Tumaini Kuu

9/254

Sura Ya 3 - Giza La Kiroho Katika Kanisa La Awali

Mtume Paulo alisema kuwa siku ya Kristo isingekuja “usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.” Na tena, “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 The. 2:3, 4, 7. Hata wakati huo, mtume aliona yakiingia amakosa mbayo yangeandaa njia kwa ajili ya utawala wa Papa. TK 35.1

“Siri ya kuasi” iliendelea kufanya kazi ya udanganyifu tararibu. Desturi za kipagani zikaingia katika kanisa la Kikristo, zikizuiwa kwa muda na mateso makali yaliyoletwa na upagani; lakini mateso yalipokoma, Ukristo uliuacha unyenyekevu Wakristo na mahali pake pakawa na majivuno ya makuhani na watawala. Kuongoka nusu nusu kwa Konstantino kulisababisha shangwe kubwa. Sasa kazi ya uharibifu iliendelea kwa kasi zaidi. Upagani, ambao ulikuwa umeonekana kushindwa, ukawa umeshinda. Mafundisho na mapokeo potuvu wa kipagani yakajumuishwa katika imani ya wale waliokuwa wanadai kuwa wafuasi Wakristo. TK 35.2

Mwafaka huu kati ya upagani na Ukristo ulizaa “mtu wa kuasi” aliyekuwa ametabiriwa katika unabii. Hiyo dini bandia ndiyo kazi ambayo Shetani alifanya kwa ustadi mkubwa, yaani juhudi zake za kukaa katika kiti cha enzi ili aitawale dunia sawasawa na mapenzi yake. TK 35.3

Moja ya mafundisho makuu katika Kanisa la Roma ni kwamba Papa amepewa mamlaka ya juu kabisa kuliko maaskofu na mapadri duniani kote. Zaidi ya hilo, Papa ameitwa “Bwana Mungu, Papa” na kutangazwa kuwa hawezi kukosea. (Angalia kiambatisho). Hoja ile ile ambayo Shetani alikuwa anaitoa wakati wa kumjaribu Yesu kule jangwani, anaendelea kuitoa kwa njia ya Kanisa la Roma, na watu wengi wanamtii. TK 35.4

Lakini wale wanaomcha Mungu wanaikabili hali hii ya kujitwalia mamlaka kama vile Kristo alivyokabiliana na adui huyo mwcnye hila: “Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.” Lk. 4:8. TK 35.5

Mungu hajawahi kumteua mtu ye yote kuwa kichwa cha kanisa. Ukuu wa Papa ni kinyume cha Maandiko. Papa hawezi kuwa na mamlaka juu ya kanisa la Kristo bila kujitwalia mamlaka hayo yeye mwenyewe. Wafuasi wa Kanisa la Roma huwatuhumu Waprotestanti kwa kujitenga kwa makusudi kutoka katika kanisa la kweli. Lakini wao ndio walioiacha “imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.” Yud. 3. TK 36.1

Shetani alikuwa anajua vema kuwa Mwokozi aliyapinga na mashambulizi yake kwa kutumia Maandiko Matakatifu. Katika kila shambulio, Kristo alitoa ngao ya ukweli wa milele, akisema, “Imeandikwa.” Ili Shetani aweze kudumisha utawala wake kwa watu na kuimarisha mamlaka ambayo Papa amejitwalia, lazima aendelee kuwafanya wasijue Maandiko. Ukweli mtakatifu wa Maandiko hayo lazima ufichwe na kuzimwa. Kwa mamia ya miaka usambazaji wa Biblia ulikuwa umepigwa marufuku na Kanisa la Roma. Watu walikuwa wamekatazwa kuisoma. Makasisi na maaskofu waliyafasiri mafundisho ya Biblia ili kulinda hila zao. Kwa namna hiyo, Papa akajulikana karibu dunia yote kama mwakilishi wa Mungu hapa duniani. TK 36.2