Kutayarisha Njia

198/210

Asili ya Magonjwa Mengi

Kamwe nyama haikuwa chakula bora; lakini kuitumia sana kumekuwa jambo baya maradufu, kwa kuwa magonjwa ya wanyama huongezeka upesi sana. Mara nyingi kama wangewaona wanyama hao wakiwa hai na kujua hali ya nyama wanayoila, wangeiacha na kuichukia kabisa. Watu daima huila nyama inayojawa na vijidudu vya ugonjwa wa kifua kikuu na vya donda baya la ‘saratani’. Kifua kikuu, ‘saratani’ na magonjwa mengine makubwa huenezwa kwa njia hiyo. 3 KN 259.3