Nabii Danieli Alitabiri Kazi ya Kristo
Mzigo wa mahubiri ya Kristo ulikuwa: “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni mkaiamini Injili.” Marko 1:1 5. Ujumbe wa Injili kama ulivyosemwa na Mwokozi, ulijengwa juu ya unabii. “Wakati” ambao alisema kuwa umetimia, ulikuwa muda ule aliofunuliwa Danieli. “Majuma sabini yamekusudiwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha uasi, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho wa maovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri njozi na unabii, na kumtia mafuta Mtakatifu.” Danieli 9:24. Kwa unabii siku inasimama badala ya mwaka. Ezekiel 4:6. Majuma sabini au siku 490 ni sawa na miaka 490.
TVV 124.1
Mwanzo wa muda huu umeelezwa: “Ujue basi na kufahamu, kuwa tangu kutolewa amri ya kuujenga Yerusalemu hata Masihi Mkuu, utakuwa muda wa majuma saba na muda wa majuma sitini na mawili. Majuma sitini na tisa au miaka 483. Danieli 9:25.
TVV 124.2
Amri ya kuurudisha na kuujenga Yerusalemu, kama ilivyotimizwa kwa amri ya Artashashta Longimanus (Tazama Ezra 6:14; 7:1-9) iliyotolewa mwaka B.C. 457. Tangu wakati huo miaka 483 iliendelea mpaka A.D. 27, kama unabii usemavyo. Muda huu utafika mpaka kwa Masihi, ambaye ni mtiwa mafuta: Mwaka A.D. 27 Yesu alipobatizwa alitiwa mafuta kwa Roho Mtakatifu, na baadaye akaanza kazi yake. Kisha ujumbe ulitangazwa kwamba: “Wakati umetimia.”
TVV 124.3
Kisha malaika alisema: “Kwa juma moja atathibitisha agano kwa wengi (miaka saba). Kwa muda wa miaka saba baada ya Mwokozi kuingia kazini, Injili itatangazwa hasa kwa Wayahudi. Kristo mwenyewe atatangaza injili miaka mitatu na nusu, na mitume miaka iliyobaki.
TVV 124.4
“Kati ya juma atakomesha kafara ya dhabihu.” Danieli 9:27. Katika mwaka A.D. 31 Kristo ambaye ni kafara halisi alitolewa huko Kalwari. Kisha pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kuonyesha kuwa umuhimu wa huduma na kafara za kawaida umeondoka. Wakati umefika wa kukomesha kafara na dhabihu.
TVV 124.5
Juma moja, yaani siku au miaka saba ilimalizika katika mwaka A.D. 34. Ndipo kwa kumpiga Stefano kwa mawe, Wayahudi walitia muhuri kukataa kwao injili. Mitume waliotawanyika kwa ajili ya mateso. “Walienda huko na huko wakilihubiri lile neno.” Matendo 8:4. Baadaye Sauli mtesaji aliongoka, akawa Paulo, mtume kwa watu wa mataifa.
TVV 124.6
Muda wa kuja kwa Kristo, kufa kwake, na kuhubiri injili kwa mataifa vilionyeshwa dhahiri. Iliwapasa Wayahudi waufahamu unabii huu na jinsi ulivyotimia katika kazi ya Yesu. Kufuatana na unabii wa Danieli, Yesu alisema: “Asomaye afahamu.” Mathayo 24:15. Alisema hayo kuhusu wakati wao. Baada ya kufufuka kwake, alieleza kwa wanafunzi wake: “Unabii wote unaomhusu yeye.” Luka 24:27. Mwokozi alikuwa amesema kwa njia ya manabii, akishuhudia kabla na mateso yake na utukufu utakaofunuliwa baadaye. 1 Petro 1:11. Alikuwa Gabrieli, malaika mkuu, aliyekuja kumfunulia Danieli. Malaika huyu huyu ndiye alitumwa na Kristo kwenda kumfunulia Yohana mambo ya Ufunuo. Uheri umesemwa kwa wale wenye kusoma maneno ya unabii na kuyashika mambo yaliyoandikwa humo, Ufunuo 1:3. Mungu atawabariki wenye kutii, wakisoma unabii kwa unyenyekevu kwa roho ya maombi.
