Tumaini Kuu

180/254

Kipimo cha Hukumu

Sheria ya Mungu ni kipimo katika hukumu. “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni” “Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.” Mhubiri 12:13, 14; Yakobo 2:12. TK 298.1

“Lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili” watakuwa na sehemu katika ufufuo wa wenye haki. Yesu anasema: “wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu...ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.” “Wale waliofanya mema” watatoka kwanza “kwa ufufuo wa uzima” Luka 20:35, 36; Yohana 5:29. Wafu walio hai hawatafufuliwa mpaka baada ya hukumu watapohesabiwa wamestahili “kwa ufufuo wa uzima.” Hivyo hawatakuwepo wakati kumbukumbu zao zitakapokuwa zinachunguzwa na mashauri yao kuamuliwa. TK 298.2

Yesu atatokea kama wakili wao, kusihi mbele za Mungu kwa niaba yao. “Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki” “Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” “Kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.” lYohana 2:1; Waebrania 9:24; 7:25. TK 298.3

Vitabu vya kumbukumbu vitakapofimguliwa katika hukumu, maisha ya wote waliokuwa wanamwamini Yesu yataonekana mbele za Mungu. Wakili wetu ataleta mashauri ya kila kizazi kwa mfuatano, akianza na wale waliokuwa wa kwanza kuishi hapa duniani. Kila jina litatajwa na kila shauri litachunguzwa. Majina yatakubaliwa na mengine yatakataliwa. Wote watakaoonekana na dhambi kwenye vitabu vya kumbukumbu, ambazo hawakutubu na kusamehewa; majina yao yatafutwa kutoka kwenye kitabu cha uzima. Bwana alimwambia Musa: “Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.” Kutoka 32:33. TK 298.4

Wale wote ambao wamefanya toba ya kweli na kwa imani wamedai damu ya Yesu kama kafara yao ya upatanisho wamepata msamaha na umeingizwa kwenye vitabu vya mbinguni. Kwa sababu wamekuwa washirika wa haki ya Kristo na tabia zao zinaonekana kuwa zinapatana na sheria ya Bwana, dhambi zao zitafutwa, na watahesabiwa kuwa wamestahili uzima wa milele. Bwana anatangaza kuwa: “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.” Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe...nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.” “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.’Tsaya 43:25; Ufunuo 3:5; Mathayo 10:32, 33. TK 299.1

Mpatanishi wa mbinguni anapeleka ombi kwamba wote walioshinda kwa imani katika damu yake, warejeshwe kwenye makazi yao ya Edeni na pia wavikwe taji ya kuwa warithi pamoja naye katika “Mamlaka ya kwanza.” Mika 4:8. Kristo sasa anaomba kwamba ule mpango wa Mungu wa kumwumba mwanadamu uendelee kana kwamba mwanadamu alikuwa hakuanguka. Hawaombei watu wake msamaha na kuhesabiwa haki tu, bali pia wawe na sehemu katika utukufu wake na kiti cha enzi katika Ufalme wake. TK 299.2

Wakati Yesu anaendelea kusihi kwa ajili ya walengwa wa neema yake, Shetani anawashtaki mbele za Mungu. Ananyosha kidole chake kwenye kumbukumbu za maisha yao, upungufu wa kitabia, kutofanana na Kristo, kwenye dhambi zote alizowajaribu ili watende. Kwa ajili ya dhambi hizo, anadai kuwa hao ni watu wake. TK 299.3

Yesu hawaondolei dhambi zao tu, bali huonesha toba na imani yao. Anapowaombea msamaha, huinua mikono yake iliyojeruhiwa mbele za Baba, na kusema: Nimewaandika kwenye viganja vya mikono yangu. “Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” Zaburi 51:17. TK 299.4