Pambano Kuu

151/261

23/Kufunua Siri ya Patakatifu

Maandiko ambayo yamekuwa msingi na kiini cha imani ya watu wa marejeo (Waadventista) kuliko yote ni yale yasemayo, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakasika” Daniel 8:14. Usemi huu umekuwa ukijulikana sana miongoni mwa wale waliokuwa wakikutazamia kurudi kwake Bwana kuliko karibu. Lakini Bwana hakutokea. Waumini walifahamu kuwa Neno la Mungu halina kasoro, ni lazima walivyoutafsiri unabii, andiko kuna makosa. Lakini basi kosa lilikuwa wapi? TU 196.1

Mungu amewaongoza watu wake katika mkusanyiko mkuu wa marejeo. Na wala asingewaacha wamalizikie gizani, katika huzuni kuu na kushutumiwa kwa aibu; kana kwamba ni wahuni tu wanaotangatanga. Ingawa wengi waliacha msimamo wao wa kuutafsiri unabii, na kukanusha imani ya wale walioambatana nao, lakini wengine hawakuikana imani ambayo inathibitishwa na Maandiko na Roho wa Mungu. Ilikuwa wajibu wao kushikamana na ukweli walioupata. Walijifunza maandiko kwa bidii na kwa maombi ili wapate kugundua kosa lao. Kwa kuwa kwa upande wa kuhesabu miaka ya unabii hawakuona kosa lolote. Waligeukia fundisho lihusulo patakatifu. TU 196.2

Wakagundua kwamba hakuna andiko lolote linalosema kuwa dunia hii ndiyo patakatifu, kama wengi wanavyoamini. Bali waligundua maelezo tele kuhusu patakatifu, asili yake na mahali pake pamoja na huduma zake, kama isemavyo: “Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida zake za ibada, na patakatifu pake pa kidunia. Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya wonyesho ndipo palipoitwa patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo patakatifu pa patakatifu yenye chetezo cha dhahabu sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; na juu yake Makerubi ya utukufu yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari ya vitu hivi kimoja kimoja” Waebrania 9:1-5. TU 196.3

Patakatifu palikuwa ni hema iliyojengwa na Musa, kwa agizo la Mungu kuwa mahali patakatifu pa kukaa Mungu. “Na wanifanyie patakatifu, ili nipate kukaa kati yao” Kutoka 25:8. Hivyo ndivyo Musa alivyoagizwa. Patakatifu na patakatifu pa patakatifu, vyumba hivyo vilitengwa na pazia. Na pazia kama hilo lilifunga mlango wa chumba cha kwanza. TU 196.4