Kutayarisha Njia

112/210

Sura Ya 24 - Baba na Mama Mkristo

KADIRI mfanyavyo kwa uaminifu wajibu wenu nyumbani baba kama kuhani wa nyumbani, mama kama mmishenari nyumbani mwazidisha njia za kufanya mema nje ya nyumba hiyo. Kadiri mnavyotumia vizuri uwezo wenu wenyewe, ndivyo mnavyofanywa kufaa zaidi kutumika kanisani na jirani. Kwa kufungamana na watoto wenu na kuwafungamanisha na Mungu, baba na mama na watoto pia huwa watenda Kazi pamoja na Mungu. 1 KN 163.1