TVV 125.1
Kwa ujumbe kwa kuzaliwa kwa Kristo ulivyotangazwa, ambao ulikuwa ni ujumbe wa neema, ndivyo na ujumbe wa kurudi kwake kwa utukufu utakavyotangazwa. Ujumbe huu wa pili, sawa na ule wa kwanza, umejengwa juu ya unabii. Mwokozi mwenyewe ametoa unabii kuhusu kurudi kwake kwa kuonyesha dalili nyingi. Amesema: “Jiangalieni mioyo yenu isije ikalemewa na ulevi na ulafi, na masumbuko ya dunia hii, hata siku ile iwaghafilishe kama mtego unasavyo.” “Kesheni basi, na kuomba daima, ili mhesabiwe kuwa mnastahili, mambo haya yatakapotokea, mpate kusimama mbele ya Mwana wa Adamu ajapo.” Luka 21:34, 36.
TVV 125.2
Wayahudi waliutafsiri unabii kimakosa, na wala hawakujua wakati wa kujiliwa kwao. Miaka ya kazi ya Kristo na ya mitume Wayahudi walishughulika kupanga namna ya kuwaangamiza tu wajumbe wa Mungu. Anasa za dunia na kutafuta makuu ya dunia hii kumewapumbaza watu wengi, hata hawaoni mambo yanayotimiza unabii yatokeayo kwa haraka sana, na dalili za kuja kwake zinazoharakisha mno, zikitangaza kuja kwa ufalme wa Mungu. Ingawa hatujui siku kamili ya kuja kwa Bwana, tunaweza kujua jinsi ilivyokaribia sana. “Kwa hiyo tusilale usingizi kama wengine; ila tukeshe na kuwa na kiasi.” 1 Wathesalonike 5:6.
TVV 125.3
13871
TVV
Tumaini la Vizazi Vyote
[{"para_id":"13871.97","title":"4 \u2014 Kuzaliwa Zizini","mp3":"\/mp3\/13871\/0014_swa_f_4_kuzaliwa_zizini_13871_97.mp3#duration=342&size=5577659"},{"para_id":"13871.145","title":"6 \u2014 Tumeiona Nyota Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0020_swa_f_6_tumeiona_nyota_yake_13871_145.mp3#duration=699&size=11277784"},{"para_id":"13871.184","title":"7 \u2014 Mtoto Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0025_swa_f_7_mtoto_yesu_13871_184.mp3#duration=598&size=6083499"},{"para_id":"13871.216","title":"8 \u2014 Kuhudhuria Katika Pasaka","mp3":"\/mp3\/13871\/0029_swa_f_8_kuhudhuria_katika_pasaka_13871_216.mp3#duration=664&size=6739433"},{"para_id":"13871.248","title":"9 \u2014 Matatizo ya Kristo Wakati wa Utoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0032_swa_f_9_matatizo_ya_kristo_wakati_wa_utoto_13871_248.mp3#duration=834&size=8439843"},{"para_id":"13871.282","title":"10 \u2014 Sauti Nyikani","mp3":"\/mp3\/13871\/0036_swa_f_10_sauti_nyikani_13871_282.mp3#duration=1057&size=10667758"},{"para_id":"13871.336","title":"11 \u2014 Ubatizo wa Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0042_swa_f_11_ubatizo_wa_yesu_13871_336.mp3#duration=478&size=4879322"},{"para_id":"13871.360","title":"12 \u2014 Majaribu","mp3":"\/mp3\/13871\/0045_swa_f_12_majaribu_13871_360.mp3#duration=977&size=9870882"},{"para_id":"13871.401","title":"13 \u2014 Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0050_swa_f_13_ushindi_13871_401.mp3#duration=623&size=6329203"},{"para_id":"13871.428","title":"14 \u2014 