Hakuna Mashaka wala kusitasita
Alinena kama mwenye mamlaka. Marabi walinena kwa kusitasita, wakiwa na mashaka, na maana ya maandiko. Lakini Yesu alifundisha ukweli bila shaka yoyote. Fundisho lolote alilofundisha, alilinena kwa mamlaka.
TVV 136.3
Walakini alinena kwa juhudi na kwa moyo, si kwa magombano. Kwa kila hali, Mungu alidhihirishwa. Yesu alitaka kuvunja hali ya kupumbaza, inayowang’ang’ania watu katika mambo ya ulimwengu. Aliweka mambo ya ulimwengu kuwa, ni hafifu kulinganisha na ya milele. Lakini hakusahau umuhimu wake. Alifundisha kuwa, kufahamu mambo ya Mungu vema, humtayarisha mtu kutekeleza mambo ya dunia kwa uzuri zaidi, katika maisha ya kila siku. Akifahamu uhusiano wake na Mungu, alitambua nia mwungano wake na kila mtu katika ujamaa wa kibinadamu.
TVV 136.4
Alijua jinsi ya kunena kwa mtu mchovu, kwa wakati unaofaa. Isaya 50:4. Alikuwa na busara na jinsi ya kukutana na wenye chuki, na kuwaambia mifano itakayowavuta. Mifano yake alitumia mambo ya kila siku katika maisha. Ingawa huwa vielelezo rahisi sana, walakini huwaingia wasikilizaji wake kabisa. Ndege, maua, mbegu, mchungaji kondoo wa vielelezo hivi vyepesi, alifundisha ukweli. Na baadaye walipovikumbuka na kuviona, walikumbuka fundisho lake, au mafundisho yake.
TVV 136.5
Kristo hakuwasifusifu watu kamwe, wala kuwatukuza kwa ajili ya mambo yao mazuri. Lakini bila chuki wasikilizaji wake waliona kuwa maneno yake, kwa kweli ni ya busara, nayo yanapima ujuzi wao. Wasomi wakubwa waliburudishwa kwa maneno yake, na wasiokuwa na elimu walifaidika. Aliwafanya hata watu wa mataifa waone kuwa ujumbe wake unawahusu pia.
TVV 136.6
Hata katikati ya uhasama mkali, ulikaa katika hali ya salama. Tabia yake ya upendo, usemi wake na hali yake ya upendo, viliwavuta wote kwake, wale ambao hawakuharibiwa roho zao na hali ya kutoamini. Watu wenye dhiki na mateso walimhesabu kuwa rafiki mfadhili mkuu, nao walitaka kujua zaidi ukweli anaoufundisha. Walitamani kukaa kwenye fadhili zake siku zote.
TVV 137.1
Yesu aliziangalia nyuso za wasikilizaji wake. Alipoziona jinsi zinavyong’aa kwa kuchangamka, zilimtia nguvu, na utoshelevu mkubwa. Mishale ya ukweli ilipokuwa ikipenya katika roho za watu wapendao ubinafsi, wakigeuka kuwa wema, Mwokozi alifurahi. Macho yake yalipowaona watu, ambao walikutana naye siku zilizopita, aling’aa kwa furaha. Aliposema maneno ya ukweli kwa wenye kushikilia sanamu, yaani anasa ya dunia, hali yake ilionyesha kuwa ujumbe wake haukukubalia na watu hao. Alipoona kuwa watu wameukataa ujumbe wa amani, roho yake ilisonononeka vikubwa mno.
TVV 137.2
Katika sinagogi Yesu alipokuwa akifundisha alikomeshwa, ili amweke huru mtu aliyefungwa na Shetani, yaani mwenda wazimu aliruka kutoka katika mkutano, huku akipiga makelele na kusema: “Tuache, tuna nini nawe, Ee Yesu wa Nazareti? Je umekuja kutuangamiza? Najua kuwa wewe mtakatifu wa Mungu.” Mambo yalichafuka na kuvurugika. Watu waliangalia mambo ya mtu huyu, wakaacha mambo ya Yesu. Lakini Yesu alimkemea pepo, akisema: “Nyamaza, mtoke.” Wakati pepo alipomwangusha kati ya watu, alimtoka asimzuru.
