Pambano Kuu

20/261

5/ Nuru Yapambazuka Uingereza

Mungu hakuacha neno lake liharibiwe kabisa. Katika nchi kadhaa wa kadhaa za Ulaya watu waliamshwa na roho wa Mungu ili watafute ukweli kama watafutavyo hazina iliyosetirika. Hasa wakielekea kwenye Neno Takatifu la Biblia, walikuwa tayari kulifuata bila kujali vitisho. Ingawa hawakuuelewa ukweli wote. Waligundua mambo mengine yaliyofichwa kwa muda mrefu. TU 30.1

Wakati ulikuwa umefika ili neno la Mungu liweze kutolewa kwa lugha za watu, kila mtu lugha yao. Ulimwengu ulikuwa umekaa gizani, na sasa mapambazuko yalikaribia. TU 30.2

Katika karne ya kumi na nne, nyota ya asubuhi ya matengenezo ya kanisa ilitokea katika Uingereza. John Wycliffe alionekana katika chuo kikuu kuwa mcha Mungu sana na mwenye akili. Chuoni alijifunza utaalamu wa sheria na mambo ya dini. Mambo hayo yalimwandaa kwa kazi kubwa iliyokuwa mbele yake na uhuru wa dini. Alikuwa na elimu nzuri na kanuni imara. Hali hiyo ilimpatia heshima kwa rafiki zake na adui zake pia. Maadui zake walishindwa kudharau kazi ya matengenezo ya kanisa aliyokuwa akishughulikia, kwa ajili ya ujinga waliokuwa nao. Wycliffe alipokuwa angali mwanafunzi chuoni alikuwa akijifunza maandiko matakatifu. Wycliffe aliona upungufu mwingi sana ambavyo hakuweza kupata mahali pa kumridhisha. Katika neno la Mungu alipata jawabu la haja yake ambayo ameitafuta sana bila mafanikio. Hapa katika Biblia ndipo aliona kuwa Kristo ndiye Mwombezi wa pekee wa binadamu. Kwa hiyo alikusudia kuitangaza kweli hiyo aliyogundua. TU 30.3

Wycliffe hakuanza kazi hiyo na upinzani na Rumi mara moja. Lakini kwa kadiri alivyozidi kuona wazi makosa ya mapapa, ndivyo alivyoweza kufundisha ukweli hasa kama ulivyo katika Biblia. Aliona kuwa Rumi imekataa kufuata Biblia, ila inafuata hadithi za kibinadamu tu. Aliwalaumu mapadri kwamba hawafuati Biblia. Akasema kwamba Biblia lazima ifundishwe kwa watu na kufuatwa kama katika kanisa. Alikuwa mhubiri hodari, na maisha yake yalishuhudia mambo yale aliyohubiri. Ujuzi wake wa maandiko matakatifu, maisha yake ya utawa, na ujasiri wake, vilimpatia usikizi wa watu wote. Watu wengi waliona makosa ya kanisa la Rumi. Wakaikubali wazi kweli iliyohubiriwa na Wycliffe, lakini waongozi wa mapapa walijazwa na ghadhabu; wakasema, mtu huyu anapata heshima kuliko yetu. TU 30.4