Pambano Kuu

1/261

Pambano Kuu

Kwa Nini Huna Budi Ukisome Kitabu Hiki

Kwa mamilioni ya watu maisha kwao hayana maana yoyote na huonekana kama upuuzi. Elimu ya Sayansi na ya ufundi wote, Elimu ya Filosofia hata ya mambo ya dini imemdhihirisha binadamu kama kiumbe aliyetokea kwa bahati tu. Walakini, kwa kusudi watu wake wanaona kwamba ni vigumu kukubali kuishi maisha ya ubatili. Ujeuri, ukaidi na uasi, kujaribisha madawa haya yote, kwa ujumla huonyesha upumbavu wa watu wanaoshindana na hali ya kutisha ya upotevu. Sawa kama mtoto yatima wanalia katika hali ya kukata tamaa, wakisema Mimi ni nani? Wazazi wangu walikuwa akina nani? Nitawapateje? TU i.1

Wengi hugeukia Sayansi ili wapate jawabu; hugeukia kwamba huuliza, Je, kuna mtu yeyote huko anayenifahamu ambaye ananiangalia? Lakini Sayansi haina jawabu. Sayansi imewekwa kuuliza tu maswali, chembechembe hufanyikaje? Hutawanyikaje? Mawazo yetu hufanyaje kazi? Ulimwengu umefanyikaje? TU i.2

Sayansi haiwezi kutueleza sababu za kuwako chembe ndogo, au kwa nini biandamu anaishi, au kwa nini ulimwengu uliumbwa. Wala haiawezi kujibu maswali muhimu ya watu wenye hekima ya dunia. TU i.3

Kama kuna maana na haki ulilmwnguni kwa nini mwenye haki hutaabika pamoja na mwovu? Je, kuna maisha baada ya kufa? Je, nafsi ya mtu huishi milele? Je, makanisa ya kikristo ya leo kwa kweli humtetea Mungu? Ukweli ni nini? TU i.4

Hali ya ulimwengu wa baadaye ni nini? Je ulimwengu utakwisha kwa hali ya kitoto kutaabika kupata hewa ya mwisho katika machafuko ya hewa au utamalizwa na kombora kubwa lililotupwa kutoka katika chombo? Au mwanadamu ambaye tangu mwanzo hakuweza kuonesha uwezo wowote wa kujitawala asiwe mtu wa kuacha ubinafsi ghafla atokee kukomesha maovu, vita umaskini na kifo? TU i.5

Kitabu hiki kinatoa majibu ya hakika. Maisha yanaumuhimu! Sisi sio peke yetu ulimwenguni. Yuko mtunzaji! Kwa kweli yuko anayejishughulisha na mambo ya binadamu, ambaye alijiunga na jamii yetu ili tuweze kupitia kwake na yeye kwetu. Yuko ambaye mkono wake hodari hutunza sayari yetu ambaye ataongoza na kufikisha mahali pa usalama tena karibuni. TU ii.1

Lakini zamani za miaka iliyopita adui mwenye kushawishi alikusudia kuinyakua dunia yetu na kuitawala na kuuharibu mpango bora wa Mungu wa amani na furaha kwa jamaa nzima ya binadamu. Maelezo ya hali ya ulimwengu yameitaja hatari hii isiyoonekana ya uwezo ulio tayari kuuharibu ulimwengu wetu. Katika onekano la kibinadamu ukafiri na hali ya makanisa vimeungana pamoja na kuwa katika hatia. TU ii.2

Kitabu hiki kitaweza kuchapishwa na kutawanywa tu pale palipo na uhuru wa dini, maana kinatoboa wazi makosa katika siku zetu. Kinaeleza sababu zilizofanya matengenezo ya kanisa yakahitajika na kwa nini yalisimamishwa. Kinatoa kisa cha kusikitisha cha makanisa yaliyoanguka, na muungano wa kikatili wenye kutesa watu na kuinua kwa ushirikiano wa kanisa na serikali ambao utafanya sehemu yake ya ukatili kabla ya kumalizika kwa mshindano makuu kati ya uovu na wema. Katika mapambano haya kila mwanadamu atahusika. TU ii.3

Mwandishi anaandika mambo ambayo hayajatukia wakati wa uhai wake, lakini hayana budu kutukia. Anasema kwa hakika mambo ya kustusha. Mambo ya mapambano haya ni mazito mno kiasi cha kutaka mtu ayatangaze ili kuonya watu. TU ii.4

Hakuna msomaji atakayesoma mambo haya bila kushanga na kutaka kuyachunguza zaidi, na kuwa ilikuwa zaidi bahati yake kuyapata. TU ii.5

Watengenezaji. TU ii.6