Pambano Kuu

226/261

36/Mapambano Yaliyo Karibu Sana

Tangu mwanzo wa mapambano huko mbinguni, limekuwa azimio la shetani kuharibu sheria ya Mungu na kuondoa. Haidhuru ama ni kuindoa sheria yote nzima, au kukataa kutambua sehemu moja tu ya sheria, matokeo ni yale yale. Mtu avunjaye sehemu moja ya seria hudhihirisha nia yake ya kuvunja sheria nzima, maana mvuto wake na kielelezo chake huelekea upande wa kuasi. Basi “amekosa juu ya yote” Yakobo 2:10. TU 284.1

Shetani amepotosha mafundsiho ya Biblia, kwa hiyo makosa yamefanywa na watu maelfu katika ukristo wao. Pamoja na mwisho baina ya ukweli na uovu ni kuhusu sheria ya Mungu, baina ya mafundisho ya Biblia na sehemu ya dini. Biblia inaweza kufikiwa na watu wote lakini ni watu wachache tu wanaoikubali Biblia kuwa ndiyo kiongozi wa maisha yao. Katika kanisa wengi hukataa misingi au nguzo za imani ya Kikristo, yaani uumbaji, anguko la mwanadamu dhambini, upatanisho na sheria ya Mungu. Nguzo hizi zimekataliwa, yote au sehemu yake. Wengi huona kuwa ni udhaifu tu kuitegemea Biblia peke yake. TU 284.2

Ni vyepesi kufanya sanamu ya mafundisho ya uongo, sawasawa na kufanya sanamu za kuchonga. Kule kumweleza Mungu kwa njia potofu, yaani kuitafsiri tabia yake vibaya, shetani huwaongoza watu kwa njia potofu. Sanamu ya wenye elimu inatwalishwa na kuabudiwa, badala ya kumwabudu Mungu. Kama anavyofunuliwa katika Neno Lake, na katika Kristo, na katika kazi zake za kuumba Mungu na wenye elimu, watungaji wa mashairi, wana siasa, waandishi wa magazeti, wa vyuo vikuu vingi, hata vyuo vya kufunza mambo ya dini, anazidi Baali kidogo tu, mungu jua ambaye ni mungu wa Wafoeniki kama ilivyo siku za Eliya nabii. TU 284.3

Hakuna kosa la ujasiri kabisa kuhusu mamlaka ya Mungu lenye matokeo ya hatari zaidi kuliko kosa la kufundisha kuwa sheria ya Mungu imefutika. Tuseme kuwa, wachungaji mashuhuri wahubiri waziwazi kuwa, sheria ya mtawala wa nchi yao haina ulazima kuishika, kwamba inazuia uhuru wa watu, kwa hiyo haina lazima ya kutiiwa. Je, mtu kama huyu angevumiliwa muda gani aendelee kufundisha hivyo? TU 284.4

Hata hivyo ingekuwa rahisi kama taifa kuondoa sheria zao kuliko mfalme wa malimwengu kutangua sheria yake. Jaribio la kuziepuka sheria za Mungu lilifanywa ufaransa, wakati nchi ilipotawaliwa na makafiri. Ilionekana kuwa kuondoa ua wa ulinzi uliowekwa na Mungu, na kukubali kuweka nchi hiyo mikononi mwa utawala wa mfalme wa uovu. TU 284.5