Tangu Sasa Hata Milele
Ushindi Ulioonekana Mbele
Katika gereza hii ya chini ya ngome aliona ushindi wa imani ya kweli. Katika ndoto zake aliona Papa na maaskofu wakifuta picha za Kristo alizofananisha kwa ukuta za kanisa ndogo huko Prague. “Njozi hii ilimsumbua: lakini kesho yake akaona wapaka rangi wengi walikuwa wakitumika katika kurudisha picha hizi katika hesabu kubwa na rangi zenye kung’aa. ... Wapaga rangi, ... wakazungukwa na makutano mengi, wakasema kwa nguvu, Sasa Papa na maaskofu waje; hawatayafuta tena kamwe!” Akasema Mtengenezaji, “Sura ya Kristo haitafutwa kamwe. Walitamani kuuharibu, lakini utapakaliwa tena, upya katika mioyo yote na wahubiri bora kuliko mimi mwenyewe.” TSHM 44.2
Kwa wakati wa mwisho, Huss akapelekwa mbele ya baraza, mkutano mkubwa na kungaa--mfalme, watoto wa kifalme, makamu (deputes) ya kifalme, wakuu (cardinals) maaskofu-mapadri, na makundi makubwa. TSHM 44.3
Alipoitwa juu ya hukumu yake ya mwisho, Huss akatangaza makatao yake kuwa hata kana. Kwa kukazia macho mfalme ambaye kwa haya neno lake la ahadi halikutimizwa kamwe, akatangaza: “Nilikusudia, kwa mapenzi yangu, nionekane mbele ya baraza hili, chini ya ulinzi wa watu wote na imani ya mfalme anayekuwa hapa.” Sigismuna akageuka uso kwa haya, namna macho ya wote yaligeuka kumwangalia. TSHM 44.4
Hukumu ilipokwisha kutangazwa, sherehe ya haya ikaanza. Tena akaombwa kukana. Huss akajibu, kwa kugeukia watu: “kwa uso gani, basi, napaswa kuangalia mbinguni? Namna gani naweza kuangalia makutano haya ya watu ambao nimewahubiri injili kamilifu? Sivyo; ninaheshimu wokovu wao zaidi kuliko mwili huu zaifu, ambayo sasa unaamriwa kufa.” Mavazi ya ukasisi yakavuliwa moja kwa moja, kila askofu kutamka laana wakati alipokuwa akitimiliza sehemu yake ya sherehe. Mwishowe, “wakaweka juu ya kichwa chake kofia ao kofia ya kiaskofu ya umbo la jengo la mawe ya kartasi, ambapo sanamu za kuogofya za pepo mbaya zilipakwa rangi, na neno “Mzushi mkuu” yenye kuonekana kwa mbali mbele. “Furaha kubwa kuliko,” akasema Huss, “nitavaa taji la haya kwa ajili ya jina lako, o Yesu. Kwa ajili yangu ulivaa taji la miiba.” TSHM 44.5