Vita Kuu
Vita Kuu
Ujumbe wa Mwandishi kwa Wasomaji wa Kitabu Hiki
KWA njia ya mwangaza wa Roho Mtakatifu, mambo ya shindano baina ya wema na uovu, ambalo limeendelea tangu zamani, yamefunuliwa kwa mwandishi wa kitabu hiki. Mara kwa mara niliruhusiwa kuona yaliyofanywa nyakati nyingine maalum katika shindano kuu baina ya Kristo, aliye Mkuu wa Uzima, na Sababu ya wokovu wetu, na Shetani aliye mkuu wa uovu, na sababu ya dhambi, mwasi wa kwanza wa amri takatifu za Mungu. Uadui wa Shetani juu ya Kristo umeonyeshwa juu ya wafuasi wake. Chuki ile aliyokuwa nayo juu ya sheria ya Mungu, shauri lue fake la udanganyifu, ambalo kwalo hufanya uongo kuonekana kana kwamba ni kweli, tena kwalo wanadamu huongozwa wakakisujudia kiumbe badala ya Muumba: mambo haya yameonekana tangu awali. Jitihada ya Shetani katika kueleza vibaya tabia za Mungu, na katika kuongoza wanadamu wamdhanie Mungu kwa namna isiyo ya haki, hata wamwogope n kumehukia badala ya kumpenda; jinsi ambavyo amejaribu kubatili amri ya Mungu, na lcuongoza wanadamu ili wafikiri kwamba wamekuwa huru, tena ya kama haiwalazimu kufuata matakwa ya sheria yake; jinsi ambavyo anawadhulumu wale wanaothubutu kuyapinga madanganyifu yake, haya ndiyo mashauxi ambayo ameyafuata katika vizazi vyote... . VK 8.1
Katika vita kuu ya mwisho, Shetani atafanya namna ile ile, atakuwa n nia ile ile, tena atakuwa n kusudi sawa na file alilokuwa nlo tangu zamani zote za kale. Mambo yaliyofanywa zamani yatafanywa tena, isipokuwa mashindano yajayo yatakuwa niakali mno jinsi isivyokuwa duniani tangu awali. Madanganyifu va Shetani yatakuwa werevu zaidi, mashambulio yake yatakuwa magumu zaidi, kama yamkini, atawapoteza hata wateule wa Mungu. (Soma Marko 13:22, na Mathayo 24:24). . . . VK 8.2
Kusudi la kitabu hiki siyc kuonyesha mambo mapya hasa juu ya siku za kale, ila kueleza mambo ya hakika yanayohusika na mambo yajayo. Walakini, yakitazamiwa na kufikiriwa jinrsi yalivyo sehemu ya shindano baina ya nguvu za nuru na za giza, mambo haya ya zamani huonekana kuwa na maana mpya; kwa ajili yake nuru inaangaza siku zijazo, ikimulika njia yao ambao, kama watengezaji wa zamani wa dini, wataitwa, hata kwa kujihatarisha maisha, wawe mashahidi kwa ajili ya “Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.” Ufunuo 1:1. VK 8.3
Makusudi ya kitabu hiki ndiyo kufunua mambo ya shindano kuu baina ya kweli na uongo; kudhihirisha hila za Shetani, tena namna anavyoweza kushindwa; kueleza habari za uovu jinsi ulivyo, kuonyesha chanzo cha dhambi na jinsi itakavyomalizwa, na kueleza mambo haya kwa namna ya kufaa kwa kudhihirisha haki na wema wa Mungu katika yote awatendeavyo wanadamu; na kuonyesha sheria yake jinsi ilivyo takatifu na isivyobadilika; haya ndiyo makusudi ya kitabu hiki. Tena ombi la mwandishi ndilo hili: ili, kwa mvuto wa maneno yake, watu wapate - kuokolewa katika nguvu za giza, wapate kustahilishwa “kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru,” kwa sifa yake aliyetupenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yetu. (Kol. 1:12; Gal. 2:20.) VK 8.4
Ellen G. White