Tumemwona Masihi","mp3":"\/mp3\/13871\/0054_swa_f_14_tumemwona_masihi_13871_428.mp3#duration=1307&size=13172069"},{"para_id":"13871.485","title":"15 \u2014 Yesu Ahudhuria Harusi","mp3":"\/mp3\/13871\/0060_swa_f_15_yesu_ahudhuria_harusi_13871_485.mp3#duration=932&size=9423837"},{"para_id":"13871.527","title":"16 \u2014 Kristo Akabili Machafuko Hekaluni","mp3":"\/mp3\/13871\/0063_swa_f_16_kristo_akabili_machafuko_hekaluni_13871_527.mp3#duration=1374&size=13844801"},{"para_id":"13871.579","title":"17 \u2014 Nikodemo Amwendea Yesu Wakati wa Usiku","mp3":"\/mp3\/13871\/0068_swa_f_17_nikodemo_amwendea_yesu_wakati_wa_usiku_13871_579.mp3#duration=1110&size=11198316"},{"para_id":"13871.619","title":"18 \u2014 Yeye Hana Budi Kuzidi Bali Mimi Kupungua\u2019","mp3":"\/mp3\/13871\/0071_swa_f_18_yeye_hana_budi_kuzidi_bali_mimi_kupungua_13871_619.mp3#duration=392&size=4024084"},{"para_id":"13871.640","title":"19 \u2014 Yesu na Mwanawke Mwenye Waume Watano","mp3":"\/mp3\/13871\/0073_swa_f_19_yesu_na_mwanawke_mwenye_waume_watano_13871_640.mp3#duration=1095&size=11052730"},{"para_id":"13871.695","title":"20 \u2014 \u201cMsipoona Ishara na Maajabu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0078_swa_f_20_msipoona_ishara_na_maajabu_13871_695.mp3#duration=404&size=4140487"},{"para_id":"13871.715","title":"21 \u2014 Bethzatha na Sanhedrin","mp3":"\/mp3\/13871\/0079_swa_f_21_bethzatha_na_sanhedrin_13871_715.mp3#duration=1404&size=22570477"},{"para_id":"13871.777","title":"22 \u2014 Kifungo na Kifo cha Yohana","mp3":"\/mp3\/13871\/0086_swa_f_22_kifungo_na_kifo_cha_yohana_13871_777.mp3#duration=1163&size=11730972"},{"para_id":"13871.830","title":"23 \u2014 Jinsi Danieli Alivyomtambua Yesu kuwa ni Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0092_swa_f_23_jinsi_danieli_alivyomtambua_yesu_kuwa_ni_kristo_13871_830.mp3#duration=543&size=5530218"},{"para_id":"13871.851","title":"24 \u2014 \u201cJe, Huyu Siye Mwana wa Seremala?\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0094_swa_f_24_je_huyu_siye_mwana_wa_seremala_13871_851.mp3#duration=718&size=7276333"},{"para_id":"13871.885","title":"25 \u2014 Mwito Kando ya Bahari","mp3":"\/mp3\/13871\/0096_swa_f_25_mwito_kando_ya_bahari_13871_885.mp3#duration=618&size=6283618"},{"para_id":"13871.911","title":"26 \u2014 Siku za Shughuli na Raha katika Kapernaumu","mp3":"\/mp3\/13871\/0100_swa_f_26_siku_za_shughuli_na_raha_katika_kapernaumu_13871_911.mp3#duration=1004&size=10145925"},{"para_id":"13871.955","title":"27 \u2014 Mwenye Ukoma wa Kwanza Kuponywa na Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0103_swa_f_27_mwenye_ukoma_wa_kwanza_kuponywa_na_kristo_13871_955.mp3#duration=999&size=10093329"},{"para_id":"13871.1004","title":"28 \u2014 Mathayo: Kutoka Kutoza Ushuru Mpaka