Nikodemo aanza kuona mwanga
Wakati Yesu alipokuwa akizungumza, nuru ya ukweli ilipenya na kuingia moyoni mwa mkuu huyu. Walakini alikuwa bado kuelewa vizuri maneno ya Mwokozi. Akauliza, huku akishangaa mambo haya yanawezaje kuwa?” Yesu akajibu: “Wewe uliye mwalimu wa Israeli, hujui mambo haya?” Badala ya kuchangamka, Nikodemo angalipaswa kunyenyekea na kujidhili kwa ajili ya ujinga wake wa kutojua mambo. Walakini Yesu alimzungumzia kwa ufasaha sana ili asichukizwe. Lakini Yesu alipomweleza kuwa kazi yake ni kusimamisha ufalme wa kiroho, wala si wa dunia, Nikodemo alitiwa wasiwasi. Yesu alipoona hivyo, aliongeza kusema: “Kama nimekuambia mambo ya dunia, nawe hukuamini, utaaminije nikikuambia mambo ya mbinguni?” Ikiwa hakufahamu kazi ya Yesu duniani, atafahamuje kazi yake mbinguni?
TVV 91.2
Wayahudi walifukuzwa na Yesu hekaluni, walikuwa na juhudi ya kujionyesha kuwa ni watakatifu kijuujuu, lakini hawakuwa watakatifu mioyoni. Walikuwa na juhudi kukariri sheria, huku wakiziasi mioyoni mwao. Haja yao kubwa ilikuwa kubadilika katika maisha kama Yesu alivyomwambia Nikodemo, yaani kuzaliwa upya kiroho, kutakasika kutokana na dhambi, na kufanywa upya katika utakatifu.
TVV 91.3
Hapakuwa na udhuru kwa Waisraeli kuhusu mabadiliko ya mioyo. Daudi alikuwa ameomba: “Ee Mungu uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.” Ahadi ilitolewa kwa njia ya Ezekieli: “Nitawapa roho mpya, nitawawekea moyo mpya, nitawondolea moyo wa jiwe, nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia ndani yenu Roho yangu, ili mwenende katika amri zangu.” Zaburi 51:10; Ezekieli 36:26, 27. Nikodemo sasa alianza kufahamu maana ya fungu hili. Akaona kuwa kung’ang’ania kushika na kukariri kariri sheria hakutaweza kamwe kumpeleka mtu mbinguni.
TVV 91.4
Nikodemo alivutwa kwa Kristo sasa. Mwokozi alipomweleza habari ya kuzaliwa upya, alitamani hali hiyo ionekane kwake mwenyewe. Itafanyikaje? Yesu akasema: “Kama Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuli wa, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
TVV 92.1
Mfano wa kuinuliwa kwa nyoka kulimfanya Nikodemo aelewe kazi ya Mwokozi. Wakati Waisraeli walipokuwa wakifa kwa kuumwa na majoka, Mungu alimwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba, na kumwinua katikati ya mkutano. Wote watakaomwangalia wangeliishi. Nyoka wa shaba alikuwa mfano wa Kristo. Kama mfano ulivyofanywa wa nyoka aharibuye, aliinuliwa kwa ukombozi wao. Vivyo hivyo aliyetwaa hali ya binadamu mwenye dhambi, ndiye atakuwa Mwokozi wao. Warumi 8:3. Mungu alitamani kuwaongoza Waisraeli wamwone Mwokozi. Wamwone kwa kuponywa majeraha yao au kwa kusamehewa dhambi zao. Wasingeweza kufanya lolote kwa nguvu zao, ila wamwamini Yesu, ambaye ni kipawa cha Mungu, Iliwapasa kumwangalia na kuishi.
TVV 92.2
Wale walioumwa na nyoka, wangelidai wafahamu kwa njia ya kitaalam. Lakini hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu kupona kwao. Waliokataa kuangalia waliangamia. Nikodemo alilipokea fundisho hilo akalikubali. Alichunguza maandiko ili apate uzima kwa kuamini na kujitoa zaidi. Roho Mtakatifu akamwongoza, naye akakubaliana na uongozi huo.
