Pambano Kuu

90/261

15/Utawala Wa Ufaransa Wa Kitisho: Ukweli Wake

Baadhi ya mataifa yaliyopokea matengenezo haya kama kwamba ni ujumbe wa mbinguni. Lakini katika nchi nyingine nuru ya Biblia ilikuwa karibu kuzimika kabisa. Katika nchi moja kulikuwa na mashindano makubwa baina ya ukweli na huo kwa karne nyingi. Mwishowe ukweli wa mbinguni ulitupiliwa mbali. Mvuto wa Roho wa Mungu uliwaondokea watu wale waliokidharau kipawa cha neema yake. Na ulimwengu wote uliona matunda ya ukaidi wa kuikataa nuru ya Mungu. TU 124.1

Vita ya kuipinga Biblia katika Ufaransa iliishia katika mapinduzi, ambayo ni matokeo ya kuuficha ukweli wa Biblia kwa Rumi. Hali hiyo ilidhihirisha wazi kabisa mambo ambayo hayajaonekana katika mafundisho ya kanisa la Rumi. TU 124.2

Mwandishi wa ufunuo alitaja matokeo ya kutisha yatakayotokea katika Ufaransa kwa ajili ya kutawaliwa na “mtu wa dhambi” TU 124.3

“Wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili. Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, wamevikwa magunia. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele ya Bwana wa nchi. Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutokea katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. Hao wana amri ya kuzifunga mbinguni, ili mvua isinye katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo. Hata watakapomaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa… Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili aliwatesa wao wakaao juu ya nchi. Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu itawaingia wakisimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama”. Ufunuo 11:2-11 TU 124.4

“Miezi ya arobaini na miwili” na “siku elfu na mia mbili na sitini” ni kitu kimoja. Ni muda ule ambao kanisa la Mungu litateswa na Rumi Siku 1260 au miaka 1260 ilianzia mwaka 538 baada ya Kristo na ikamalizika katika mwaka 1798. Katika mwaka wa 1798 jeshi la ufaransa lilimteka Papa na kumfunga. Papa aliwekwa kizuizini mpaka akafia huko. Tangu hapo utawala wa kanisa la Rumi ulififia. TU 124.5

Mateso ya kanisa hayakuendelea muda wote wa miaka 1260. Kwa rehema za Mungu aliyakatiza, maana aliwahurumia watu wake. Mungu aliyakatiza kwa njia ya mvuto wa watengenezaji wa kanisa. TU 125.1

“Mashahidi wawili” wanawakilisha maandiko matakatifu ya Agano la Kale na Agano Jipya. Ushahidi halisi wa sheria ya Mungu ya milele na mpango wa ukombozi. TU 125.2

“Watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini wakivaa nguo za magunia” Biblia ilipofafanua ushuhuda wake uliopotoshwa, ukaelezwa kinyume; na wao waliueleza halisi waliitwa wazushi, wakateswa, na kuuawa, hata ikawalazimu kukimbia ili wajiponye. Hao ndio mashahidi waaminifu wakati wa giza kuu la kiroho watu wa Mungu waaminifu walipewa hekima na uwezo wa kulihubiri neno la Mungu. TU 125.3

“Na kama mtu atawadhuru moto ulitoka katika vinywa vyao ukawateketeza adui zao. Na kama mtu atawadhuru hivyo ndivyo ilimpasa uawe” Ufunuo 11:5. Watu hawewezi kukanyaga juu ya Neno la Mungu kwa dharau na kiburi! TU 125.4

“Watakapokwisha kutoa ushahidi wao”. Kama wale mashahidi wawili walipokuwa wakikaribia mwisho wao kimya kimya, vita vitafanywa; kwao na mnyama atokaye kuzimu. Hapa uwezo wa shetani unaonekana. TU 125.5

Imekuwa kanuni ya Rumi ambaye anadai kufuata Biblia kuisitiri Biblia isijulikane, na watu wakae gizani bila nuru ya Biblia Wale mashahidi wawili wenye mavazi ya maguni walitoa unabii katika utawala wao. Lakini mnyama atokaye TU 125.6

“Mji mkuu” ambao mashahidi wawili aliuawa katika njia zake na mizoga yao ililala ni Misri ya Kiroho. Mataifa yote yanayotajwa katika Biblia, Misri ndilo taifa kaidi mno ambalo lilikana kwa ushupavu kuwako kwa Mungu aliye hai na kuzipinga amri zake. Hakuna mfalme yeyote aliyekaidi na kujitoa katika uasi mkuu kama mfalme wa Misri, Farao alivyofanya. Alisema, “Simjui Bwana, wala sitawaacha Waisraeli” Kutoka 5:2. Huu ndio ukafiri wa kukanusha kwamba hakuna Mungu, na taifa linalohusiana na hali hiyo ya Misri litasema vivyo hivyo. TU 125.7

“Mji Mkuu” pia ni mfano wa kiroho, ufananao na Sodoma, udhalimu wa Sodoma ulidhihirika hasa katika hali ya uasherati na ufedhuli na kila namna. Dhambi hii ilikumba taifa lote lililohusika kutimiza unabii huu wa Biblia. TU 125.8

Kwa kufuata unabii ni kwamba muda kitambo kabla ya mwaka 1798 uwezo mwingine wa kishetani ungeinuka kupigana na Biblia. Katika nchi ile mashahidi wawili wa Mungu watakapouawa, kutaonekana ukafiri kama ule wa Farao na ufisadi kama ule wa Sodoma. TU 126.1