Mwanafunzi","mp3":"\/mp3\/13871\/0107_swa_f_28_mathayo_kutoka_kutoza_ushuru_mpaka_mwanafunzi_13871_1004.mp3#duration=830&size=8399583"},{"para_id":"13871.1042","title":"29 \u2014 Yesu Aiokoa Sabato","mp3":"\/mp3\/13871\/0112_swa_f_29_yesu_aiokoa_sabato_13871_1042.mp3#duration=933&size=9434863"},{"para_id":"13871.1081","title":"30 \u2014 Awekea Mikono Mitume Kumi na Wawili","mp3":"\/mp3\/13871\/0117_swa_f_30_awekea_mikono_mitume_kumi_na_wawili_13871_1081.mp3#duration=405&size=4147140"},{"para_id":"13871.1100","title":"31 \u2014 Mahubiri Mlimani","mp3":"\/mp3\/13871\/0119_swa_f_31_mahubiri_mlimani_13871_1100.mp3#duration=1556&size=25001595"},{"para_id":"13871.1172","title":"32 \u2014 Afisa wa Jeshi Aomba Msaada Kwa Ajili Mtumishi Wake","mp3":"\/mp3\/13871\/0125_swa_f_32_afisa_wa_jeshi_aomba_msaada_kwa_ajili_mtumishi_wake_13871_1172.mp3#duration=533&size=8636236"},{"para_id":"13871.1199","title":"33 \u2014 Jinsi Yesu Alivyojihusisha na Matatizo ya Jamaa","mp3":"\/mp3\/13871\/0127_swa_f_33_jinsi_yesu_alivyojihusisha_na_matatizo_ya_jamaa_13871_1199.mp3#duration=744&size=11999844"},{"para_id":"13871.1229","title":"34 \u2014 Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi","mp3":"\/mp3\/13871\/0130_swa_f_34_nira_yake_ni_laini_na_mzigo_wake_ni_mwepesi_13871_1229.mp3#duration=511&size=8279056"},{"para_id":"13871.1255","title":"35 \u2014 Kutuliza Dhoruba","mp3":"\/mp3\/13871\/0133_swa_f_35_kutuliza_dhoruba_13871_1255.mp3#duration=953&size=15344257"},{"para_id":"13871.1299","title":"36 \u2014 Mguso wa Imani","mp3":"\/mp3\/13871\/0136_swa_f_36_mguso_wa_imani_13871_1299.mp3#duration=457&size=7409111"},{"para_id":"13871.1320","title":"37 \u2014 Wainjilisti wa Kwanza","mp3":"\/mp3\/13871\/0138_swa_f_37_wainjilisti_wa_kwanza_13871_1320.mp3#duration=804&size=12970024"},{"para_id":"13871.1358","title":"38 \u2014 Kristo na Wanafunzi Wapumzika","mp3":"\/mp3\/13871\/0141_swa_f_38_kristo_na_wanafunzi_wapumzika_13871_1358.mp3#duration=504&size=8168554"},{"para_id":"13871.1385","title":"39 \u2014 \u201cWapeni Ninyi Chakula\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0144_swa_f_39_wapeni_ninyi_chakula_13871_1385.mp3#duration=299&size=4886983"},{"para_id":"13871.1413","title":"40 \u2014 Usiku Ziwani","mp3":"\/mp3\/13871\/0147_swa_f_40_usiku_ziwani_13871_1413.mp3#duration=639&size=10325621"},{"para_id":"13871.1445","title":"41 \u2014 Hatari Katika Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0150_swa_f_41_hatari_katika_galilaya_13871_1445.mp3#duration=1322&size=21255291"},{"para_id":"13871.1509","title":"42 \u2014 Kristo Atabiri Juu ya Maanguko","mp3":"\/mp3\/13871\/0157_swa_f_42_kristo_atabiri_juu_ya_maanguko_13871_1509.mp3#duration=310&size=3197643"},{"para_id":"13871.1527","title":"43 \u2014 Kristo Avunja Ubaguzi wa