Pambano Kuu

174/261

Sabato ya Kweli Ilishikwa Daima

Tangu siku hiyo mpaka leo Sabato imekuwa ikishikwa. Ingawa mtu wa dhambi amefaulu kuikanyaga sabato ya Bwana chini ya miguu yake, walakini watu waaminifu wa Mungu wamekuwa wakiitunza kwa siri hapa na pale. Tangu wakati wa matengenezo, watu wa kila kizazi wamekuwa wakiitunza wakati wote. TU 220.2

Ukweli huu wa sabato pamoja na Injili ya milele vitawapambanua watu wa kweli wa Mungu, na kanisa la kweli na wapotovu mpaka Kristo arudi. “Hapa ndipo penye uvumilivu wa watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu” Ufunuo 14:12 TU 220.3

Wale waliopata nuru ya hema takatifu na huduma zake na kuona sheria ya Mungu walijazwa na furaha na kuona jinsi ukweli unavyoungana bila kasoro. Walitamani kuwafikishia wakristo wote nuru hii. Lakini ukweli huu wa aina mbali mbali haukukubaliwa na walimwengu; hasa wale wanaojiita kuwa ni wafuasi wa Kristo. TU 220.4

Wakati madai ya Sabato yaliposisitizwa wengi walisema “Tumekuwa tukishika Jumapili tangu zamani, na kwamba baba zao walitunza pia, na watu wengi watauwa walikufa wakifurahi katika utunzaji wake. Kuanza kutunza sabato hii mpya kutatutenga na waengine ulimwenguni. Kikundi kidogo cha watu wanaotunza Sabato ya Jumamosi watafanya nini kulinganisha watu wote wanaoshika Jumapili katika ulimwengu?” mambo kama hayo yalifanywa na Wayaudi pia siku za Kristo, ndiyo sababu walimkataa na mafundisho yake. Hali kadhalika na wakati wa Luther, wafuasi wa Rumi walibisha wakisema kuwa watu wengi watauwa wamefia katika imani ya Rumi, kwa hiyo dini hiyo ilitosha kabisa, haina hitilafu. Mambo kama hayo ndiyo yatakayopinga maendeleo yote ya matengenezo katika imani. TU 220.5

Wengi walidai kuwa kushika siku ya Jumapili kumeenea sana duniani, na kumekuwa kawaida ya makanisa kwa karne nyingi. Lakini upinzani wa jumapili ulielezwa kuwa sabato ni ya zamani kabisa, nayo imeshikwa hivyo tangu zama za kale. Ni ya zamani, umri wake ni kama wa ulimwengu. Ilianzishwa na Mzee wa siku, yaani Mungu. TU 220.6

Mbali na maelezo ya Biblia, wengi hubisha na kusema “kwa nini watu wengi wakuu, maarufu hawaitambui sabato hiyo? Ni wachache tu wanaoishika. Haiwezekani kwamba ninyi mkawa sawa na wengine wote wakakosea; na hali ni watu wataalamu, wenye ujuzi mkubwa!” TU 220.7

Ili kukomesha mabishano hayo ilikuwa lazima kuchunguza maandiko Matakatifu kuhusu mpango wa Mungu na jinsi anavyotendea watu katika vizazi vyote. Sabato inayofanya Mungu asiwachague watu wakuu na wenye elimu, ili kuongoza watu wake, ni kwa kuwa wao hawamtegemei, ila tu hutegemea ukuu na elimu yako, na kujiona kuwa hawana haja ya kuongozwa naye. Watu ambao wanao ujuzi mdogo, huitwa mara kwa mara ili waeneze neno lake, si kwamba kutoelimika kwao ndiko kunampendeza Mungu, bali katika hali yao huwa hawana la kujisifia wasifundishwe na Mungu. Unyenyekevu wao na utii huwafanya kuwa wakuu. TU 221.1

Historia ya Waisraeli wa kale inatuwekea kielelezo cha kushangaza sisi wa Marejeo. Mungu aliwaongoza watu wake wa Marejeo sawasawa alivyowaongoza Waisraeli kutoka Misri. Kama wale waliofanya kazi mwaka 1844 wangaliupokea ujumbe wa malaika wa tatu, na kuutangaza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ulimwengu ungekuwa umeonywa zamani, na Kristo angekuwa amekuja kuokoa watu wake. TU 221.2