Pambano Kuu

62/261

11/Wakuu Wakataa

Moja ya shuhuda bora kabisa zilizotolea kuhusu Matengenezo ilikuwa ushuhuda uliotolewa na watawala wa Ujerumani katika mkutano uliofanyika huko Spires katika mwaka 1929. Ujasiri na ushujaa wa watu hao wa Mungu ulipata uhuru wa dhamiri wa kudumu kwa ajili ya vizazi vijavyo, na kulipatia kanisa la matengenezo jina la “Protestant” TU 91.1

Mungu alikuwa amezuia majeshi ya upinzani ambayo yalikuwa yanapinga ukweli. Charles V alikazana kuangamiza matengenezo lakini kila mara alipounyosha mkono wake ili atende madhara, alilazimika kwa njia fulani kutotenda kitu. Tena na tena wakati ilipoonekana hatari kuu inakabili Matengenezo, majeshi ya uturuki yalionekana kwenye mpaka, au majeshi ya ufaransa, au papa mwenyewe alipingana nayo. Hivyo basi katikati ya misukosuko na ghasia za mataifa, matengenezo yalizidi kuwa imara na kuenea. TU 91.2

Walakini mwishowe utawala wa papa ukalifanya jambo la kupinga watengenezaji kuwa jambo la kawaida. Mfalme aliitisha baraza likutane huko Spares katika mwaka wa 1529 ili kupanga jinsi ya kuangamiza uzushi. Kama njia za kawaida amani zingeshindwa, Charles alikuwa tayari kutumia nguvu yaani silaha. TU 91.3

Wafuasi wa papa katika baraza la Spires walidhihirisha wazi uadui na chuki yao juu ya watengenezaji. Melanchton alisema, “Tumekuwa machukizo na takataka katika ulimwengu, lakini Kristo atatazama hapo chini kwa watu wake maskini, na atawatunza”. Watu wa Spires wakiwa na kiu ya Neno la Mungu walifurika katika kanisa, bila kujali vizuizi vilivyowekwa ili kufanya ibada halali. Jambo hili liliharakisha hatari. Uhuru wa dini ulikuwako kisheria, na wainjilisti walikusudia kuwaondolea haki yao ya uhuru wa dini. Mahali pa Luther palikuwa pameshikwa na watendakazi wengine, na wakuu ambao Mungu aliwainua ili kulinda kazi hii. Fredrick wa Saxony alikuwa amefariki, lakini Duke John aliyewekwa badala yake aliyakaribisha Matengenezo na kuyaunga mkono. TU 91.4

Makasisi walidai kwamba majimbo ambayo yamekubali matengenezo yafanyike kwao lazima yasalimu amri na kukubali uamuzi wa Kiroma. Watengenezaji wa upande wao wasingekubali hata kidogo kuwa majimbo yaliyopokea Neno la Mungu yawekwe chini ya utawala wa Roma. TU 91.5

Mwisho ilikusudiwa kuwa, pale ambapo matengenezo hayajafanyika, sheria ya Worms itumike; na kwamba pale ambapo watu hawafuati matengenezo bila hatari ya kuasi na miisho ya misa, wala wasiruhusu Roman Catholic kuwaingilia watu wa Luther. Wakuu waliamua hivyo. Uamuzi huo uliwaridhisha makasisi na maaskofu. TU 91.6