Kutayarisha Njia

146/210

Matokeo Yaletwayo na Lawama za Kanisa na Viongozi wa Jamii ya Watu

Moyo wa kutoa maneno ya upuzi na kuchongea ni mojawapo ya njia kubwa za Shetani za kueneza fitina na ugomvi ili kuwatenga marafiki, na kuharibu imani ya wengi katika ukweli wa hali zetu. Ndugu na dada wako tayari mno kuongea makosa ambayo hudhani yamo kwa wengine, na hasa kwa wale ambao wameutoa kwa uthabiti ujumbe wa maonyo walioupewa na Mungu. KN 201.1

Watoto wa hao wanung’unikaji husikiliza sana na kupokea sumu ya chuki. Hivyo ndivyo wazazi wanavyofunga, bila kujua, njia ambazo kwazo mioyo ya watoto hao ingeweza kufikiwa. Kwa hili Mungu hudharauliwa. Yesu amesema: “Kadiri mlivyomtendea mmoiawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Matnayo 25:40). Hivyo Kristo hudharauliwa na kutukanwa na wale wanowasingizia watumishi wake. KN 201.2

Majina ya watumishi wateule wa Mungu yametumiwa kwa dharau, na wakati mwingine kwa aibu kabisa, na watu fulani ambalo wajibu wao ni kuwasaidia. Watoto hawakukosa kusikia maneno ya dharau ya wazazi wao kwa habasri za makaripio na maonyo ya nao watumishi wa Mungu. Wamefahamu maneno ya mzaha na ya kukashifu ambayo mara kwa mara yamesikika masikioni mwao, na mwelekeo umekuwa kuyalinganisha akilini mwao mambo mazuri ya kupendeza moyo na mambo matakatifu na ya milele, sawa na mambo ya kawaida ya ulimwengu huu. Kazi gani hii watendayo wazazi hao kuwafanya watoto wao kuwa makafiri hata utotoni mwao! Hivi ndivyo watoto wanavyofundishwa kuwa watu wasio na heshima na kuyaasi maonyo ya Mungu juu ya dhambi. KN 201.3

Upungufu wa hali ya kiroho huweza kuwa na nguvu mahali penye maovu. Hao baba na mama, wakiwa wamepofusnwa na yule adui, hustaajabu kwa nini watoto wao huelekea sana kutoamini na kulitilia shaka neno la kweli la Biblia. Hushangaa kuona kuwa ni shida sana kuwapata kwa mivuto ya adili na dini. Kama wangekuwa na macho ya kiroho, mara moja wangegundua kuwa hali hiyo mbaya ya kusikitisha ni matokeo ya mvuto wa nyumbani mwao wenyewe, imezaa wivu na mashaka yao. Hivyo ndivyo makafiri wengi wanavyofundishwa na kutayarishwa nyumbani mwa wale wanaojita Wakristo. KN 201.4

Kuna wengi wanaopendezwa hasa na kufikiri sana makosa, yakiwa ya hakika au ya kuwaziwa tu, ya wale wenye madaraka kazini mwa Mungu. Hawatazami mema ambayo yametendwa, na faida zilizotokana na kazi ngumu na moyo thabiti wa kicho kazini, bali hukazia macho kosa fulani lililo dhahiri, neno ambalo, likisha kutendwa na kupata mradi wake, huona kuwa lingeweza kutendwa kwa njia bora yenye matokeo mema zaidi; ambapo kama wangeachwa kuitenda kazi hiyo, wasingethubutu hata kidogo kufanya To lote kwa sababu ya mambo ya kukatisha tamaa ya hali hiyo, ama wangeweza kufanya hivyo kijinga zaidi ya wale walioifanya kazi hiyo, wakifuata majaliwa ya Mungu. KN 201.5

Lakini wasengenyaji hawa watashikilia mambo mabaya zaidi ya kazi, kama vile ukoga unavyoshikilia juu ya maparuzo ya mwamba. Watu hawa wamedumaa kiroho kwa kuendelea kukaa juu va kushindwa na makosa ya wengine. Hawana uwezo wa kiroho wa kuweza kupambanua matendo yaliyo mema na bora, jitihada zisizo za kujipenda nafsi, ujasiri wa kweli na kujinyima. Huharibu tabia kila siku na kuzidi kupungua maoni yao Uhafifu katika sehemu yao, na hali inayowazunguka ni sumu kwa amani na raha. 7 KN 202.1

Kila idara ya kazi itapaswa kushindana na shida. Dhiki hurusiwa ili kuipima mioyo ya watu wa Mungu na kwa kazi yake. Wakati kama huo mtu awaye yote asiyaangahe mambo vibaya na kuonyesha moyo wa mashaka na kutokuamini. Msiwalaumu wale wanaochukua mizigo ya madaraka. Mazungumzo nyumbani mwenu yasitiwe sumu na moyo wa kuwalaumu watenda kazi wa Mungu. Wazazi wenye moyo huo wa kulaumu hawawaletei watoto wao kile ambacho kitawahekimisha hata kupata wokovu. Maneno yao huelekea kuiharibu imani na matumaini siyo ya watoto tu, bali nata ya wazee pia. 8 KN 202.2

Wakubwa wa kazi zetu wanayo kazi ngumu kudumisha utaratibu na kuwatawala kwa busara vijana walio chini ya uangalizi wao. Washiriki wa kanisa wanaweza kufanya mengi kuimarisha mikono yao. Vijana wakikataa kukaa chini ya utawala wa wakuu wa idara ya kazi, au kwa jambo lo lote kuwa kinyume cha wakuu wao hukusudia kufanya kama wapendavyo wenyewe; basi wazazi wasiwasaidie wala kuwahurumia watoto wao bila kufikiri kwanza. KN 202.3

Ni heri watoto wenu kuumia, naam, heri walale makaburini mwao, kuliko kufundishwa kuzidharau kanuni zilizo msingi hasa wa kuutii ukweli kwa wanadamu wenzao, na kwa Mungu. 9 KN 202.4