Pambano Kuu

109/261

Ujumbe Ulitolewa na Wanyenyekevu

Kama Wasomi na wataalamu, wachunguzi wa maandiko, wangelikuwa waaminifu na wacha Mungu, ambao wanasoma Biblia kwa roho ya maombi na unyenyekevu wa kweli, wangelifahamu wakati. Unabii ungeeleweka kwao, na mambo yaliyotabiriwa kuwa yatatokea yasingaliwakuta gizani. Lakini basi ujumbe haukutolewa na wasomi hao, bali ulitolewa na watu duni, wanyenyekevu tu. Wale walipuuza kushikilia nuru iliyokuwa karibu nao, waliachwa gizani. Lakini Mwokozi alisema “Anifuataye mimi hatakwenda gizani, bali atakuwa na nuru ya uzima” Yohana 8:12. Mtu wa aina hiyo nuru ya mbinguni itamwongoza kwenye kweli yote. TU 147.1

Wakati Kristo alipokuja mara ya kwanza kuzaliwa makuhani waandishi waliokuwa katika mji mtakatifu ingelipasa wafahamu ishara na kutangaza kuzaliwa kwake. Mika alitaja mahali atakapozaliwa atakapozaliwa, Daniel naye akataja wakati atakapozaliwa. Mika 5:2; Daniel 9:25. Waongozi wa Kiyahudi hawakuwa na udhuru wo wote, kwa kutojua kwao. TU 147.2

Wazee wa Israeli, kama wangalitia nia kusoma unabii wangekuwa mahali, na wakati wa kuzaliwa kwa Kristo, ambako lilikuwa tukio kuu ulimwenguni; kuja kwa Mwana wa Mungu ulimwenguni. Lakini katika mji wa Bethlehemu wasafiri wawili waliochoka sana kutoka Nazareth walikuwa wakipitia kinjia mahali pa kulala usiku. Hakuna nyumba iliyokuwa tayari kuwakaribisha. Mwisho wakaingia katika kibanda kibovu cha ng'ombe, na mle ndimo Mwokozi wa ulimwengu alimozaliwa. TU 147.3

Malaika waliagizwa kuwapasha habari watu waliokuwa tayari kuzipokea, na kuzipitisha kwa wengine. Kristo amejishusha kabisa ili atwae haki ya asili ya binadamu, na maafa yao mpaka atoe nafsi yake iwe kafara ya dhambi. Hata hivyo malaika walitamani kuwa, ingawa amejishusha kiasi hicho, Mwana wake Mungu aliye juu, heri aonekane kwa watu wengine heshima na fahari inayofanana na hadhi yake. TU 147.4

Je, wakuu wa Israeli, watakusanyika Yerusalemu ili kumsalimu? Je, malaika watamjulishwa kwao? TU 147.5

Malaika alikuja duniani ili kuona kuwa ni watu wangapi waliokuwa tayari kumkaribisha Yesu. Lakini hakusikia sauti yoyote ya kumshangilia Masihi. Malaika aliruka juu ya mji mteule wa Yerusalemu na hekalu tukufu ambapo upendeleo wa mbinguni umekuwa kwa miaka mingi, lakini hata hapo mambo yalikuwa yale yale ya kutoamini. Makuhani waliendelea kutoa dhabihu ambazo ni najisi juu ya madhabahu najisi. Mafarisayo waliendelea kupaza sauti zao kwa majivuno wakisali popote walipopenda, mabarabarani. Wafalme wenye elimu, waalimu wote hao hawakushughulika na habari ya kuzaliwa kwa Mwokozi. TU 148.1