TVV 92.3
Leo watu maelfu wanahitaji kujifunza fundisho lile la kuinuliwa kwa nyoka, alilojifunza Nikodemo. “Hakuna jina jingine chini ya mbingu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Matendo 4:12. Tunapokea neema ya Mungu kwa imani, lakini imani siyo wokovu wetu. Haileti chochote. Ni mkono tu unaoweza kumshika Kristo, ambaye ndiye dawa ya dhambi. Hatuwezi hata kutubu bila msaada wa Roho wa Mungu. Maandiko husema juu ya Kristo Mtu huyu Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisrael toba na msamaha wa dhambi.” Matendo 5:31. Toba hutoka kwa Kristo, kama vile msamaha wa dhambi.
TVV 92.4
Sisi basi tutaokolewaje? “Tazama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana 1:29. Nuru inayong’aa kutoka msalabani huufunua upendo wa Mungu. Upendo wake hutuvuta kwake. Tusipokaidi upendo huu tutaongozwa mpaka chini ya msalaba kwa kutubu dhambi zile zilizomsulubisha Mwokozi. Halafu Roho wa Mungu huleta uzima mpya kwa imani. Ndipo mawazo, na hamu ya mtu humtii Kristo. Moyo na nia huumbika upya kwa mfano wake atendaye kazi ndani yetu, ambaye huvihisha vyote chini yake. Halafu sheria ya Mungu huandikwa katika dhamiri zetu na roho zetu, nasi tunaweza kusema pamoja na Kristo, kwamba: “Kuyafanya mapenzi yako, ee Mungu, ndiyo furaha yangu.” Zaburi 40:8
TVV 92.5
Katika mazungumzo ya Yesu na Nikodemo, Yesu aliufunua mpango wa wokovu. Katika hotuba zake zote, hakuna hata moja ambayo alieleza mpango wa wokovu kwa ukamilifu hatua kwa hatua kazi inayopaswa kutendwa katika moyo wa mtu yeyote atakayeurithi ufalme wa mbinguni. Tangu mwanzo wa kazi yake, alieleza ukweli kamili kwa mbunge huyu wa Sanhedrin, ambaye ni mwalimu wa watu wa Israeli. Lakini viongozi wa Israel hawakuikubali nuru. Nikodemo alihifadhi kweli ya Mungu moyoni mwake, na kwa muda wa miaka mitatu matunda yalikuwa kidogo sana.
TVV 93.1
Lakini maneno yaliyosemwa usiku katika mlima hayakupotea. Katika baraza la Sanhedrin Nikodemo alikazia kuuvunja mpango wa kumwangamiza Yesu. Mwishoni Yesu aliposulubishwa Nikodemo alikumbuka maneno ya Yesu kwamba “Kama Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.” Nuru kutokana na maongezi ya usiku ilimulika msalabani pale Kalwari, na Nikodemo akamwona Yesu kuwa ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
TVV 93.2
Baada ya kufufuka kwake Bwana, wakati wanafunzi wametawanyika kwa ajili ya mateso. Nikodemo alijitokeza mbele. Alitumia mali yake kulisaidia kanisa, changa ambalo Wayahudi walikusudia kuliangamiza wakati wa kifo cha Kristo. Wakati wa hatari, Nikodemo aliyekuwa mwenye maswali na wasiwasi, alisimama imara kama mwamba, akiitetea imani na kulisaidia kahisa lipate kueneza Injili. Alitoa mali yote, akabaki kuwa maskini, lakini aliimarika katika imani aliyoipata wakati wa mazungunzo ya usiku.
TVV 93.3
Nikodemo alihusiana na Yohana kwa damu kwa historia iliyosemwa, na kwa kalamu ya kuwafundisha watu mamilioni. Ukweli wanaofundisha leo ni muhimu kama ulivyokuwa wakati wa maongezi ya usiku, wakati mtu mkuu alipokuja kujifunza kwa mnyenyekevu wa Galilaya.