TVV 137.3
Mtu huyu aliyesumbuliwa hivyo, mawazo yake yalikuwa yameharibiwa na Sheteni lakini alipofika kwa Yesu aliamka kutaka afunguliwe kutokana na kifungo hicho cha Shetani. Lakini pepo mchafu alishindana ili amng’ang’anie. Mtu huyu alipotaka kuomba msaada kwa Yesu, pepo mchafu alitia maneno kinywani mwake, akapiga makelele kwa masumbuko na hofu.
TVV 137.4
Mwenye pepo mchafu alifahamu kidogo kuwa alikuwa mbele ya mwenye uwezo wa kumponya, lakini alipojaribu kumsogelea yule mwenye uwezo wa kuponya, alizuiliwa na uwezo fulani, uwezo huo ukaweka maneno fulani kinywani mwake. Mashindano baina ya Shetani na yeye yalikuwa makubwa.
TVV 137.5
Pepo mchafu alitumia uwezo wake wote ili amshikilie mtu huyu. Ilionekana kuwa mtu huyu atapoteza maisha yake, katika mashindano haya na adui huyu aliyeharibu hali yake. Lakini Mwokozi aliamuru na mtu akafunguliwa. Mtu huyu alisimama katika kundi la watu, hali wakishangaa, lakini wakifurahi kwa kuponywa kwake. Hata pepo mchafu alishuhudia mamlaka ya Mwokozi. Macho ya mtu huyo yaliyokuwa yakitisha sana kuangalia, yalionekaria matulivu yakishukuru nguvu ya Yesu. Watu wakasema: “Jambo gani hili? Hili ni fundisho jipya! Kwa amri huwaamuru hata pepo wachafu nao humtii.”
TVV 137.6
Mtu huyu amekuwa ameharibiwa na anasa za dhambi naye alidhani kuwa maisha yake yatakuwa yenye furaha na sikukuu. Hakufikiri kuwa atakuwa kitisho kwa watu, na shutumu kwa jamaa yake. Alidhani kuwa maisha yake yatakuwa katika hali safi ya upuzi wa anasa. Lakini pasipokuwa na kiasi na upuzi viliyaongoza maisha yake vibaya, na Shetani akamteka. Wakati alipotaka kujiokoa katika mtego huo, hakuweza. Alikuwa ameshikiliwa katika uwezo wa mwovu. Shetani alikuwa ametawala viungo vyake vyote. Mtu huyu alipokwisha kuwa katika utawala wake, Shetani akamtendea mambo ambayo hayana huruma. Ndivyo ilivyo kwa watu wanaojiweka katika mikono ya Shetani. Mtu anayejitumbukiza katika maisha ya anasa katika maisha yake ya ujana, huishia katika hali ya wazimu.
TVV 138.1
Roho ile iliwatawala Wayahudi wasioamini, lakini kulikuwako na Yesu ambaye alikuwa mtawa. Hali ya Wayahudi wasioamini ilikuwa mbaya kuliko ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Maana wao hawakumhitaji Kristo. Kwa hiyo walikuwa katika uwezo wa Shetani zaidi.
TVV 138.2
Kuwako kwa Kristo, akifanya kazi kati ya watu, kulikuwa na juhudi kuu na msukosuko mkuu wa ufalme wa giza. Kwa vizazi na vizazi Shetani amewakandamiza watu katika masumbuko na maradhi ya namna namna. Amewatumbukiza dhambini na matatizoni. Halafu amemsingizia Mungu kuwa ndiye amesababisha hayo yote. Yesu alikuwa akiwafunulia watu tabia ya Mungu jinsi ilivyo. Alikuwa akivunja uwezo wa Shetani na kuwaweka watu huru kutokana na mambo ya Shetani. Upendo na uwezo wa mbinguni ulikuwa ukiwachangamsha watu, na mkuu wa giza alichukizwa sana. Alipinga kazi ya Kristo kwa kila hatua.
