Kutayarisha Njia

142/210

Sura Ya 33 - Mateto na Matokeo Yake ya Baadaye

YAWAPASA Wakristo kujihadhari na maneno yao. Kamwe Wasieneze habari mbaya toka kwa rafiki mwingine huyu mpaka wanafahamu kwamba kuna mafarakano baina yao. Ni udhalimu kukonyeza na kusema kwa fumbo, kwamba unajua mengi juu ya rafiki huyo au kwamba unafahamu mambo mengine wasiyoyajua. Madokezo ya namna hiyo huenea mbali, na kuleta moyo mbaya kuliko kusema mambo wazi bila kutia chumvi. Kanisa la Kristo limepata madhara kama nini kwa mambo hayo! Mwenendo usiosawa wa kijinga wa washiriki wake umelidhoofisha kanisa kabisa. Matumaini yametupwa na washiriki wa kanisa hilo, walakini wakosaji hawakukusudia kutia fitina. Kutotumia busara katika kuchagua mambo ya kuzungumza kumeleta madhara mengi. KN 197.1

Ingefaa mazungumzo yawe juu ya mambo ya kirono, lakini yamekuwa kinyume chake. Kama kushirikiana na marafiki Wakristo hutumiwa zaidi kuzidisha ubora wa akili na moyo, hapatakuwa na majuto baadaye, nao wanaweza kutazama mambo ya nyuma na kuridhika. Lakini kama saa zinatumiwa kwa mazungumzo ya ovyo, bila kicho, na wakati wa thamani unatumiwa kwa kusengenya myenendo na tabia za wengine, maongezi ya kirafiki yatakuwa chanzo cha mabaya, na mvuto wako utakuwa harufu ya mauti iletayo mauti. 1 KN 197.2