TVV 93.4
13871
TVV
Tumaini la Vizazi Vyote
[{"para_id":"13871.97","title":"4 \u2014 Kuzaliwa Zizini","mp3":"\/mp3\/13871\/0014_swa_f_4_kuzaliwa_zizini_13871_97.mp3#duration=342&size=5577659"},{"para_id":"13871.145","title":"6 \u2014 Tumeiona Nyota Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0020_swa_f_6_tumeiona_nyota_yake_13871_145.mp3#duration=699&size=11277784"},{"para_id":"13871.184","title":"7 \u2014 Mtoto Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0025_swa_f_7_mtoto_yesu_13871_184.mp3#duration=598&size=6083499"},{"para_id":"13871.216","title":"8 \u2014 Kuhudhuria Katika Pasaka","mp3":"\/mp3\/13871\/0029_swa_f_8_kuhudhuria_katika_pasaka_13871_216.mp3#duration=664&size=6739433"},{"para_id":"13871.248","title":"9 \u2014 Matatizo ya Kristo Wakati wa Utoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0032_swa_f_9_matatizo_ya_kristo_wakati_wa_utoto_13871_248.mp3#duration=834&size=8439843"},{"para_id":"13871.282","title":"10 \u2014 Sauti Nyikani","mp3":"\/mp3\/13871\/0036_swa_f_10_sauti_nyikani_13871_282.mp3#duration=1057&size=10667758"},{"para_id":"13871.336","title":"11 \u2014 Ubatizo wa Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0042_swa_f_11_ubatizo_wa_yesu_13871_336.mp3#duration=478&size=4879322"},{"para_id":"13871.360","title":"12 \u2014 Majaribu","mp3":"\/mp3\/13871\/0045_swa_f_12_majaribu_13871_360.mp3#duration=977&size=9870882"},{"para_id":"13871.401","title":"13 \u2014 Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0050_swa_f_13_ushindi_13871_401.mp3#duration=623&size=6329203"},{"para_id":"13871.428","title":"14 \u2014 Tumemwona Masihi","mp3":"\/mp3\/13871\/0054_swa_f_14_tumemwona_masihi_13871_428.mp3#duration=1307&size=13172069"},{"para_id":"13871.485","title":"15 \u2014 Yesu Ahudhuria Harusi","mp3":"\/mp3\/13871\/0060_swa_f_15_yesu_ahudhuria_harusi_13871_485.mp3#duration=932&size=9423837"},{"para_id":"13871.527","title":"16 \u2014 Kristo Akabili Machafuko Hekaluni","mp3":"\/mp3\/13871\/0063_swa_f_16_kristo_akabili_machafuko_hekaluni_13871_527.mp3#duration=1374&size=13844801"},{"para_id":"13871.579","title":"17 \u2014 Nikodemo Amwendea Yesu Wakati wa Usiku","mp3":"\/mp3\/13871\/0068_swa_f_17_nikodemo_amwendea_yesu_wakati_wa_usiku_13871_579.mp3#duration=1110&size=11198316"},{"para_id":"13871.619","title":"18 \u2014 Yeye Hana Budi Kuzidi Bali Mimi Kupungua\u2019","mp3":"\/mp3\/13871\/0071_swa_f_18_yeye_hana_budi_kuzidi_bali_mimi_kupungua_13871_619.mp3#duration=392&size=4024084"},{"para_id":"13871.640","title":"19 \u2014 Yesu na Mwanawke Mwenye Waume Watano","mp3":"\/mp3\/13871\/0073_swa_f_19_yesu_na_mwanawke_mwenye_waume_watano_13871_640.mp3#duration=1095&size=11052730"},{"para_id":"13871.695","title":"20 \u2014 \u201cMsipoona Ishara na Maajabu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0078_swa_f_20_msipoona_ishara_na_maajabu_13871_695.mp3#duration=404&size=4140487"},{"para_id":"13871.715","title":"21 \u2014 Bethzatha na Sanhedrin","mp3":"\/mp3\/13871\/0079_swa_f_21_bethzatha_na_sanhedrin_13871_715.mp3#duration=1404&size=22570477"},{"para_id":"13871.777","title":"22 \u2014 Kifungo na Kifo cha Yohana","mp3":"\/mp3\/13871\/0086_swa_f_22_kifungo_na_kifo_cha_yohana_13871_777.mp3#duration=1163&size=11730972"},{"para_id":"13871.830","title":"23 \u2014 Jinsi Danieli Alivyomtambua Yesu kuwa ni Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0092_swa_f_23_jinsi_danieli_alivyomtambua_yesu_kuwa_ni_kristo_13871_830.mp3#duration=543&size=5530218"},{"para_id":"13871.851","title":"24 \u2014 \u201cJe, Huyu Siye Mwana wa Seremala?