Pambano Kuu

99/261

16/Kutafuta Uhuru Katika Nchi Mpya

Ingawa mamlaka na mafundisho ya Rumi yalikataliwa, lakini kawaida nyingi za imani yao ziliunga na kuendeshwa katika ibada ya kanisa la Aglikan. Ilidaiwa kwamba mambo ambayo hayakukanushwa katika Biblia hayakuwa na ubaya wowote. Kule kushikilia kawaida nyingi za Rumi kulipunguza mtengano uliokuwapo baina ya kanisa la Matengenezo na Rumi na ikahimizwa kwamba kwa kufanya hivo watazidi kuingiza kanuni za matengenezo zikubaliwe na Rumi. TU 136.1

Watu wengine hawakukubaliana na mawazo hayo. Waliona kuwa kawaida hizo ni alama ya utumwa ambao walipigana ili kujiondoa humo. Hawawezi kuzikubali ziingizwe katika ibada zao. Walisema kuwa Mungu amepanga kanuni za kufuatwa katika ibada, ambazo zimeandikwa katika Neno lake, na ya kwamba watu hawana ruhusa kuongeza mambo yao juu ya kanuni hizo, wala kuondoa mambo mengine. Rumi ilianza kwa kukataza mambo ambayo Mungu hakukataza, na ikaishia na kukataza mambo ambayo Mungu aliamuru yafanyike. TU 136.2

Watu wengi waliona kuwa kawaida hizo zinazofuatwa na kanisa la Anglikana ni ukumbusho wa ibada ya sanamu, na kanisa hilo likiungwa mkono na serikali likasisitiza mambo yawe hivyo tu, na ibada iwe kama inavyoendeshwa na kanisa la Anglikana. Mtu akikaidi, adhabu ni kifungo, kutiwa kizuizini au kifo. TU 136.3

Waprotestant hawakuweza kuona uhakika na maisha yao kwa siku za mbele, kwa vile walivyokuwa wakiwindwa kila mahali, wakiteswa na kufungwa ovyo magerezani. Wengine waliotafuta makimbilio katika nchi ya Uholanzi, walisalitiwa na kutiwa katika mikono ya adui zao. Lakini kwa juhudi na uvumilivu walifaulu, wakapata hifahdi katika pwani za watu ambao ni marafiki. TU 136.4

Walikuwa wameacha nyumba zao na mali zao pia. Walikuwa wakimbizi katika nchi za kigeni, wakilazimika kufanya kazi ngumu ili wapate chakula. Lakini hawakuishi kivivu au kwa manung'uniko. Walimshukuru Mungu kwa ajili ya mibaraka aliyowapa, na furaha ya ushirika waliyopata bila masumbufu yo yote. TU 136.5