Pambano Kuu

19/261

Rumi Yaazimu Kuwaadhibu Waldenses

Sasa ulianzishwa mpango hatari wa kuwasaka watu wa Mungu katika maficho yao ya milimani. Wapelelezi waliwekwa ili kuwachunguza, Basi mara kwa mara, na tena na tena walishambuliwa na kuvurugwa. Makao yao na makanisa yao yaliharibiwa. Watu hawa hawakupatikana na uhalifu wa aina yoyote, isipokuwa walishitakiwa, eti kuwa ibada yao haifuati taratibu za papa. Na adhabu ya kosa hilo ilikuwa mateso makali mno ya ukatili usiosemeka. TU 28.2

Rumi ilipoazimu kuliondolea mbali dhehebu hilo la Wakristo wa Waldenses, tangazo lilitolewa na papa kuwa watu hawa wahesabiwe kuwa wazushi, na hukumu yao ni kuchinjwa. Hawakushitakiwa kwa kosa la uvivu, au uhaini au watangatangaji, bali walishitakiwa kwa kosa la uzushi, wenye kupotosha kondoo, kutoka katika zizi la kweli. Tangazo hilo lilitaka washiriki wote wa kanisa la Rumi kuhusika na kazi ya kuwaharibu wazushi hao. Kivutio kilichowekwa ni kwamba Wote wa watakaoshiriki kazi hiyo watakuwa huru kwa kila jambo wanalodaiwa, kama walikuwa na kesi yoyote iliyofanywa na watu wa Vaudois ilifutwa, na watu wote walikatazwa kutoa msaada wa aina yoyote kwao. Watu wakaruhusiwa kuwanyanga'anya mali zao bila kizuizi. Tangazo hili lilidhihirisha ghadhabu ya joka, wala siyo sauti ya Kristo. Roho ile ile ilimsulubisha Kristo na kuwaua mitume, roho ya kikatili ya Nero kwa watu wa Mungu, ndiyo hiyo iliyowaongoza kuwaangamiza watu wapendwa wa Mungu. TU 28.3

Ingawa mipango ya kuwaangamiza ilikuwa ikitekelezwa lakini watu hawa hawakuacha kutumia wahubiri ili kuendeza ukweli wa Biblia. Waliwindwa sana na kuuawa, lakini damu yao ilikuwa ndiyo maji ya kuotesha mbegu ya Injili. TU 28.4

Hivyo ndivyo Waldenses walivyomshuhudia Mungu Kabla Martin Luther hajatokea. Walipanda mbegu ya matengenezo ya kanisa yaliyoanza siku za Wycliffe yakakuwa mpaka wakati wa Luther, na yataendelea mpaka mwisho wa wakati. TU 29.1

Marejeo: TU 29.2

J.H. Merle D'Aubigne — History of Reformation of Sixteenth Century, book 17, chap. 2 TU 29.3

Wylie, book 1 chap 7. TU 29.4

Ibid, book 16, chap. 1. TU 29.5