Pambano Kuu

138/261

Kukataa Nuru kwa Mwanadamu

Giza la kiroho lilikuwa ndani yao, si kwa sababu wanadamu wamekataa nuru ya Mungu. Wayahudi walipojitia katika mambo ya ulimwengu na kumsahau Mungu, waliachwa gizani wala wasitambue kuzaliwa kwa Masihi. Na kwa kutokuamini kwao walimkataa Mwokozi. Mungu hakuwa na kusudi la kuwakatilia mbali na wokovu, bali wao wenyewe ndio walijikatilia mbali. “Wale wanaoikataa kweli hugeuza giza kuwa nuru, na nuru kuwa giza”. Isaya 5:20. TU 181.1

Baada ya kuikataa Injili, Wayahudi waliendelea kuadhimisha mambo yao ya mfano wa dini, ambavyo sivyo yalivyo, huku wakikubali wazi kuwa Mungu hayumo kati yao. Unabii wa Danieli ulionyesha dhahiri wakati wa kuja kwa Masihi na wa kufa kwake pia. Hawakushughulika kujifunza unabii huo, na mwishowe viongozi wao wakalaani mtu yeyote anayejaribu kuweka muda wa tokeo hilo. Katika upofu wao na kutokuamini kwao Waisraeli waliendelea kuuupuza wokovu wao kwa mfuatano wa vizazi. Hawakuona hatari yo yote ya kuikataa nuru ya Injili iliyokuwa bahati yao, ambayo ni nuru ya mbinguni. TU 181.2

Mtu anayeshupaza shingo yake asifanye wajibu umpasao, mwishowe atapotewa na uwezo wa kupambanua baina ya kweli na makosa, ndipo atatengana na neema ya mbinguni hubaki katika giza, imani hupoa na upendo wao hupoa pia, na mafarakano hutokea. Makanisa hushughulikia mambo yao ya ulimwengu tu, na wenye dhambi hushupaa wasione haja ya kutubu. TU 181.3