Pambano Kuu

127/261

20/Upendo kwa Kurudi Kwake Yesu

Mwamko mkuu wa kidini ulitangazwa katika ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14. Malaika alionekana akiruka katikati ya mbingu, “mwenye injili ya milele ili awahubiri watu wakaao duniani, watu wa kila taifa, na kabila na lugha na jamaa”. Akisema kwa sauti kuu, “Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyefanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji. Ufunuo 14:6-7. TU 170.1

Malaika anafananishwa na nguvu na uwezo wa ujumbe utakaotangazwa na kukamilishwa. Kule kuruka kwa malaika katikati ya mbingu, na sauti kuu, na kutangazia watu wa kila taifa, na kabila na lugha na jamaa huonyesha wepesi wa kuendesha kazi na watu wahusikao. Wakati watu hao watakapotoka na kuanza kazi, watatangaza hukumu itakayoanza. TU 170.2

Ujumbe huu ni sehemu ya Injili itakayohubiriwa wakati wa mwisho tu, ambapo saa ya hukumu imekuja kwa hakika. Sehemu hiyo ya ujumbe uhusuo wakati wa mwisho, Danieli aliambiwa aufunge, mpaka wakati wa mwisho”. Daniel 12:4. Ujumbe huu wa hukumu ambao utahubiriwa wakati wa mwisho, haukutimilika wakati mwingine mpaka wakati huo, kama unabii ulivyotabiri. TU 170.3

Paulo alilionya kanisa la wakati wake kuwa, lisikutazamie kurudi kwa Kristo wakati huo mpaka uasi mkuu utakapotokea, na “mtu wa dhambi” kushika uongozi wa kanisa kwa muda mrefu, ndipo tutakutazamia kurudi kwa Bwana. 2Wathesalonike 2:3. “Mtu wa dhambi” — “pia siri ya kuasi” “Mwana wa uharibifu” — ni upapa, ambao ulijitwalia mamlaka ya kuongoza dini kwa muda wa miaka 1260. Muda huo ulimalizika mwaka 1798. Kurudi kwa Kristo kusingeweza kutokea kabla ya muda huo. Paulo alijumlisha kipindi chote cha ukristo mpaka mwaka 1798. Tangu wakati huo kurudi kwake Yesu kunaweza kutangazwa. TU 170.4

Kabla ya wakati huo ujumbe wa aina hiyo haukutangazwa. Kama tuonavyo, Paulo hakukutangaza kurudi kwa Yesu, ila alionyesha kuwa kurudi kwa Bwana kungali mbali. Watengenezaji wa kanisa hawakuhubiri kurudi kwa Bwana. Martin Luther alisema kuwa kurudi kwa Yesu kunaweza kutokea baada ya miaka 300 tangu wakati wake. Lakini tangu mwaka 1798 kitabu cha Danieli kilifunguliwa, kwa hiyo watu wengi walianza kuhubiri saa ya hukumu. TU 170.5