\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0094_swa_f_24_je_huyu_siye_mwana_wa_seremala_13871_851.mp3#duration=718&size=7276333"},{"para_id":"13871.885","title":"25 \u2014 Mwito Kando ya Bahari","mp3":"\/mp3\/13871\/0096_swa_f_25_mwito_kando_ya_bahari_13871_885.mp3#duration=618&size=6283618"},{"para_id":"13871.911","title":"26 \u2014 Siku za Shughuli na Raha katika Kapernaumu","mp3":"\/mp3\/13871\/0100_swa_f_26_siku_za_shughuli_na_raha_katika_kapernaumu_13871_911.mp3#duration=1004&size=10145925"},{"para_id":"13871.955","title":"27 \u2014 Mwenye Ukoma wa Kwanza Kuponywa na Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0103_swa_f_27_mwenye_ukoma_wa_kwanza_kuponywa_na_kristo_13871_955.mp3#duration=999&size=10093329"},{"para_id":"13871.1004","title":"28 \u2014 Mathayo: Kutoka Kutoza Ushuru Mpaka Mwanafunzi","mp3":"\/mp3\/13871\/0107_swa_f_28_mathayo_kutoka_kutoza_ushuru_mpaka_mwanafunzi_13871_1004.mp3#duration=830&size=8399583"},{"para_id":"13871.1042","title":"29 \u2014 Yesu Aiokoa Sabato","mp3":"\/mp3\/13871\/0112_swa_f_29_yesu_aiokoa_sabato_13871_1042.mp3#duration=933&size=9434863"},{"para_id":"13871.1081","title":"30 \u2014 Awekea Mikono Mitume Kumi na Wawili","mp3":"\/mp3\/13871\/0117_swa_f_30_awekea_mikono_mitume_kumi_na_wawili_13871_1081.mp3#duration=405&size=4147140"},{"para_id":"13871.1100","title":"31 \u2014 Mahubiri Mlimani","mp3":"\/mp3\/13871\/0119_swa_f_31_mahubiri_mlimani_13871_1100.mp3#duration=1556&size=25001595"},{"para_id":"13871.1172","title":"32 \u2014 Afisa wa Jeshi Aomba Msaada Kwa Ajili Mtumishi Wake","mp3":"\/mp3\/13871\/0125_swa_f_32_afisa_wa_jeshi_aomba_msaada_kwa_ajili_mtumishi_wake_13871_1172.mp3#duration=533&size=8636236"},{"para_id":"13871.1199","title":"33 \u2014 Jinsi Yesu Alivyojihusisha na Matatizo ya Jamaa","mp3":"\/mp3\/13871\/0127_swa_f_33_jinsi_yesu_alivyojihusisha_na_matatizo_ya_jamaa_13871_1199.mp3#duration=744&size=11999844"},{"para_id":"13871.1229","title":"34 \u2014 Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi","mp3":"\/mp3\/13871\/0130_swa_f_34_nira_yake_ni_laini_na_mzigo_wake_ni_mwepesi_13871_1229.mp3#duration=511&size=8279056"},{"para_id":"13871.1255","title":"35 \u2014 Kutuliza Dhoruba","mp3":"\/mp3\/13871\/0133_swa_f_35_kutuliza_dhoruba_13871_1255.mp3#duration=953&size=15344257"},{"para_id":"13871.1299","title":"36 \u2014 Mguso wa Imani","mp3":"\/mp3\/13871\/0136_swa_f_36_mguso_wa_imani_13871_1299.mp3#duration=457&size=7409111"},{"para_id":"13871.1320","title":"37 \u2014 Wainjilisti wa Kwanza","mp3":"\/mp3\/13871\/0138_swa_f_37_wainjilisti_wa_kwanza_13871_1320.mp3#duration=804&size=12970024"},{"para_id":"13871.1358","title":"38 \u2014 Kristo na Wanafunzi