Kutayarisha Njia

147/210

Kujilaumu Mwenyewe Kwafaa Sana

Kama wote wanaojidai kuwa ni Wakristo wangetumia uwezo wao wa kujihoji ili kuona mabaya yapasayo kusahihishwa ndani yao wenyewe, badala ya kuongea juu ya makosa ya wengine, pangekuwa na hali njema kanisani leo. Bwana atengenezapo vito vyake vya thamani, waaminifu, wenye adili, watatazamwa kwa furaha. Malaika hutumiwa kuzitengeneza taji za watu wa jinsi hiyo, na juu ya hao taji zenye nyota zitang’aa na kutoa nuru ambayo hutoka katika kiti cha enzi cha Mungu. KN 202.5

Mungu huwapima na kuwathibitisha watu wake. Waweza kuwa mkali na mwepesi kuvumbua na kutoa makosa madogo madogo uliyo nayo mwenyewe kama upendavyo; lakini, uwe mpole, mwenye huruma, na mwenye adabu kwa wengine. Uliza kila siku; Nina maana, au ninajidanganya nafsini? Mwombe Mungu kukuokoa na udanganyifu wote juu ya jambo hili. Mambo ya milele hutatanisha. Je, naugu mpendwa, wengi wanapotamani heshima na faida isiyo ya halali, unatafuta kwa bidii ahadi ya upendo wa Mungu na kulia: Ni nani atakayenionyesha jinsi ya kufanya imara kuitwa kwangu na uteule wangu? KN 202.6

Shetani huchunguza kwa uangalifu dhambi za watu za asili, kisha huanza kazi yake ya kuwadanganya na kuwawekea mitego. Tumo kwenye majaribu makali, lakini tunaweza kushinda kama tukipigana kiume vita vya Bwana. Wote wako hatarini. Lakini kama mkienenda kwa unyenyekevu na kuomba kwa bidii mtatoka katika jaribio mkiwa wenye thamani zaidi ya dhahabu safi, naam, kuliko dhahabu ya Ofiri. Mkiwa wazembe na wasiomwomba Mungu, mtakuwa kama shaba iliayo na upatu uvumao.10 KN 203.1