Dhambi ya Siri ya Petro
Sasa sauti ya Petro ilisikika ikipinga “Hata wajapo kunguwazwa wote, lakini siyo mimi” Yesu alikuwa amemwonya kwamba usiku ule atamkana Mwokozi wake. Sasa akarudia onyo lake akisema, “Amini, nakuambia wewe, Leo usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili utanikana mara tatu.” Lakini Petro “akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe, hata hivyo sitakukana kamwe. Na wote wakasema vile vile.” Marko 14:29-31).
TVV 381.5
Petro aliposema kuwa atamfuata Bwana wake hata kama ni gerezani au kifoni, alisema kweli, lakini hakujifahamu alivyo. Katika moyo wake kulifichika chembechembe za uovu ambazo hali halisi ya mambo ingezifunua wazi. Asipotahadharishwa juu ya hali hiyo ingemwingiza katika hatari ya kupotea. Mwokozi aliona ndani yake kujipenda ambako kungelemea upendo wake kwa Kristo. Petro alihitaji kuwa na hali ya kutokujiamini na kuwa na imani kamili katika Kristo. Wakati akiwa katika bahari ya Galilaya, alipotaka kuzama, alilalama na kusema: “Bwana uniokoe.” Hivyo hivyo na sasa kama angalilia na kusema niokoe katika hali hii ya kujitumainia, angalilindwa. Lakini Petro akaona kama ukatili kule kutoaminika na hivyo akazidi katika kujiamini kwake.
TVV 382.1
Yesu hakuweza kuwaokoa wanafunzi wake katika majaribu, lakini pia hakuwaacha bila faraja. Kabla ya kumkana walikuwa na uhakika wa msamaha. Baada ya kifo na ufufuo wake Kristo walielewa kuwa wamesamehewa na walikuwa wapenzi wa moyoni wa Kristo.
TVV 382.2
Yesu na wanafunzi wake walikuwa njiani kwenda Gethsemane, chini ya Mlima wa Mizeituni. Mwezi ulikuwa uking’aa na bustani ya mizeituni iliyositawi ilionekana kwake vizuri sana. Yesu akiwaelekeza wanafunzi wake kwa mizabibu hiyo, alisema “Mimi ndimi mzabibu wa kweli.” Mzabibu uliozungukwa kwa vikonyo unamwakilisha yeye Mwenyewe. Miti ya minazi, mierezi na mpingo husimama peke yake; haihitaji kitu cha kuitegemeza. Lakini mizabibu hujisokotesha katika fito na hivyo kupanda kuelekea mbinguni. Vivyo hivyo na Kristo katika hali yake ya kibinadamu aliegemea uwezo wa Mungu. “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe.” Yohana 5:30.
TVV 382.3
“Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.” Katika vilima vya Palestine Baba yetu wa mbinguni alikuwa ameupanda Mzabibu huu mzuri. Watu wengi walikuwa wakivutiwa na uzuri wa Mzabibu huu na kuusifia kuwa ni wa kutoka mbinguni. Lakini wakuu wa Israeli waliukanyaga mmea huu chini ya miguu yao miovu. Baada ya watu kudhani kwamba wameuua, Mkulima wa mbinguni aliuchukua na kupanda tena upande mwingine wa kitalu. Shina la Mzabibu lisingeonekana tena. Lilifichika lisionekane na watu wakorofi. Bali matawi yake yalining’inia ukutani ili kupitia kwayo chipukizi ya mizabibu mingine ipandikizwe kwa ule Mzabibu tena. Yesu alisema kuwa mwungano wa shina la mzabibu na matawi hufananishwa na uhusiano ambao wafuasi wake wanapaswa kudumisha kwake. Mche hupandikizwa katika Mzabibu ulio hai na hivyo kitembwe kwa kitembwe chelewa kwa chelewa hukua na kuzama katika shina la Mzabibu.
TVV 382.4
Ndivyo moyo hupata uhai kwa kuungana kwake na Kristo. Mwenye dhambi huunganisha udhaifu wake pamoja na nguvu za Kristo, uwazi wake kwa ujazo wa Kristo. Ndipo hupata nia ya Kristo. Ubinadamu wa Kristo umegusa wetu na ubinadamu wetu umegusa Uungu.
