Tangu Sasa Hata Milele

23/257

Wycliffe Anakataa Kukana

Lakini Wycliffe hakukana. Pasipo hofu akashikilia mafundisho yake na sukumia mbali mashitaka ya watesi wake. Akaalika wasikilizi wake mbele ya hukumu la Mungu na akupima uzito wa madanganyo na wongo wao katika mizani ya ukweli ya milele. Uwezo wa Roho Mtakatifu ulikuwa juu ya wasikilizaji. Kama mishale kutoka kwa mfuko wa mishale ya Bwana, maneno ya Mtengenezaji yakatoboa mioyo yao. Mashitaka ya upinga dini, waliyoyaleta juu yake, akayarudisha kwao. TSHM 35.2

“Pamoja na nani, munavyo fikiri,” akasema, “munayeshindana naye? na mzee anaye kuwa kwa ukingo wa kaburi? la! pamoja na ukweli-Ambayo unakuwa na nguvu kuliko wewe, na utakushinda”. Aliposema vile, akatoka na hata mtu moja wa maadui zake hakujaribu kumzuia. TSHM 35.3

Kazi ya Wycliffe ilikuwa karibu kutimizwa, lakini mara nyingine tena alipashwa kutoa ushuhuda wa injili. Aliitwa kwa kusikilizwa mbele ya baraza la kuhukumu la kipapa kule Roma, ambalo kila mara lilikuwa likimwanga damu ya watakatifu. Msiba wa kupooza ulizuia safari ile. Lakini ingawa sauti yake haikuweza kusikiwa pale Roma, aliweza kusema kwa njia ya barua. Mtengenezaji akamwandikia Papa barua, ambayo, ingawa ya heshima na kikristo moyoni, ilikuwa kemeo kali kwa ukuu na kiburi kya jimbo la Papa. TSHM 35.4

Wycliffe akaonyesha kwa Papa na maaskofu wake upole na unyenyekevu wa Kristo, muonyesha wazi si kwao tu bali kwa miliki ya Wakristo wote tofauti kati yao na Bwana ambaye wanajidai kuwa wajumbe wake. TSHM 35.5

Wycliffe alitumainia kabisa kwamba maisha yake yangekuwa bei ya uaminifu wake. Mfalme, Papa na maaskofu wakajiunga kwa kutimiza maangamizi yake, na ilionekana kweli kwamba kwa mda wa miezi michache ikiwezekana wangemletea kifo kwa ajili ya imani ya dini. Lakini uhodari wake ulikuwa imara. TSHM 36.1

Mtu ambaye kwa wakati wote wa maisha yake alisimama imara katika kutetea ukweli hakuna mtu wakusumbuliwa kwa ajili ya adui zake. Bwana alikuwa mlinzi wake; na sasa, wakati adui zake walipohakikisha kupata mawindo yao, mkono wa Mungu ukamuhamisha mbali yao. Katika kanisa lake huko Lutterworth, wakati alipotaka kufanya ibada ya meza ya Bwana, akaanguka na kupinga kupooza communion), anakauka viungo, na kwa wakati mfupi akakata roho yake. TSHM 36.2