Vita Kuu
Kuamshwa kwa Mambo ya Mungu
Po pote palisikiwa ushuhuda uliowaonya wenye dliambi, wayafuatao mambo ya kidunia pamoja na washiriki wa kanisa, wapate kuikimbia ile hasira itakayokuja. Wahubiri walilitia shoka chini ya mti, kama Yohana Mbatizaji aliyemtangulia Kristo, wakawavuta watu wapate kuyazaa matunda yapasayo toba. Mafundisho yao yaliyogusa sana mioyo yalihitilafiana kabisa na ahadi za amani na salama zilizohubiriwa katika makanisa ya kupendeza watu wengi. na po pote ujumbe huu ulipopelekwa, uliamsh^ mioyo ya watu. VK 56.1
Ushuhuda wa Biblia, uliokuwa dhahiri sana na rahisi kufahamika, na uliochoma mioyo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ulikuwa na uwezo mkuu wa kuwasadikisha watu, hata watu wachache tu ndio walioweza kuupinga kabisa. Walimu wakuu wa dini waliamshwa movo wakafahamu hali yao ya kimoyo jinsi walivyo hatarini. Walifahamu maasi yao, tabia yao ya kuyapenda mambo na anasa za dunia, na kutoamini kwao, kiburi chao na hali yao ya kujipenda nafsi. Wengi walimtafuta Bwana kwa kutubu na kujidhili. Upendo wao uliokuwa umedumu sana juu ya mali za dunia hii uligeuka ukaelekea mbinguni. Roho ya Mungu aliwakalia, na kwa mioyo iliyopondeka na kutulizwa wakajiunga katika kuutangaza ujumbe huu, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” Ufunuo 14:7. VK 56.2
’Wenye dhambi waliuliza sana kwa machozi wakisema, “Nifanye nini nipate kuokolewa?” Wale ambao maisha yao hayakuwa ya uaminifu walikuwa na hamu ya kurudisha walivyonyang’anya wengine. Wote waliopokea amani katika Kristo walitaka kuwashirikisha wengine mibaraka hiyo. Mioyo ya wazazi iliwageukia watoto wao, na mioyo ya watoto iliwageukia wazazi wao. Matengano ya kiburi na unyamavu ulitokomelea mbali. Maungamo ya kweli yalitolewa, na watu wa nyumba fulani fulani walikuwa wakiwaombea wapendwa wao wengine kusudi wapate kuokolewa. VK 57.1
Mara nyingi sauti ya maombi ilisikika. Po pote watu walikuwa na maumivu rohoni na kumwomba Mungu. Wengi waliomba usiku kucha kwa kupata tumaini ya kwamba wanasamehewa dhambi zao wenyewe, au wakiomba kwa ajili ya jamaa zao na jirani zao wapate kuongoka. Imani ile kuu iliwafaidia sana. Watu wa Mungu wangaliendelea kuwa wenye juhudi kwa kuomba hivi, kwa kupeleka maombi yao mbele ya kiti cha neema wangekuwa na hali njema ya kiroho zaidi ya ile hali yao ya sasa. Lakini kuomba kumekuwa haba zaidi, hali ya kusadiki hatia ya dhambi hiionekana mara chache sana, hali ya kutokuwa na imani huwaondolea wengi ile neema kuu iliyotolewa kwa wingi na Mwokozi wetu mwenye rehema. VK 57.2
Watu wa kila aina walikuia wengi kwa mikutano ya Waadventista. Matajiri na maskini, watu wenye heshima na watu duni, walikuja kwa ajili ya sababu mbali mbali, wakiwa na hamu sana kuyasikia wenyewe mafundisho ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Wakati ule ambapo watumishi wa Mungu walikuwa wakieleza sababu ya imani yao, Bwana Mungu mwenyewe aliituliza ile nia ya kushindana. Pengine mjumbe aliweza kuwa mnyonge, lakini Roho ya Mungu alilitilia nguvu Neno lake. Kuwako kwa malaika watakatifu kulionekana katika mikutano hii, na kila sik” waaminio waliongezeka wakawa wengi. Mambo yaliyoonyesha kukaribia kwa marejeo ya Yesu yalipokaririwa, makutano makubwa ya watu walikaa kimya wakiyasikiliza maneno yale mazito. Nyakati zile ilionekana kana kwamba mbingu na dunia zilikaribiana. Uwezo wa Mungu ulionekana juu ya wazee, vijana na watu wazima. Watu walikwenda nyumbani midomo yao ikijaa sifa za Bwana, na kwa utulivu wa siku zilisikika sauti za watu zikishangilia. Ha-kuna hata mmoja aliyehudhuria mikutano hiyo awezaye kuyasahau maneno mazito waliyoyasikia. VK 57.3