Mjumbe wa mbinguni alikuwa karibu kurudi mbingu kwa mshangao mkuu, ndipo alipogundua kundi la wachungaji wakilinda kondoo zao. Walipokuwa wakiangalia nyota huko mbinguni, walikumbuka unabii unaohusu kuzaliwa kwa Mwokozi, nao wakatamani sana utimizo wa unabii huo. Kumbe, hapa liko kundi la watu walio tayari kupokea habari za mbinguni. Ghafla, utukufu wa mbinguni ukaangaza uwanda mzima. Malaika wengi sana wasiohesabika wakatokea, kana kwamba malaika mmoja asingetosha kuleta habari hiyo, kwa kuwa nyingi mno; Sauti za waliokombolewa wa mataifa yote, zikisema “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na dunia yote iwe amani, kwa watu waliowaridhia” Luka 2:14. TU 148.2

Lo, hili ni fundisho gani la hadithi ya ajabu ya Bethlehemu! Hadithi hii inatuaibishaje? Inatufanyaje tuwe tayari, tusije tukashindwa kutambua dalili za wakati wa majilio. TU 148.3

Malaika hawakukuta watu alio tayari kwa wachungaji peke yao, la. Katika nchi ya watu wa mataifa pia kulikuwa na wakeshaji. Mamajusi wa Mashariki, watu waheshimiwa na matajiri. Wenye elimu wa Mashariki walikuwako. Walijifunza kutoka katika maandiko ya Waebrania juu ya Nyota itakayotoka kwa Yakobo. Basi walingoja kwa hamu sana, yule atakayekufa Mariji, sio wa Israeli pekee, bali na watu wote wa ulimwengu mzima. “Nuru ya kuwaangazia mataifa, na wokovu mpaka mwisho wa nchi” Luka 2:25, 32; Matendo 13:47. Nyota ya mbinguni iliwaongoza Mamajusi, ambao ni wageni mpaka mahali alipozaliwa mfalme. TU 148.4

Kristo atatokea kwa wale wanaomtazamia kwa wokovu. Waebrania 9:28. Kama habari za kuzaliwa Kristo, zilivyokuwa, zikiwafikia watu wa hali ya kawaida, ujumbe wa kurudi kwake umekabidhiwa kwa watu wa hali ya kawaida, sio kwa wataalamu, wala waalimu wa makanisa ya Kikristo ya dunia. Wao wameikataa nuru ya mbinguni, kwa hiyo hawamo katika hesabu inayosemwa na Paulo: “Bali ninyi, ndugu hamno gizani mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza”. 1Tes. 5:4-5. TU 148.5

Walinzi juu ya kuta za Sayuni wangekuwa wa kwanza kupata habari za kurudi kwa Mwokozi, na kuzitangaza. Lakini wanajikalia tu, wakati watu wanafia dhambini. Yesu aliona kanisa lake likiwa kama mti usiozaa, lakini wenye majani tele. Roho ya unyenyekevu na uchaji wa imani ya kweli imepungua sana. Kilichoko ni kiburi, ubinafsi, mfano wa utawa na unafiki. Kanisa asi limefumba macho halizioni dalili. Wamejitenga na Mungu na upendo wake. Kwa jinsi wasivyohusiana na ahadi zake hazitimii kwao. TU 149.1

Wafuasi wengi wa Kristo wanaikana nuru ya mbinguni. Sawa na Wayahudi wa kale hawatambui dalili za majilio yao. Bwana aliwaacha, akawafunulia waliokuwa wakikesha kama Wachungaji wa Bethlehemu, na Mamajusi wa Mashariki. TU 149.2

Marejeo: TU 149.3

Tazama Daniel T. Taylor, Te Reign of Christ on Earth or the Voice of the Church in all Ages p. 33 TU 149.4

Sir, Charles Lyell — Principles of Geology p. 495 TU 149.5

Encyclopedia American Art “Lisbon” (ed. 1831) TU 149.6

The Assex Antiquarian, April 1899 Vol. 3 No. 4 p. 53-54. TU 149.7

William Gordon, History of the Rise — Progress Vol. 3 p. 57. TU 149.8

Isaiah Thomas, Massachusets. Spy or American Oracle of Liberty Vol. 10, No. 472 (May 1780) TU 149.9

Letter by Dr. Samuel Tenney of Exeter New Hampshire, Collection 1792 (1st Series Vol. 1 p. 97). TU 149.10