TVV 138.3
13871
TVV
Tumaini la Vizazi Vyote
[{"para_id":"13871.97","title":"4 \u2014 Kuzaliwa Zizini","mp3":"\/mp3\/13871\/0014_swa_f_4_kuzaliwa_zizini_13871_97.mp3#duration=342&size=5577659"},{"para_id":"13871.145","title":"6 \u2014 Tumeiona Nyota Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0020_swa_f_6_tumeiona_nyota_yake_13871_145.mp3#duration=699&size=11277784"},{"para_id":"13871.184","title":"7 \u2014 Mtoto Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0025_swa_f_7_mtoto_yesu_13871_184.mp3#duration=598&size=6083499"},{"para_id":"13871.216","title":"8 \u2014 Kuhudhuria Katika Pasaka","mp3":"\/mp3\/13871\/0029_swa_f_8_kuhudhuria_katika_pasaka_13871_216.mp3#duration=664&size=6739433"},{"para_id":"13871.248","title":"9 \u2014 Matatizo ya Kristo Wakati wa Utoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0032_swa_f_9_matatizo_ya_kristo_wakati_wa_utoto_13871_248.mp3#duration=834&size=8439843"},{"para_id":"13871.282","title":"10 \u2014 Sauti Nyikani","mp3":"\/mp3\/13871\/0036_swa_f_10_sauti_nyikani_13871_282.mp3#duration=1057&size=10667758"},{"para_id":"13871.336","title":"11 \u2014 Ubatizo wa Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0042_swa_f_11_ubatizo_wa_yesu_13871_336.mp3#duration=478&size=4879322"},{"para_id":"13871.360","title":"12 \u2014 Majaribu","mp3":"\/mp3\/13871\/0045_swa_f_12_majaribu_13871_360.mp3#duration=977&size=9870882"},{"para_id":"13871.401","title":"13 \u2014 Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0050_swa_f_13_ushindi_13871_401.mp3#duration=623&size=6329203"},{"para_id":"13871.428","title":"14 \u2014 Tumemwona Masihi","mp3":"\/mp3\/13871\/0054_swa_f_14_tumemwona_masihi_13871_428.mp3#duration=1307&size=13172069"},{"para_id":"13871.485","title":"15 \u2014 Yesu Ahudhuria Harusi","mp3":"\/mp3\/13871\/0060_swa_f_15_yesu_ahudhuria_harusi_13871_485.mp3#duration=932&size=9423837"},{"para_id":"13871.527","title":"16 \u2014 Kristo Akabili Machafuko Hekaluni","mp3":"\/mp3\/13871\/0063_swa_f_16_kristo_akabili_machafuko_hekaluni_13871_527.mp3#duration=1374&size=13844801"},{"para_id":"13871.579","title":"17 \u2014 Nikodemo Amwendea Yesu Wakati wa Usiku","mp3":"\/mp3\/13871\/0068_swa_f_17_nikodemo_amwendea_yesu_wakati_wa_usiku_13871_579.mp3#duration=1110&size=11198316"},{"para_id":"13871.619","title":"18 \u2014 Yeye Hana Budi Kuzidi Bali Mimi Kupungua\u2019","mp3":"\/mp3\/13871\/0071_swa_f_18_yeye_hana_budi_kuzidi_bali_mimi_kupungua_13871_619.mp3#duration=392&size=4024084"},{"para_id":"13871.640","title":"19 \u2014 Yesu na Mwanawke Mwenye Waume Watano","mp3":"\/mp3\/13871\/0073_swa_f_19_yesu_na_mwanawke_mwenye_waume_watano_13871_640.mp3#duration=1095&size=11052730"},{"para_id":"13871.695","title":"20 \u2014 \u201cMsipoona Ishara na Maajabu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0078_swa_f_20_msipoona_ishara_na_maajabu_13871_695.mp3#duration=404&size=4140487"},{"para_id":"13871.715","title":"21 \u2014 Bethzatha na Sanhedrin","mp3":"\/mp3\/13871\/0079_swa_f_21_bethzatha_na_sanhedrin_13871_715.mp3#duration=1404&size=22570477"},{"para_id":"13871.777","title":"22 \u2014 Kifungo na Kifo cha Yohana","mp3":"\/mp3\/13871\/0086_swa_f_22_kifungo_na_kifo_cha_yohana_13871_777.mp3#duration=1163&size=11730972"},{"para_id":"13871.830","title":"23 \u2014 Jinsi Danieli Alivyomtambua Yesu kuwa ni Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0092_swa_f_23_jinsi_danieli_alivyomtambua_yesu_kuwa_ni_kristo_13871_830.mp3#duration=543&size=5530218"},{"para_id":"13871.851","title":"24 \u2014 \u201cJe, Huyu Siye Mwana wa Seremala?