Pambano Kuu

182/261

28/Kukubalika Kumbukumbu ya Maisha yetu.

“Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye Mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji na nywele za kichwa chake kama sufi safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto; na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa” Daniel 7:9-10. TU 232.1

Haya ndiyo maono aliyopewa Daniel ya siku ile kuu ya hukumu ambayo maisha ya kila mtu yatakapopitishwa katika uchunguzi wa Hakimu wa dunia yote. Mzee wa siku ni Baba Mungu. Yeye ambaye ndiye asili ya maisha yote ya kila kitu, chemichemi ya sheria zote, ndiyo atakuwa mwenye kiti katika hukumu. Na malaika watakuwa wahudumu na mashahidi. TU 232.2

“Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja na mawingu ya mbinguni akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” Daniel 7:13-14. TU 232.3

Kuja kwa Kristo kunakoelezwa hapa siko kurudi kwake mara ya pili duniani. Anakuja kwa Mzee wa siku huko mbinguni ili kupokea ufalme atakaopewa mwisho wa kazi yake ya uombezi. Kuja huko ndiko kulitokea mwaka 1844, wala si kurudi duniani mara ya pili. Hivyo ndiyo ilikuwa mwisho wa unabii wa siku 2300. Kuhani wetu Mkuu anaingia katika patakatifu pa patakatifu ili kufanya kazi yake ya mwisho ya kuwaombea wanadamu. TU 232.4

Katika huduma ya hema takatifu hapa duniani, watu ambao dhambi zao zilihamishiwa kutoka patakatifu, ndivyo waliofaidi siku ya upatanisho. Hali kadhalika katika siku kuu ya uchunguzi wa mwisho, watu ambao yao yataangaliwa ni wale watu wa Mungu tu. Hukumu ya waovu itakuwa wakati mwingine. “Hukumu lazima ianzie katika nyumba ya Mungu” 1Petro 4:17. TU 232.5

Vitabu vya kumbukumbu vya mbinguni vitahusika na uamuzi wa kesi ya kila mtu. Kitabu cha uzima kimeandikwa majina ya watu wote walioingia katika huduma ya Mungu. Yesu aliwaagiza wanafunzi wake, “Furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni”. Paulo anasema kuhusu wakazi wenzake, “ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima” Danieli asema kuwa watu wa Mungu wataokolewa, “Kila mmoja atakayeonekana ameandiwa kitabuni” Na mwandishi wa ufunuo “asema kuwa wale watakaoingia katika mji wa Mungu, ni wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana Kondoo” Luka 10:20 Wafilipi 4:3; Danieli 12:1; Ufunuo 21:27. TU 232.6

Katika kitabu cha ukumbusho yamo majina ya matendo mema ya wale wamchao Bwana, na kulitafakari jina lake; Kila jaribu linapingwa, kila uovu unashindwa, kila neno la fadhili linalosemwa, kila tendo la kujinyima, na kila tendo la kusikitisha lililovumiliwa, kwa ajili ya Kristo, huandikwa. “Umehesabu kutangatanga kwangu, uyatie machozi yangu katika chupa yako. Je, hayamo katika kitabu chako?” Malaki 3:16; Zaburi 56:8. TU 233.1