengenezaji, mwanafunzi mwaminifu akajitayarisha kutimiza ahadi yake. Bila ruhusa mwenendo wa usalama akashika njia kwenda Constance. Alipofika, akasadiki kwamba alijiingiza yeye mwenyewe hatarini ya kupotea bila kuwa na namna ya kufanya lolote kwa ajili ya Huss. Akakimbia lakini akafungwa na akarudishwa anapofungwa na minyororo. Kwa kutokea kwake kwa kwanza mbele ya baraza majaribio yake kwa kujibu yalikutana na makelele, “Kwa myako ya moto pamoja naye!” Akatupwa gerezani chini ya ngome na akalishwa mkate na maji. Mateso ya kufungwa kwake yakaleta ugonjwa na kutiisha maisha yake; na adui zake kuogopa kwamba angeweza kuwakimbia, wakamtendea si kwa ukali sana, japo akidumu katika gereza mda wa mwaka moja. TSHM 45.4