\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0094_swa_f_24_je_huyu_siye_mwana_wa_seremala_13871_851.mp3#duration=718&size=7276333"},{"para_id":"13871.885","title":"25 \u2014 Mwito Kando ya Bahari","mp3":"\/mp3\/13871\/0096_swa_f_25_mwito_kando_ya_bahari_13871_885.mp3#duration=618&size=6283618"},{"para_id":"13871.911","title":"26 \u2014 Siku za Shughuli na Raha katika Kapernaumu","mp3":"\/mp3\/13871\/0100_swa_f_26_siku_za_shughuli_na_raha_katika_kapernaumu_13871_911.mp3#duration=1004&size=10145925"},{"para_id":"13871.955","title":"27 \u2014 Mwenye Ukoma wa Kwanza Kuponywa na Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0103_swa_f_27_mwenye_ukoma_wa_kwanza_kuponywa_na_kristo_13871_955.mp3#duration=999&size=10093329"},{"para_id":"13871.1004","title":"28 \u2014 Mathayo: Kutoka Kutoza Ushuru Mpaka Mwanafunzi","mp3":"\/mp3\/13871\/0107_swa_f_28_mathayo_kutoka_kutoza_ushuru_mpaka_mwanafunzi_13871_1004.mp3#duration=830&size=8399583"},{"para_id":"13871.1042","title":"29 \u2014 Yesu Aiokoa Sabato","mp3":"\/mp3\/13871\/0112_swa_f_29_yesu_aiokoa_sabato_13871_1042.mp3#duration=933&size=9434863"},{"para_id":"13871.1081","title":"30 \u2014 Awekea Mikono Mitume Kumi na Wawili","mp3":"\/mp3\/13871\/0117_swa_f_30_awekea_mikono_mitume_kumi_na_wawili_13871_1081.mp3#duration=405&size=4147140"},{"para_id":"13871.1100","title":"31 \u2014 Mahubiri Mlimani","mp3":"\/mp3\/13871\/0119_swa_f_31_mahubiri_mlimani_13871_1100.mp3#duration=1556&size=25001595"},{"para_id":"13871.1172","title":"32 \u2014 Afisa wa Jeshi Aomba Msaada Kwa Ajili Mtumishi Wake","mp3":"\/mp3\/13871\/0125_swa_f_32_afisa_wa_jeshi_aomba_msaada_kwa_ajili_mtumishi_wake_13871_1172.mp3#duration=533&size=8636236"},{"para_id":"13871.1199","title":"33 \u2014 Jinsi Yesu Alivyojihusisha na Matatizo ya Jamaa","mp3":"\/mp3\/13871\/0127_swa_f_33_jinsi_yesu_alivyojihusisha_na_matatizo_ya_jamaa_13871_1199.mp3#duration=744&size=11999844"},{"para_id":"13871.1229","title":"34 \u2014 Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi","mp3":"\/mp3\/13871\/0130_swa_f_34_nira_yake_ni_laini_na_mzigo_wake_ni_mwepesi_13871_1229.mp3#duration=511&size=8279056"},{"para_id":"13871.1255","title":"35 \u2014 Kutuliza Dhoruba","mp3":"\/mp3\/13871\/0133_swa_f_35_kutuliza_dhoruba_13871_1255.mp3#duration=953&size=15344257"},{"para_id":"13871.1299","title":"36 \u2014 Mguso wa Imani","mp3":"\/mp3\/13871\/0136_swa_f_36_mguso_wa_imani_13871_1299.mp3#duration=457&size=7409111"},{"para_id":"13871.1320","title":"37 \u2014 Wainjilisti wa Kwanza","mp3":"\/mp3\/13871\/0138_swa_f_37_wainjilisti_wa_kwanza_13871_1320.mp3#duration=804&size=12970024"},{"para_id":"13871.1358","title":"38 \u2014 Kristo na Wanafunzi