Tumaini la Vizazi Vyote

47/307

Jaribu la kutia shaka

Neno lililotoka mbinguni, kwamba “Huyu ni Mwanangu mpendwa, lilikuwa lingali likisikika katika masikio ya Shetani. Lakini aliazimia kumpata Yesu asiliamini neno hilo. Neno la Mungu lilikuwa thibitisho la kazi ya Kristo kuwa ni ya mbinguni, maana neno hilo lilionyesha ushikamano wake na mbinguni. Ushikamano wa Kristo na mbingu ulikuwa imara usio tikiswa. Shetan alijua kuwa hawezi kumshinda Kristo. Alidhani kuwa kwa njia ya njaa na kukata tamaa, Kristo atakubali kutia shaka juu ya Babaye, na kufanya miujiza yeye binafsi. Kama angalifanya hivyo mpango wa wokovu ungalivunjika kabisa. TVV 58.4

Shetani alitegemea silaha yake kuu, malaika aliyefukuzwa kutoka mbinguni. Kuonekana kwa Yesu kulikuwa kama malaika aliyefukuzwa mbinguni na kudharauliwa na wanadamu. Basi mwenye asili ya Uungu angeonyesha uwezo wake kwa kufanya miujiza. “Kama wewe ni Mwana wa Mungu amuru mawe haya yawe mkate.” Shetani alisema kuwa kwa kutenda miujiza, kungekuwa uthibitisho wa Uungu wake. Basi mashaka yangekoma. TVV 59.1

Lakini Mwana wa Mungu asingemhakikishia Shetani Uungu wake. Kama Kristo angekubali mashauri ya Shetani, angelimwambia amwonyeshe ishara ya kuthibitisha kuwa yeye ni Mwana wa Mungu. Kristo asingetumia uwezo wa Uungu kwa kujiagiza. Amekuja kukabili mambo tunayokabili sisi, ili awe kielelezo chetu. Kazi zake za ajabu zote zilikuwa kwa ajili ya wengine. Akitiwa nguvu na ile sauti ya mbinguni, Yesu alitegemea neno la Baba tu. TVV 59.2

Yesu alikabiliana na Shetani kwa maandiko. “Imeandikwa”. Silaha yake ilikuwa maandiko. Shetani alidai Yesu afanye mwujiza. Lakini mwujiza mkuu kuliko yote ni “Hivyo ndivyo asemavyo Bwana.” Kristo aliposhikilia silaha hiyo, Shetani hakuwa na njia nyingine, ya kumweza. TVV 59.3

Wakati wa udhaifu mkuu, Kristo alishambuliwa na majaribu makali mno. Hivyo ndivyo Shetani anavyowatendea watu. Hesabu 20:1-17; 1 Wafalme 19:114. Mtu anaposhindwa na wasiwasi, au matatizo mengine, au ufukara, Shetani huwa tayari kushambulia. Hutushambulia kwenye hali zetu za udhaifu. Hutumaini kutudhoofisha na kututenga na Mungu. Lakini tukikabiliana naye kama Yesu alivyofanya, tutaepukana na kuanguka kwingi. TVV 59.4

Kristo alimwambia mjaribu, “Mtu haishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Katika jangwa kwa muda wa miaka elfu moja na mia nne iliyopita, Mungu alituma watu wake kuwalisha na chakula kutoka mbinguni. Jambo hili liliwafundisha kuwa kama wakimtumaini na kuenenda katika maagizo yake, hawezi kuwaacha. Kwa neno la Bwana Waebrania walilishwa huko jangwani. Na kwa neno hilo hilo Yesu alilishwa. Alimgojea Mungu ampe mahitaji yake kwa wakati wake. Asingepata chakula kwa kushauriwa na Shetani. Ni vizuri kuteseka kwa vyo vyote kuliko kujitenga na neno la Mungu. TVV 59.5

Mfuasi wa Mungu, mara kwa mara hufika mahali ambapo huonekana kuwa, kama akiambatana na mapenzi ya Mungu hatapata riziki yake. Shetani humfanya aamini kuwa kwa njia ya kujitenga na mapenzi ya Mungu kutamsaidia. Lakini jambo moja tu tuwezalo kutumaini ni uwezo wa neno la Mungu. Hatuwezi kufuata mashauri ya Shetani kuwa tukijenga neno la Mungu tutapungukiwa na riziki zetu. Lazima tushike amri yake na kuamini ahadi zake. TVV 59.6

Katika mashindano makuu ya mwisho pamoja na Shetani, wale wanaomtegemea Mungu, wataona kuwa mahitaji yao yanaondolewa, kwa sababu wanakataa kuvunja amri za Mungu. Watakatazwa kuuza na kununua. Soma Ufanuo 13:11-17. Lakini kwa watiifu wa amri za Mungu wamepewa ahadi, “Huyu ndiye atakayekaa juu, majabali ni ngome yake, atapewa chakula chake, maji yake hayatakoma.” Isaya 33:16. Wakati nchi itakapoangamizwa na njaa, yeye atalishwa. Zaburi 37-19 TVV 60.1