Mataifa","mp3":"\/mp3\/13871\/0159_swa_f_43_kristo_avunja_ubaguzi_wa_mataifa_13871_1527.mp3#duration=551&size=5609425"},{"para_id":"13871.1551","title":"44 \u2014 Ishara ya Kweli","mp3":"\/mp3\/13871\/0161_swa_f_44_ishara_ya_kweli_13871_1551.mp3#duration=684&size=6941240"},{"para_id":"13871.1582","title":"45 \u2014 Kuonyeshwa Mbele Fumbo la Msalaba","mp3":"\/mp3\/13871\/0165_swa_f_45_kuonyeshwa_mbele_fumbo_la_msalaba_13871_1582.mp3#duration=1145&size=11549078"},{"para_id":"13871.1631","title":"46 \u2014 Yesu Ageuka Sura","mp3":"\/mp3\/13871\/0169_swa_f_46_yesu_ageuka_sura_13871_1631.mp3#duration=510&size=5201013"},{"para_id":"13871.1653","title":"47 \u2014 Kupingana na Roho za Mashetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0171_swa_f_47_kupingana_na_roho_za_mashetani_13871_1653.mp3#duration=530&size=5405611"},{"para_id":"13871.1675","title":"48 \u2014 Nani Aliye Mkubwa Zaidi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0173_swa_f_48_nani_aliye_mkubwa_zaidi_13871_1675.mp3#duration=1120&size=11299793"},{"para_id":"13871.1724","title":"49 \u2014 \u201cMtu Akiwa na Kiu, na Aje\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0177_swa_f_49_mtu_akiwa_na_kiu_na_aje_13871_1724.mp3#duration=703&size=7128511"},{"para_id":"13871.1758","title":"50 \u2014 Katikati ya Mitego","mp3":"\/mp3\/13871\/0180_swa_f_50_katikati_ya_mitego_13871_1758.mp3#duration=856&size=8662407"},{"para_id":"13871.1798","title":"51 \u2014 Nuru ya Uzima","mp3":"\/mp3\/13871\/0184_swa_f_51_nuru_ya_uzima_13871_1798.mp3#duration=1310&size=13204222"},{"para_id":"13871.1859","title":"52 \u2014 Mchungaji, Mungu","mp3":"\/mp3\/13871\/0190_swa_f_52_mchungaji_mungu_13871_1859.mp3#duration=580&size=5898525"},{"para_id":"13871.1886","title":"53 \u2014 Safari ya Mwisho Kutoka Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0194_swa_f_53_safari_ya_mwisho_kutoka_galilaya_13871_1886.mp3#duration=863&size=8730237"},{"para_id":"13871.1925","title":"54 \u2014 Msamaria Mwema","mp3":"\/mp3\/13871\/0198_swa_f_54_msamaria_mwema_13871_1925.mp3#duration=616&size=6260151"},{"para_id":"13871.1952","title":"55 \u2014 Si Kujionyesha kwa Nje","mp3":"\/mp3\/13871\/0200_swa_f_55_si_kujionyesha_kwa_nje_13871_1952.mp3#duration=433&size=4434757"},{"para_id":"13871.1971","title":"56 \u2014 Upendo wa Yesu kwa Watoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0201_swa_f_56_upendo_wa_yesu_kwa_watoto_13871_1971.mp3#duration=543&size=5526138"},{"para_id":"13871.1996","title":"57 \u2014 Kijana Tajiri Mtawala Amepungukiwa na jambo Moja","mp3":"\/mp3\/13871\/0203_swa_f_57_kijana_tajiri_mtawala_amepungukiwa_na_jambo_moja_13871_1996.mp3#duration=478&size=4879601"},{"para_id":"13871.2019","title":"58 \u2014 Kufufuliwa kwa Lazaro","mp3":"\/mp3\/13871\/0205_swa_f_58_kufufuliwa_kwa_lazaro_13871_2019.mp3#duration=1099&size=11092144"},{"para_id":"13871.2066","title":"59 \u2014 Makuhani na Wakuu Wanaendelea na Njama Yao","mp3":"\/mp3\/13871\/0206_swa_f_59_makuhani_na_wakuu_wanaendelea_na_njama_yao_13871_2066.mp3#duration=454&size=4641463"},{"para_id":"13871.2088","title":"60 \u2014 Cheo Kikuu Ni Kipi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0208_swa_f_60_cheo_kikuu_ni_kipi_13871_2088.mp3#duration=406&size=4158184"},{"para_id":"13871.2112","title":"61 \u2014 Mtu Mfupi Aliyekuwa Mashuhuri","mp3":"\/mp3\/13871\/0210_swa_f_61_mtu_mfupi_aliyekuwa_mashuhuri_13871_2112.mp3#duration=401&size=4111640"},{"para_id":"13871.2133","title":"62 \u2014 Mariamu Ampaka Yesu Mafuta","mp3":"\/mp3\/13871\/0211_swa_f_62_mariamu_ampaka_yesu_mafuta_13871_2133.mp3#duration=1307&size=13170907"},{"para_id":"13871.2190","title":"63 \u2014 Yesu Atangazwa Kuwa Mfalme wa Israeli","mp3":"\/mp3\/13871\/0218_swa_f_63_yesu_atangazwa_kuwa_mfalme_wa_israeli_13871_2190.mp3#duration=707&size=7169996"},{"para_id":"13871.2232","title":"64 \u2014 Watu wa Kuangamia","mp3":"\/mp3\/13871\/0222_swa_f_64_watu_wa_kuangamia_13871_2232.mp3#duration=693&size=7031722"},{"para_id":"13871.2263","title":"65 \u2014 Hekalu Latakaswa Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0224_swa_f_65_hekalu_latakaswa_tena_13871_2263.mp3#duration=1329&size=13390450"},{"para_id":"13871.2316","title":"66 \u2014 Kristo Akabiliana na Adui Zake","mp3":"\/mp3\/13871\/0228_swa_f_66_kristo_akabiliana_na_adui_zake_13871_2316.mp3#duration=740&size=7505171"},{"para_id":"13871.2352","title":"67 \u2014 Yesu Azuru Hekalu Mara ya Mwisho","mp3":"\/mp3\/13871\/0231_swa_f_67_yesu_azuru_hekalu_mara_ya_mwisho_13871_2352.mp3#duration=1219&size=12295749"},{"para_id":"13871.2400","title":"68 \u2014 Wayunani Walipotaka \u201cKumwona Yesu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0233_swa_f_68_wayunani_walipotaka_kumwona_yesu_13871_2400.mp3#duration=666&size=6756313"},{"para_id":"13871.2430","title":"69 \u2014 Dalili za Kuja Kwa Kristo Mara ya Pili","mp3":"\/mp3\/13871\/0235_swa_f_69_dalili_za_kuja_kwa_kristo_mara_ya_pili_13871_2430.mp3#duration=1155&size=11655117"},{"para_id":"13871.2473","title":"70 \u2014 Kristo Ashirikiana na Wenye Dhiki na Masikini","mp3":"\/mp3\/13871\/0239_swa_f_70_kristo_ashirikiana_na_wenye_dhiki_na_masikini_13871_2473.mp3#duration=566&size=5758478"},{"para_id":"13871.2498","title":"71 \u2014 Mtumishi wa Watumishi","mp3":"\/mp3\/13871\/0241_swa_f_71_mtumishi_wa_watumishi_13871_2498.mp3#duration=943&size=9526890"},{"para_id":"13871.2539","title":"72 \u2014 Meza ya Bwana Yaanzishwa","mp3":"\/mp3\/13871\/0243_swa_f_72_meza_ya_bwana_yaanzishwa_13871_2539.mp3#duration=958&size=9677405"},{"para_id":"13871.2576","title":"73 \u2014 \u201cMsifadhaike Mioyoni Mwenu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0246_swa_f_73_msifadhaike_mioyoni_mwenu_13871_2576.mp3#duration=1908&size=19179012"},{"para_id":"13871.2641","title":"74 \u2014 Pambano la Kutisha Katika Gethsemane","mp3":"\/mp3\/13871\/0251_swa_f_74_pambano_la_kutisha_katika_gethsemane_13871_2641.mp3#duration=1080&size=10900601"},{"para_id":"13871.2688","title":"75 \u2014 Kesi Batili Dhidi ya Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0256_swa_f_75_kesi_batili_dhidi_ya_yesu_13871_2688.mp3#duration=1590&size=25543110"},{"para_id":"13871.2752","title":"76 \u2014 Jinsi Yuda Alivyopoteza Roho Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0262_swa_f_76_jinsi_yuda_alivyopoteza_roho_yake_13871_2752.mp3#duration=692&size=7020406"},{"para_id":"13871.2784","title":"77 \u2014 Kristo Ashtakiwa Mbele Ya Gavana Wa Kirumi","mp3":"\/mp3\/13871\/0266_swa_f_77_kristo_ashtakiwa_mbele_ya_gavana_wa_kirumi_13871_2784.mp3#duration=1936&size=19458815"},{"para_id":"13871.2868","title":"78 \u2014 Yesu Afa Juu Ya Kalwari","mp3":"\/mp3\/13871\/0274_swa_f_78_yesu_afa_juu_ya_kalwari_13871_2868.mp3#duration=1671&size=16811964"},{"para_id":"13871.2932","title":"79 \u2014 Jinsi Kifo Cha Kristo Kilivyomshinda Shetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0281_swa_f_79_jinsi_kifo_cha_kristo_kilivyomshinda_shetani_13871_2932.mp3#duration=884&size=8938225"},{"para_id":"13871.2968","title":"80 \u2014 Yesu Apumzika Katika Kaburi La Yusufu","mp3":"\/mp3\/13871\/0285_swa_f_80_yesu_apumzika_katika_kaburi_la_yusufu_13871_2968.mp3#duration=708&size=7178978"},{"para_id":"13871.2994","title":"81 \u2014 \u201cBwana Amefufuka\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0288_swa_f_81_bwana_amefufuka_13871_2994.mp3#duration=562&size=5718538"},{"para_id":"13871.3022","title":"82 \u2014 \u201cMama Unalilia Nini?","mp3":"\/mp3\/13871\/0292_swa_f_82_mama_unalilia_nini_13871_3022.mp3#duration=578&size=5878775"},{"para_id":"13871.3051","title":"83 \u2014 Kutembea Kwenda Emau","mp3":"\/mp3\/13871\/0293_swa_f_83_kutembea_kwenda_emau_13871_3051.mp3#duration=498&size=5083897"},{"para_id":"13871.3073","title":"84 \u2014 Kristo Aliyefufuka Atokea","mp3":"\/mp3\/13871\/0296_swa_f_84_kristo_aliyefufuka_atokea_13871_3073.mp3#duration=595&size=6053282"},{"para_id":"13871.3100","title":"85 \u2014 Kando Ya Bahari Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0299_swa_f_85_kando_ya_bahari_tena_13871_3100.mp3#duration=789&size=12730367"},{"para_id":"13871.3133","title":"86 \u2014 \u201cEnendeni . . . Mkawafanye Mataifa Yote\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0302_swa_f_86_enendeni_mkawafanye_mataifa_yote_13871_3133.mp3#duration=936&size=15074513"},{"para_id":"13871.3172","title":"87 \u2014 Kristo Aingia Mbinguni Kwa Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0306_swa_f_87_kristo_aingia_mbinguni_kwa_ushindi_13871_3172.mp3#duration=691&size=11154751"}]