Kutayarisha Njia

144/210

Mwenye Kijicho haoni Jema Lo Lote kwa Wengine

Tusikubali mashaka yetu na mambo nyenye kutukatisha tamaa kula rohoni mwetu na kutufanya wenye ucnungu na moyo wa harara. Yasiwepo mashindano yo yote, ama kuonea mabaya wala masengenyano, tusije tukamchukiza Mungu. Ndugu, ukifungulia wivu nakudhania maovu moyoni mwako, Roho Mtakatifu hawezi kukaa nawe. Tafuta ukamilifu uliomo ndani ya Kristo. Tumika kazini mwake. Kila wazo na neno na tendo navimdhihirishe. Wahitaji ubatizo wa kila siku wa upendo ambao siku za mitume uliwafanya wote kuwa na moyo mmoja. Upendo huo utaleta afya mwilini, akilini, na rohoni. Zungushia roho yako hali ya kupendeza ambayo itatia nguvu maisha ya kiroho. Kuza imani, matumaini, moyo mkuu, na upendo. Acha amani ya Mungu itawale moyoni mwako. 4 KN 198.3

Wivu siyo huharibu tu tabia ya mtu bali ni chuki, ambayo huchafua uelekevu wote. Umeanzishwa na Shetani. Yeye alitamani kuwa wa kwanza mbinguni, na kwa sababu hakuweza kupata mamlaka yote na utukufu aliotaka, akauasi utawala wa Mungu. Akawaonea wivu wazazi wetu wa kwanza akawashawishi kutenda dhambi, hivyo akawaharibu pamoja na wanadamu wote pia. KN 199.1

Mwenye kijicho huyafumba macho yake ili asione matendo mema na bora ya watu wengine. Yu tayari siku zote kudharau na kueleza vibaya kile kilicho bora. Watu mara nyingi huungama na kuyaacha makosa mengine, lakini hakuna matumaini ila kidogo tu kwa mwenye kijicho kufanya hivyo. Kwa kuwa mtu hawezi kuonea wivu mpaka kwanza akiri kwamoa ni mkuu; kiburi hakitamkubalia kuomba radhi. Kama jitihadi ikifanywa kusadikisha mwenye kijicho aina ya dhambi yake, huzidi kuona uchungu juu ya kitu kinachomchukiza, na mara nyingi hukaa hali hiyo bila kupona. KN 199.2

Mtu mwenye kijicho hueneza sumu po pote aendako, akifitini marafiki na kuamsha chuki na uasi juu ya Mungu na mwanadamu. Atafuta kudhaniwa kuwa yu bora na mkuu kuliko wote wengine, siyo kwa kuonyesha ushujaa, ili kuufikia upeo wa wema, bali kwa kusimama mahali alipo bila kusogea na kupunguza sifa inayozistahili bidii za wengine. KN 199.3

Ulimi unaofurahia fitina, ulimi wenye kubwata ambao husema, “Nipe habari, nami nitasimulia habari hizo.” umeelezwa na mtume Yakobo kuwa ni ulimi unaowasha moto wa jehanam. Hutawanya vinga vya moto kila upande. Kwani mwenezaji wa vijineno anajali kumsingizia mtu asiye na hatia? Hatazuia kazi yake ya uovu ingawa huharibu matumaini na kuwaflsha moyo wale ambao tayari wamekwisha kuanza kuzama ndani ya udhia wao. Anachojali tu ni kufungua njia ya mwelekeo wake wa kupenda machongezi. Hata wale wanaojidai kuwa ni Wakristo huyafumba macho yao wasione kitu chochote kilicho safi, amini, bora, na cha kupendeza, wakathamini chochote kile kilicho kibaya na cha kuchukiza, na kukitangaza kwa walimwengu. KN 199.4