Tangu Sasa Hata Milele

22/257

Anashambuliwa na Ugonjwa wa Hatari

Lakini kwa gafula kazi zake zikasimamishwa. Ingawa alikuwa hajaeneza miaka makumi sita, taabu isiyokoma, kujifunza, na mashambulio ya maadui yalilegeza nguvu zake nakumfanya aonekane mzee upesi. Akashambuliwa na ugonjwa wa hatari. Watawa walifikiri kwamba atatubu kwa uovu alioufanya kwa kanisa, na wakaenda haraka kwa chumba chake ili wasikilize maungamo yake. “Unakuwa na kifo kwa midomo yako”, wakasema; “uguswe basi kwa makosa yako, na ukane mbele yetu mambo yote uliyosema kwa hasara yetu”. TSHM 33.5

Mtengenezaji akasikiliza kwa utulivu. Ndipo akamwambia mlinzi wake kumuinua katika kitanda chake. Katika kuwakazia macho kwa imara, akasema katika sauti hodari ya nguvu ambayo ilikuwa ikiwaletea kutetemeka mara kwa mara, “Sitakufa, bali nitaishi; na tena nitatangaza matendo maovu ya watawa”. Waliposhangazwa na kupata haya, watawa wakatoka chumbani kwa haraka. TSHM 33.6

Wycliffe aliishi kwa kuweka katika mikono wana inchi wake silaha za nguvu sana kwa kupinganisha Roma-Biblia, mjumbe wa mbinguni waliyewekwa kwa kutoa utumwani, kuangazia na kuhubiri watu. Wycliffe alijua kwamba ni miaka michache tu ya kazi iliyobaki kwake; aliona upinzani aliopashwa kukutana nao; lakini kwa kutiwa moyo na ahadi za Neno la Mungu, akaendelea. Katika nguvu zote zake za akili, na tajiri kwa matendo, alitayarishwa na maongozi ya Mungu kwa jambo hili, kazi yake kubwa kuliko zote. Mtengenezaji katika nyumba yake ya ukasisi huko Lutterworth, alizarau wimbi lililosirika, akajitia mwenyewe kwa kazi yake aliyoichagua. TSHM 34.1

Mwishowe kazi ikatimilika-tafsiri ya kwanza ya Biblia kwa kingereza. Mtengenezaji akaweka katika mikono ya watu wa Kiingereza nuru ambayo haipashwi kuzimishwa kamwe. Alifanya mengi zaidi kuvunja vifungo vya ujinga na kufungua na kuinua inchi yake kuliko ilivyo kwisha kufanyiwa na washindi kwa shamba za vita. TSHM 34.2

Ni kwa kazi ya taabu tu nakala za Biblia ziliweza kuzidishwa. Mapezi yalikuwa makubwa sana kupata kitabu kile, kwa sababu ilikuwa vigumu kwa wenye kufanya nakala kuweza kumaliza maombi ya watu. Wanunuzi watajiri walitamani Biblia nzima. Wengine wakanunua tu kipande. Katika hali nyingi, jamaa zilijiunga kununua nakala moja. Biblia ya Wycliffe kwa upesi ikapata njia yake nyumbani mwa watu. TSHM 34.3

Wycliffe sasa akafundisha mafundisho ya kipekee ya Kiprotestanti-wokovu kwa njia ya imani katika Kristo na haki moja tu ya Maandiko. Imani mpya ikakubaliwa karibu nusu ya Wangereza. TSHM 34.4

Tokeo la Maandiko likaleta hofu kwa watawala wa kanisa. Wakati ule hapakuwa na sheria katika inchi ya Uingereza ya kukataza Biblia, kwa sababu ilikuwa haijaandikwa bado katika lughanyingine. Sheria za namna ile zilifanyika baadaye na zikakazwa kwa nguvu. TSHM 34.5

Tena waongozi wa papa wakafanya shauri mbaya kwa kunyamazisha sauti ya Mtengenezaji. Kwanza, mkutano wa waaskofu ukatangaza maandiko yake kuwa ya kupinga mafundisho ya dini. Walipovuta mfalme kijana, Richard II, upande wao, wakapata agizo la kifalme kufunga wote wanaohukumu mafundisho yaliyokatazwa na Roma. TSHM 34.6

Wycliffe akaitwa toka kwa mkutano kwenda kwa baraza kuu la taifa (parlement). Kwa uhodari akashitaki serkali ya Kanisa la Rome mbele ya baraza la taifa na akaomba matengenezo ya desturi mbaya zilizotolewa na kanisa. Adui zake wakakosa lakufanya. Ilikuwa ikitazamiwa kwamba Mtengenezaji, katika miaka yake ya uzee, peke yake bila rafiki, angeinama kwa mamlaka ya mfalme. Lakini baadala yake, Baraza likaamsha na mwito wa kugusa moyo uliofanywa na ghasia (makelele) za Wycliffe, ukavunja amri ya kuteso, na Mtengenezaji alikuwa huru tena. TSHM 34.7

Mara ya tatu aliletwa hukumunu, na mbele ya mahakama makuu ya Kanisa ya kifalme. Hapa sasa kazi ya Mtengenezaji itasimamishwa. Hii ilikuwa mawazo ya wafuasi wa Papa. Kama walitimiza kusudi zao, Wycliffe atatoka katika nyumba ya hukumu na na kuelekea kwenye nyali za moto. TSHM 35.1