Pambano Kuu

205/261

Ushahidi Utoshao

Mungu ametoa ushahidi utoshao katika Neno lake kuonyesha tabia yake halisi, walakini mawazo hafifu ya binadamu hayawezi kufahamu mawazo ya Mungu. “Jinsi zilivyokuu, tajiri, hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani” Warumi 11:33. Tunaweza kuufahamu upendo wa Mungu kwa uwezo wake tu. Baba yetu wa mbinguni atatufunulia kadiri ya vile inavyotufaa, ili tuweze kufahamu zaidi ya hayo tumtumaini tu. TU 257.4

Mungu hawezi kuondoa udhuru wa kutoamini. Wanaotafuta vichaka vya kujificha ili wasiamini watavipata. Na wale wanaotoa vikwazo vyote viondoke kwanza ndipo waamini, hawatafikia nuru. Roho isiyoongoka ni adui wa Mungu. Lakini imani inayochochewa na Roho Mtakatifu itastawi. Hakuna mtu atakayeimarisha imani yake bila kujitahidi. Watu wakijilegeza, mashaka yatawagharikisha. TU 257.5

Wala wenye mashaka, wasiamini humdharau Kristo. Wao ni miti isiyozaa, na huzuia miti mingine isipate nuru huwafunika na majani yao yanayozuia mwanga wa jua usiwafikie. Maisha ya watu hawa watawashuhudia kama watu wasiofaa. TU 258.1

Kuna njia moja ya kufuata kwa wale wenye mashaka. Badala ya kushughulika na mambo ambayo hawayajui wakazanie nuru ile waliyokwishaangaziwa na ndipo watapokea nuru zaidi. TU 258.2

Shetani ataleta vitu vinavyofanana na ukweli ili uwapotoshe wenye mashaka. Lakini hawezi kamwe kumpotosha mtu mtafuta ukweli kwa uaminifu. Kristo ndiye kweli, “Nuru inayomwangazia kila mtu ajaye ulimwenguni” “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake atajua habari ya yale mafunzo.” Yohana 1:9; 7:17. TU 258.3

Bwana huwaruhusu watu wake waingie majaribuni, si kwa kuwa anapendezwa iwe hivyo, ila kwa sababu ni muhimu kwao kwa ajili ya ushindi wao wa mwisho. Angetaka kuwaficha wasiingie majaribu kwa utukufu wake, lakini hafanyi hivyo, kwa kuwa majaribu huwaandaa kushindana na hali zote za uovu. Hakuna kitakachowatenga na Mungu, wale wanaomtumaini kamili. Hakuna kitu, shetani au wanadamu waovu hawetaweza kuwatenganisha na Mungu. Kila jaribu la wazi au la siri linaweza kushindwa, “si kwa ushujaa au kwa nguvu, bali kwa Roho yangu, asema Bwana wa majeshi”. Zekaria 4:6. TU 258.4

“Ni nani atakayewadhuru, iwapo mnafuata mambo ya kweli na yaliyo mema?” 1 Pet. 3:13. Shetani anajua kuwa mtu mnyonge anayemtumaini Kristo, huwa na nguvu kuliko majeshi yote ya mwovu. Kwa hiyo hutafuta kuwatoa askari wa msalaba watoke katika ngome yao, aliwashawishi kutoka apate kuwaaangamiza wote watakaothubutu kutoka. Kuambatana na Mungu na kushikilia ari zake tu, ndipo tutakuwa salama. TU 258.5

Hakuna mtu atakayekuwa salama kwa siku au saa bila maombi. Msihi Bwana akupe hekima ujue Neno lake. Shetani ni hodari kusoma Maandiko, akiyatafsiri kama aonavyo, hasa sehemu anazoona kuwa zitakunasa. Tunapasa kujifunza kwa unyenyekevu na kuomba, wakati wote katika imani, ili tupate kujua hila za shetani. Ombi letu na liwe: “Usitutie majaribuni” Mathayo 6:13 TU 259.1