Wapumzika","mp3":"\/mp3\/13871\/0141_swa_f_38_kristo_na_wanafunzi_wapumzika_13871_1358.mp3#duration=504&size=8168554"},{"para_id":"13871.1385","title":"39 \u2014 \u201cWapeni Ninyi Chakula\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0144_swa_f_39_wapeni_ninyi_chakula_13871_1385.mp3#duration=299&size=4886983"},{"para_id":"13871.1413","title":"40 \u2014 Usiku Ziwani","mp3":"\/mp3\/13871\/0147_swa_f_40_usiku_ziwani_13871_1413.mp3#duration=639&size=10325621"},{"para_id":"13871.1445","title":"41 \u2014 Hatari Katika Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0150_swa_f_41_hatari_katika_galilaya_13871_1445.mp3#duration=1322&size=21255291"},{"para_id":"13871.1509","title":"42 \u2014 Kristo Atabiri Juu ya Maanguko","mp3":"\/mp3\/13871\/0157_swa_f_42_kristo_atabiri_juu_ya_maanguko_13871_1509.mp3#duration=310&size=3197643"},{"para_id":"13871.1527","title":"43 \u2014 Kristo Avunja Ubaguzi wa Mataifa","mp3":"\/mp3\/13871\/0159_swa_f_43_kristo_avunja_ubaguzi_wa_mataifa_13871_1527.mp3#duration=551&size=5609425"},{"para_id":"13871.1551","title":"44 \u2014 Ishara ya Kweli","mp3":"\/mp3\/13871\/0161_swa_f_44_ishara_ya_kweli_13871_1551.mp3#duration=684&size=6941240"},{"para_id":"13871.1582","title":"45 \u2014 Kuonyeshwa Mbele Fumbo la Msalaba","mp3":"\/mp3\/13871\/0165_swa_f_45_kuonyeshwa_mbele_fumbo_la_msalaba_13871_1582.mp3#duration=1145&size=11549078"},{"para_id":"13871.1631","title":"46 \u2014 Yesu Ageuka Sura","mp3":"\/mp3\/13871\/0169_swa_f_46_yesu_ageuka_sura_13871_1631.mp3#duration=510&size=5201013"},{"para_id":"13871.1653","title":"47 \u2014 Kupingana na Roho za Mashetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0171_swa_f_47_kupingana_na_roho_za_mashetani_13871_1653.mp3#duration=530&size=5405611"},{"para_id":"13871.1675","title":"48 \u2014 Nani Aliye Mkubwa Zaidi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0173_swa_f_48_nani_aliye_mkubwa_zaidi_13871_1675.mp3#duration=1120&size=11299793"},{"para_id":"13871.1724","title":"49 \u2014 \u201cMtu Akiwa na Kiu, na Aje\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0177_swa_f_49_mtu_akiwa_na_kiu_na_aje_13871_1724.mp3#duration=703&size=7128511"},{"para_id":"13871.1758","title":"50 \u2014 Katikati ya Mitego","mp3":"\/mp3\/13871\/0180_swa_f_50_katikati_ya_mitego_13871_1758.mp3#duration=856&size=8662407"},{"para_id":"13871.1798","title":"51 \u2014 Nuru ya Uzima","mp3":"\/mp3\/13871\/0184_swa_f_51_nuru_ya_uzima_13871_1798.mp3#duration=1310&size=13204222"},{"para_id":"13871.1859","title":"52 \u2014 Mchungaji, Mungu","mp3":"\/mp3\/13871\/0190_swa_f_52_mchungaji_mungu_13871_1859.mp3#duration=580&size=5898525"},{"para_id":"13871.1886","title":"53 \u2014 Safari ya Mwisho Kutoka Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0194_swa_f_53_safari_ya_mwisho_kutoka_galilaya_13871_1886.mp3#duration=863&size=8730237"},{"para_id":"13871.1925","title":"54 \u2014 Msamaria Mwema","mp3":"\/mp3\/13871\/0198_swa_f_54_msamaria_mwema_13871_1925.mp3#duration=616&size=6260151"},{"para_id":"13871.1952","title":"55 \u2014 Si Kujionyesha kwa Nje","mp3":"\/mp3\/13871\/0200_swa_f_55_si_kujionyesha_kwa_nje_13871_1952.mp3#duration=433&size=4434757"},{"para_id":"13871.1971","title":"56 \u2014 Upendo wa Yesu kwa Watoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0201_swa_f_56_upendo_wa_yesu_kwa_watoto_13871_1971.mp3#duration=543&size=5526138"},{"para_id":"13871.1996","title":"57 \u2014 Kijana Tajiri Mtawala Amepungukiwa na jambo Moja","mp3":"\/mp3\/13871\/0203_swa_f_57_kijana_tajiri_mtawala_amepungukiwa_na_jambo_moja_13871_1996.mp3#duration=478&size=4879601"},{"para_id":"13871.2019","title":"58 \u2014 Kufufuliwa kwa Lazaro","mp3":"\/mp3\/13871\/0205_swa_f_58_kufufuliwa_kwa_lazaro_13871_2019.mp3#duration=1099&size=11092144"},{"para_id":"13871.2066","title":"59 \u2014 Makuhani na Wakuu Wanaendelea na Njama Yao","mp3":"\/mp3\/13871\/0206_swa_f_59_makuhani_na_wakuu_wanaendelea_na_njama_yao_13871_2066.mp3#duration=454&size=4641463"},{"para_id":"13871.2088","title":"60 \u2014 Cheo Kikuu Ni Kipi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0208_swa_f_60_cheo_kikuu_ni_kipi_13871_2088.mp3#duration=406&size=4158184"},{"para_id":"13871.2112","title":"61 \u2014 Mtu Mfupi Aliyekuwa Mashuhuri","mp3":"\/mp3\/13871\/0210_swa_f_61_mtu_mfupi_aliyekuwa_mashuhuri_13871_2112.mp3#duration=401&size=4111640"},{"para_id":"13871.2133","title":"62 \u2014 Mariamu Ampaka Yesu Mafuta","mp3":"\/mp3\/13871\/0211_swa_f_62_mariamu_ampaka_yesu_mafuta_13871_2133.mp3#duration=1307&size=13170907"},{"para_id":"13871.2190","title":"63 \u2014 Yesu Atangazwa Kuwa Mfalme wa Israeli","mp3":"\/mp3\/13871\/0218_swa_f_63_yesu_atangazwa_kuwa_mfalme_wa_israeli_13871_2190.mp3#duration=707&size=7169996"},{"para_id":"13871.2232","title":"64 \u2014 Watu wa Kuangamia","mp3":"\/mp3\/13871\/0222_swa_f_64_watu_wa_kuangamia_13871_2232.mp3#duration=693&size=7031722"},{"para_id":"13871.2263","title":"65 \u2014 Hekalu Latakaswa Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0224_swa_f_65_hekalu_latakaswa_tena_13871_2263.mp3#duration=1329&size=13390450"},{"para_id":"13871.2316","title":"66 \u2014 Kristo Akabiliana na Adui Zake","mp3":"\/mp3\/13871\/0228_swa_f_66_kristo_akabiliana_na_adui_zake_13871_2316.mp3#duration=740&size=7505171"},{"para_id":"13871.2352","title":"67 \u2014 Yesu Azuru Hekalu Mara ya Mwisho","mp3":"\/mp3\/13871\/0231_swa_f_67_yesu_azuru_hekalu_mara_ya_mwisho_13871_2352.mp3#duration=1219&size=12295749"},{"para_id":"13871.2400","title":"68 \u2014 Wayunani Walipotaka \u201cKumwona Yesu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0233_swa_f_68_wayunani_walipotaka_kumwona_yesu_13871_2400.mp3#duration=666&size=6756313"},{"para_id":"13871.2430","title":"69 \u2014 Dalili za Kuja Kwa Kristo Mara ya Pili","mp3":"\/mp3\/13871\/0235_swa_f_69_dalili_za_kuja_kwa_kristo_mara_ya_pili_13871_2430.mp3#duration=1155&size=11655117"},{"para_id":"13871.2473","title":"70 \u2014 Kristo Ashirikiana na Wenye Dhiki na Masikini","mp3":"\/mp3\/13871\/0239_swa_f_70_kristo_ashirikiana_na_wenye_dhiki_na_masikini_13871_2473.mp3#duration=566&size=5758478"},{"para_id":"13871.2498","title":"71 \u2014 Mtumishi wa Watumishi","mp3":"\/mp3\/13871\/0241_swa_f_71_mtumishi_wa_watumishi_13871_2498.mp3#duration=943&size=9526890"},{"para_id":"13871.2539","title":"72 \u2014 Meza ya Bwana Yaanzishwa","mp3":"\/mp3\/13871\/0243_swa_f_72_meza_ya_bwana_yaanzishwa_13871_2539.mp3#duration=958&size=9677405"},{"para_id":"13871.2576","title":"73 \u2014 \u201cMsifadhaike Mioyoni Mwenu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0246_swa_f_73_msifadhaike_mioyoni_mwenu_13871_2576.mp3#duration=1908&size=19179012"},{"para_id":"13871.2641","title":"74 \u2014 Pambano la Kutisha Katika Gethsemane","mp3":"\/mp3\/13871\/0251_swa_f_74_pambano_la_kutisha_katika_gethsemane_13871_2641.mp3#duration=1080&size=10900601"},{"para_id":"13871.2688","title":"75 \u2014 Kesi Batili Dhidi ya Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0256_swa_f_75_kesi_batili_dhidi_ya_yesu_13871_2688.mp3#duration=1590&size=25543110"},{"para_id":"13871.2752","title":"76 \u2014 Jinsi Yuda Alivyopoteza Roho Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0262_swa_f_76_jinsi_yuda_alivyopoteza_roho_yake_13871_2752.mp3#duration=692&size=7020406"},{"para_id":"13871.2784","title":"77 \u2014 Kristo Ashtakiwa Mbele Ya Gavana Wa Kirumi","mp3":"\/mp3\/13871\/0266_swa_f_77_kristo_ashtakiwa_mbele_ya_gavana_wa_kirumi_13871_2784.mp3#duration=1936&size=19458815"},{"para_id":"13871.2868","title":"78 \u2014 Yesu Afa Juu Ya Kalwari","mp3":"\/mp3\/13871\/0274_swa_f_78_yesu_afa_juu_ya_kalwari_13871_2868.mp3#duration=1671&size=16811964"},{"para_id":"13871.2932","title":"79 \u2014 Jinsi Kifo Cha Kristo Kilivyomshinda Shetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0281_swa_f_79_jinsi_kifo_cha_kristo_kilivyomshinda_shetani_13871_2932.mp3#duration=884&size=8938225"},{"para_id":"13871.2968","title":"80 \u2014 Yesu Apumzika Katika Kaburi La Yusufu","mp3":"\/mp3\/13871\/0285_swa_f_80_yesu_apumzika_katika_kaburi_la_yusufu_13871_2968.mp3#duration=708&size=7178978"},{"para_id":"13871.2994","title":"81 \u2014 \u201cBwana Amefufuka\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0288_swa_f_81_bwana_amefufuka_13871_2994.mp3#duration=562&size=5718538"},{"para_id":"13871.3022","title":"82 \u2014 \u201cMama Unalilia Nini?","mp3":"\/mp3\/13871\/0292_swa_f_82_mama_unalilia_nini_13871_3022.mp3#duration=578&size=5878775"},{"para_id":"13871.3051","title":"83 \u2014 Kutembea Kwenda Emau","mp3":"\/mp3\/13871\/0293_swa_f_83_kutembea_kwenda_emau_13871_3051.mp3#duration=498&size=5083897"},{"para_id":"13871.3073","title":"84 \u2014 Kristo Aliyefufuka Atokea","mp3":"\/mp3\/13871\/0296_swa_f_84_kristo_aliyefufuka_atokea_13871_3073.mp3#duration=595&size=6053282"},{"para_id":"13871.3100","title":"85 \u2014 Kando Ya Bahari Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0299_swa_f_85_kando_ya_bahari_tena_13871_3100.mp3#duration=789&size=12730367"},{"para_id":"13871.3133","title":"86 \u2014 \u201cEnendeni . . . Mkawafanye Mataifa Yote\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0302_swa_f_86_enendeni_mkawafanye_mataifa_yote_13871_3133.mp3#duration=936&size=15074513"},{"para_id":"13871.3172","title":"87 \u2014 Kristo Aingia Mbinguni Kwa Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0306_swa_f_87_kristo_aingia_mbinguni_kwa_ushindi_13871_3172.mp3#duration=691&size=11154751"}]