Pambano Kuu

197/261

31/Roho Chafu

Malaika wa Mungu na malaika wa Shetani yaani roho wachafu, huelezwa dhahiri katika Maandiko Matakatifu nao wamejihusisha katika Historia ya wanadamu. Malaika watakatifu ambao huwahudumia wale watakaorithi wokovu, (Waebrania 1:14) hudhaniwa na wanadamu kuwa ni roho za wafu. Lakini maandiko hueleza wazi kuwa hawa sio zo roho za wafu. TU 249.1

Kabla mtu hajaumbwa, malaika walikuwako, kwa maana wakati msingi wa dunia ulipowekwa, “nyota za asubuhi ziliimba pamoja, na wana wa Mungu walipinga kelele za shangwe”. Ayubu 38:7. Badala ya kuanguka kwa mwanadamu dhambini, malaika walitumwa ili kuulinda mti wa uzima kabla mtu hajafa. Malaika wanawazidi wanadamu maana mwanadamu alifanywa “mdogo punde kuliko malaika” Zab. 8:5 TU 249.2

Nabii husema, “Nilisikia sauti za malaika wengi pande zote za kiti cha enzi” mbele ya mfalme wa wafalme malaika hawa walikuwa tayari ili, “Mtendao neno lake”. Na “Kusikiliza sauti yake” “wasiohesabika” Ufunuo 5:11; Zaburi 103:20-21; Ebr. 12:22. Wao huenda huko na huko kama watumishi wa Mungu. Huruka kama umeme mbio yao ni ya ajabu. Malaika aliyeonekana kwenye kaburi la Mwokozi, uso wake ulikuwa kama “umeme” aliwafanya walizi wazimie kama wafu. Wakati mfalme Senakeribu aliomkufuru Mungu na kutisha Wana wa Israeli, malaika wa Bwana akatoka na kuwapiga Waashuri katika matuo yao watu mia na themanini na tano elfu. Ezekieli 1:14; Mathayo 28:3-4; 2Fal. 19:35. TU 249.3

Malaika wa Mungu hutumwa kwa kazi nzuri kuhusu watu wa Mungu. Kwa Ibrahimu walileta ahadi za mibaraka; huko Sodoma kumwokoa Lutu katika ajali; kwa Eliya, alipokuwa karibu kuangamia jangwani: kwa Elisha, katika gari la moto na farasi wa moto; alipozungukwa na adui; kwa Danieli, alipotupwa tunduni mwa simba; kwa Petro, alipofungwa na Herode ili auawawe, kwa wafunga wa Filipi kwa Paulo, katika dhoruba kali baharini; kwa Kornelio ili kufungua mawazo yake apokee Injili: kwa Petro, kupewa ujumbe wa wokovu kwa mataifa. Hivyo ndivyo malaika wa Mungu wanavyowahudumia watu wa Mungu. TU 249.4