Kutayarisha Njia

145/210

Wivu na Masuto

Naona uchungu kusema kuwa kuna walio na ndimi zisizotawaliwa miongom mwa washiriki wa kanisa. Kuna ndimi za uongo zenye kujilisha fitina. Kuna ndimi za hila zenye kunong’ona. Kuna wenye vijeneno, wafidhuli, ayari. Wengine miongoni mwa wale wapendao mazungumzo ya upuzi huchochewa na moyo wa utafiti, wengine huchochewa na wivu, na wengi huchochewa na chuki juu ya wale ambao kwa njia yao Mungu amesema nao kuwaonya. Mambo hayo yote yasiyopatana hufanya kazi. Wengine huficha nia zao hasa, huku wengine wakitaka sana kutangaza yote wajuayo, au hata vale wanayoshuku tu, juu ya ubaya wa mwingine. KN 199.5

Naliona kuwa roho ya ushuhuda wa uongo, ambao ungegeuza ukweli kuwa uongo, jema kuwa baya, na hali ya kutokuwa na hatia kuwa hali ya hatia, sasa inatenda kazi. Shetani hufurahia hali ya namna hii kwa watu wanaodai kuwa ni wa Mungu. Huku wengi wakiacha kuangalia roho zao wenyewe, wanatafuta sana nafasi ya kuwalaumu wengine. Wote wana hitilafu za tabia, na si vigumu kuona kitu ambacho wivu huweza kukielezea isivyo ili kuwadhuru. “Sasa,” ndivyo wasemavyo hao wanaojifanya wana sheria, “tunayo mamboya hakika . Tutawashitaki jambo wasiloweza kujiepusha na hatia.” Hungoja nafasi ya kufaa ndipo kutoa bunda la maneno matupu na kuleta vipande vidogo vizuri vya habari. KN 200.1

Katika kujitahidi kutimiza neno linalotakiwa, watu hao kwa asili wana uwezo mkali wa kuwazia mambo yasiyoonekana ila yanayosikika yakitajwa wamo katika hatari ya kujidanganya na kuwadanganya wengine. Hukusanya maneno ya kijinga kutoka kwa mwingine, husema kwa haraka na kukosea kuonyesha nia hasa za wasemaji. Lakini maneno hayo yasiyofikiriwa kabla ya kusema, ambayo mara nyingi ni vijineno tu visivyo na maana, huangaliwa kwenye kioo cha Shetani cha kukuza mambo hata yaonekane kuwa makubwa, yakifikiriwa, na kurudiwa mara nyingi mpaka vichuguu vya mchwa vinakuwa milima (mpaka yale maneno madogo yanakuwa makubwa). KN 200.2

Je, ni tabia ya Kikristo kukusanya habari zo zote, kufukua kila kitu kitakacholeta shuku juu ya tabia ya mwingine, ndipo kufiirahia kukitumia kumdhuru? Shetani hufurahi akiweza kumvunjia sifa au kumjeruhi mfuasi wa Kristo. Ni “mshitaki wa ndugu zetu.” Je, Wakristo wamsaidie katika kazi yake? KN 200.3

Jicho la Mungu lionalo yote huyaona makosa ya wote na hasira inayomtawala kila mmoja, lakini huyavumilia makosa yetu na kutuhurumia udhaifu wetu. Awaamuru watu wake kuihifadhi roho hiyo hiyo ya wema na uvumilivu. Wakristo wa kweli hawatafurahia kucnongea makosa na kasoro za wengine. Wataachilia mbali uovu na kombo, ili kukaza mawazo kwa kile ambacho ni kizuri na cha kupendeza machoni. Kwa Mkristo kila tendo la masuto, kila neno la lawama, huuma. 6 KN 200.4