Wapumzika","mp3":"\/mp3\/13871\/0141_swa_f_38_kristo_na_wanafunzi_wapumzika_13871_1358.mp3#duration=504&size=8168554"},{"para_id":"13871.1385","title":"39 \u2014 \u201cWapeni Ninyi Chakula\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0144_swa_f_39_wapeni_ninyi_chakula_13871_1385.mp3#duration=299&size=4886983"},{"para_id":"13871.1413","title":"40 \u2014 Usiku Ziwani","mp3":"\/mp3\/13871\/0147_swa_f_40_usiku_ziwani_13871_1413.mp3#duration=639&size=10325621"},{"para_id":"13871.1445","title":"41 \u2014 Hatari Katika Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0150_swa_f_41_hatari_katika_galilaya_13871_1445.mp3#duration=1322&size=21255291"},{"para_id":"13871.1509","title":"42 \u2014 Kristo Atabiri Juu ya Maanguko","mp3":"\/mp3\/13871\/0157_swa_f_42_kristo_atabiri_juu_ya_maanguko_13871_1509.mp3#duration=310&size=3197643"},{"para_id":"13871.1527","title":"43 \u2014 Kristo Avunja Ubaguzi wa Mataifa","mp3":"\/mp3\/13871\/0159_swa_f_43_kristo_avunja_ubaguzi_wa_mataifa_13871_1527.mp3#duration=551&size=5609425"},{"para_id":"13871.1551","title":"44 \u2014 Ishara ya Kweli","mp3":"\/mp3\/13871\/0161_swa_f_44_ishara_ya_kweli_13871_1551.mp3#duration=684&size=6941240"},{"para_id":"13871.1582","title":"45 \u2014 Kuonyeshwa Mbele Fumbo la Msalaba","mp3":"\/mp3\/13871\/0165_swa_f_45_kuonyeshwa_mbele_fumbo_la_msalaba_13871_1582.mp3#duration=1145&size=11549078"},{"para_id":"13871.1631","title":"46 \u2014 Yesu Ageuka Sura","mp3":"\/mp3\/13871\/0169_swa_f_46_yesu_ageuka_sura_13871_1631.mp3#duration=510&size=5201013"},{"para_id":"13871.1653","title":"47 \u2014 Kupingana na Roho za Mashetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0171_swa_f_47_kupingana_na_roho_za_mashetani_13871_1653.mp3#duration=530&size=5405611"},{"para_id":"13871.1675","title":"48 \u2014 Nani Aliye Mkubwa Zaidi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0173_swa_f_48_nani_aliye_mkubwa_zaidi_13871_1675.mp3#duration=1120&size=11299793"},{"para_id":"13871.1724","title":"49 \u2014 \u201cMtu Akiwa na Kiu, na Aje\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0177_swa_f_49_mtu_akiwa_na_kiu_na_aje_13871_1724.mp3#duration=703&size=7128511"},{"para_id":"13871.1758","title":"50 \u2014 Katikati ya Mitego","mp3":"\/mp3\/13871\/0180_swa_f_50_katikati_ya_mitego_13871_1758.mp3#duration=856&size=8662407"},{"para_id":"13871.1798","title":"51 \u2014 Nuru ya Uzima","mp3":"\/mp3\/13871\/0184_swa_f_51_nuru_ya_uzima_13871_1798.mp3#duration=1310&size=13204222"},{"para_id":"13871.1859","title":"52 \u2014 Mchungaji, Mungu","mp3":"\/mp3\/13871\/0190_swa_f_52_mchungaji_mungu_13871_1859.mp3#duration=580&size=5898525"},{"para_id":"13871.1886","title":"53 \u2014 Safari ya Mwisho Kutoka Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0194_swa_f_53_safari_ya_mwisho_kutoka_galilaya_13871_1886.mp3#duration=863&size=8730237"},{"para_id":"13871.1925","title":"54 \u2014 Msamaria Mwema","mp3":"\/mp3\/13871\/0198_swa_f_54_msamaria_mwema_13871_1925.mp3#duration=616&size=6260151"},{"para_id":"13871.1952","title":"55 \u2014 Si Kujionyesha kwa Nje","mp3":"\/mp3\/13871\/0200_swa_f_55_si_kujionyesha_kwa_nje_13871_1952.mp3#duration=433&size=4434757"},{"para_id":"13871.1971","title":"56 \u2014 Upendo wa Yesu kwa Watoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0201_swa_f_56_upendo_wa_yesu_kwa_watoto_13871_1971.mp3#duration=543&size=5526138"},{"para_id":"13871.1996","title":"57 \u2014 Kijana Tajiri Mtawala Amepungukiwa na jambo Moja","mp3":"\/mp3\/13871\/0203_swa_f_57_kijana_tajiri_mtawala_amepungukiwa_na_jambo_moja_13871_1996.mp3#duration=478&size=4879601"},{"para_id":"13871.2019","title":"58 \u2014 Kufufuliwa kwa Lazaro","mp3":"\/mp3\/13871\/0205_swa_f_58_kufufuliwa_kwa_lazaro_13871_2019.mp3#duration=1099&size=11092144"},{"para_id":"13871.2066","title":"59 \u2014 Makuhani na Wakuu Wanaendelea na Njama Yao","mp3":"\/mp3\/13871\/0206_swa_f_59_makuhani_na_wakuu_wanaendelea_na_njama_yao_13871_2066.mp3#duration=454&size=4641463"},{"para_id":"13871.2088","title":"60 \u2014 Cheo Kikuu Ni Kipi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0208_swa_f_60_cheo_kikuu_ni_kipi_13871_2088.mp3#duration=406&size=4158184"},{"para_id":"13871.2112","title":"61 \u2014 Mtu Mfupi Aliyekuwa Mashuhuri","mp3":"\/mp3\/13871\/0210_swa_f_61_mtu_mfupi_aliyekuwa_mashuhuri_13871_2112.mp3#duration=401&size=4111640"},{"para_id":"13871.2133","title":"62 \u2014 Mariamu Ampaka Yesu Mafuta","mp3":"\/mp3\/13871\/0211_swa_f_62_mariamu_ampaka_yesu_mafuta_13871_2133.mp3#duration=1307&size=13170907"},{"para_id":"13871.2190","title":"63 \u2014 Yesu Atangazwa Kuwa Mfalme wa Israeli","mp3":"\/mp3\/13871\/0218_swa_f_63_yesu_atangazwa_kuwa_mfalme_wa_israeli_13871_2190.mp3#duration=707&size=7169996"},{"para_id":"13871.2232","title":"64 \u2014 Watu wa Kuangamia","mp3":"\/mp3\/13871\/0222_swa_f_64_watu_wa_kuangamia_13871_2232.mp3#duration=693&size=7031722"},{"para_id":"13871.2263","title":"65 \u2014 Hekalu Latakaswa Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0224_swa_f_65_hekalu_latakaswa_tena_13871_2263.mp3#duration=1329&size=13390450"},{"para_id":"13871.2316","title":"66 \u2014 Kristo Akabiliana na Adui Zake","mp3":"\/mp3\/13871\/0228_swa_f_66_kristo_akabiliana_na_adui_zake_13871_2316.mp3#duration=740&size=7505171"},{"para_id":"13871.2352","title":"67 \u2014 Yesu Azuru Hekalu Mara ya Mwisho","mp3":"\/mp3\/13871\/0231_swa_f_67_yesu_azuru_hekalu_mara_ya_mwisho_13871_2352.mp3#duration=1219&size=12295749"},{"para_id":"13871.2400","title":"68 \u2014 Wayunani Walipotaka \u201cKumwona Yesu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0233_swa_f_68_wayunani_walipotaka_kumwona_yesu_13871_2400.mp3#duration=666&size=6756313"},{"para_id":"13871.2430","title":"69 \u2014 Dalili za Kuja Kwa Kristo Mara ya Pili","mp3":"\/mp3\/13871\/0235_swa_f_69_dalili_za_kuja_kwa_kristo_mara_ya_pili_13871_2430.mp3#duration=1155&size=11655117"},{"para_id":"13871.2473","title":"70 \u2014 Kristo Ashirikiana na Wenye Dhiki na Masikini","mp3":"\/mp3\/13871\/0239_swa_f_70_kristo_ashirikiana_na_wenye_dhiki_na_masikini_13871_2473.mp3#duration=566&size=5758478"},{"para_id":"13871.2498","title":"71 \u2014 Mtumishi wa Watumishi","mp3":"\/mp3\/13871\/0241_swa_f_71_mtumishi_wa_watumishi_13871_2498.mp3#duration=943&size=9526890"},{"para_id":"13871.2539","title":"72 \u2014 Meza ya Bwana Yaanzishwa","mp3":"\/mp3\/13871\/0243_swa_f_72_meza_ya_bwana_yaanzishwa_13871_2539.mp3#duration=958&size=9677405"},{"para_id":"13871.2576","title":"73 \u2014 \u201cMsifadhaike Mioyoni Mwenu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0246_swa_f_73_msifadhaike_mioyoni_mwenu_13871_2576.mp3#duration=1908&size=19179012"},{"para_id":"13871.2641","title":"74 \u2014 Pambano la Kutisha Katika Gethsemane","mp3":"\/mp3\/13871\/0251_swa_f_74_pambano_la_kutisha_katika_gethsemane_13871_2641.mp3#duration=1080&size=10900601"},{"para_id":"13871.2688","title":"75 \u2014 Kesi Batili Dhidi ya Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0256_swa_f_75_kesi_batili_dhidi_ya_yesu_13871_2688.mp3#duration=1590&size=25543110"},{"para_id":"13871.2752","title":"76 \u2014 Jinsi Yuda Alivyopoteza Roho Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0262_swa_f_76_jinsi_yuda_alivyopoteza_roho_yake_13871_2752.mp3#duration=692&size=7020406"},{"para_id":"13871.2784","title":"77 \u2014 Kristo Ashtakiwa Mbele Ya Gavana Wa Kirumi","mp3":"\/mp3\/13871\/0266_swa_f_77_kristo_ashtakiwa_mbele_ya_gavana_wa_kirumi_13871_2784.mp3#duration=1936&size=19458815"},{"para_id":"13871.2868","title":"78 \u2014 Yesu Afa Juu Ya Kalwari","mp3":"\/mp3\/13871\/0274_swa_f_78_yesu_afa_juu_ya_kalwari_13871_2868.mp3#duration=1671&size=16811964"},{"para_id":"13871.2932","title":"79 \u2014 Jinsi Kifo Cha Kristo Kilivyomshinda Shetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0281_swa_f_79_jinsi_kifo_cha_kristo_kilivyomshinda_shetani_13871_2932.mp3#duration=884&size=8938225"},{"para_id":"13871.2968","title":"80 \u2014 Yesu Apumzika Katika Kaburi La Yusufu","mp3":"\/mp3\/13871\/0285_swa_f_80_yesu_apumzika_katika_kaburi_la_yusufu_13871_2968.mp3#duration=708&size=7178978"},{"para_id":"13871.2994","title":"81 \u2014 \u201cBwana Amefufuka\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0288_swa_f_81_bwana_amefufuka_13871_2994.mp3#duration=562&size=5718538"},{"para_id":"13871.3022","title":"82 \u2014 \u201cMama Unalilia Nini?","mp3":"\/mp3\/13871\/0292_swa_f_82_mama_unalilia_nini_13871_3022.mp3#duration=578&size=5878775"},{"para_id":"13871.3051","title":"83 \u2014 Kutembea Kwenda Emau","mp3":"\/mp3\/13871\/0293_swa_f_83_kutembea_kwenda_emau_13871_3051.mp3#duration=498&size=5083897"},{"para_id":"13871.3073","title":"84 \u2014 Kristo Aliyefufuka Atokea","mp3":"\/mp3\/13871\/0296_swa_f_84_kristo_aliyefufuka_atokea_13871_3073.mp3#duration=595&size=6053282"},{"para_id":"13871.3100","title":"85 \u2014 Kando Ya Bahari Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0299_swa_f_85_kando_ya_bahari_tena_13871_3100.mp3#duration=789&size=12730367"},{"para_id":"13871.3133","title":"86 \u2014 \u201cEnendeni . . . Mkawafanye Mataifa Yote\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0302_swa_f_86_enendeni_mkawafanye_mataifa_yote_13871_3133.mp3#duration=936&size=15074513"},{"para_id":"13871.3172","title":"87 \u2014 Kristo Aingia Mbinguni Kwa Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0306_swa_f_87_kristo_aingia_mbinguni_kwa_ushindi_13871_3172.mp3#duration=691&size=11154751"}]