TVV 383.1
Mwungano huu lazima udumishwe. Kristo alisema, “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu” Huu siyo muungano wa mara kwa mara. Tawi huwa sehemu ya mzabibu ulio hai. Yesu alisema Uhai mliopokea kutoka kwangu unaweza kudumishwa tu kwa muungano wa kudumu. Pasipo Mimi ninyi hamwezi kushinda dhambi, au kupinga majaribu. Lazima sisi tushikamane na Yesu na kupokea hali ya tabia yake kamilifu kwa imani.
TVV 383.2
Mzizi hupeleka lishe yake kupitia tawi hadi kijiti cha mwisho. Hivo Yesu alisema, “akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyu huzaa sana maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Tunapoishi kwa imani katika Mwana wa Mungu, matunda ya Roho yataonekana maishani mwetu; hakuna hata moja litakalokosekana.
TVV 383.3
“Baba yangu ndiye Mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa.” Kuna uwezekano wa kuonekana kuungana na Yesu bila muungano halisi pamoja naye kwa imani. Kule kukiri dini huwawezesha watu kuwemo kanisani, lakini tabia itaonyesha ikiwa wanao mwuungano mkamilifu na Kristo. Ikiwa hawazai matunda yo yote basi wao ni matawi ya uongo. Kristo alisema “Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya kuyatupa motoni yakateketea.”
TVV 383.4
“Na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.” Kutoka katika wanafunzi kumi na wawili waliomfuata Yesu, mmoja kama tawi lililonyauka alikuwa karibu kuondolewa; na waliobaki walikuwa karibu kupitia chini ya kisu kisafishacho cha tanuru kali. Kupogolewa (kupunguza yasiyofaa) huumiza, lakini Baba ndiye anayepogoa. llapogoi kwa mkono wa kuumiza. Majani mengi yanayozidi na kutumia rutuba na hivyo kuhatarisha matunda lazima yaondolewe na kutupwa mbali.
TVV 383.5
Majani yote kufunika lazima yaondolewe ili yasibane tawi lizaalo; na kulizuia kupata miali ya Jua la Haki. Mkulima huondoa yale majani yanayozuia kukua kusudi matunda yawe mengi zaidi. “Hivyo hutukuzwa Baba yangu.” Yesu akasema, “kwa vile mzaavyo sana.” Mungu hutamani kujidhihirisha kupitia kwenu utakatifu, ukarimu na huruma ya tabia yake Mwenyewe. Hata hivyo Mwokozi hakuwalazimisha wanafunzi wake wafanye kazi ya kuzaa matunda. Ila huwaambia tu kukaa wao ndani yake. Kwa njia ya Neno Kristo hukaa ndani ya wafuasi wake. Maisha ya Kristo ndani yako huzaa matunda sawa sawa na ya Kristo. Kuishi ndani ya Kristo, kumfuata, ukisaidiwa na Kristo, ukipata rutuba kutoka kwake, utazaa matunda yanayofanana na Kristo.
TVV 383.6
Amri ya kwanza kabisa Yesu aliyotoa alipokuwa na wanafunzi wake peke yao katika chumba cha ghorofa ilikuwa “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi nanyi mpendane vivyo hivyo.” Amri hii ilikuwa mpya kwa wanafunzi maana walikuwa hawapendani kama Kristo alivyowapenda. Lakini kwa njia ya maisha yake na kifo chake, wangepata maana mpya ya upendo Amri ya kupendana ilikuwa na nuru mpya kufuatana na kafara yake ya kujitolea.
TVV 384.1
Watu wanaposhikana pamoja kwa upendo wala si kwa kulazimishwa, huonyesha kutenda kazi kwa mvuto ulio juu kuliko kila mvuto wa kibinadamu. Huonyesha kuwa sura ya Mungu inaumbika ndani ya ubinadamu. Upendo wa jinsi hii ukionekana kanisani, utaamsha ghadhabu ya Shetani. “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyepeleka. Injili itahubiriwa katika hali zote, katikati ya upinzani, hatari, hasara, na mateso.
TVV 384.2
Kama Mwokozi wa ulimwengu, Kristo alikabiliwa na uwezekano wa kushindwa dhahiri. Alionekana kuwa anatenda kidogo tu kuhusu kazi aliyotamani kukamilisha. Mivuto ya Shetani ilikuwa akimletea mapingamizi daima. Lakini hakukata tamaa. Kwa njia ya Isaya amesema, “Nimeiitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.” Isaya 49:4.
TVV 384.3
Yesu alisimama katika Neno hili na hakumpa Shetani nafasi. Wakati huzuni kuu ilipoikabili nafasi yake aliwaambia kwa wanafunzi wake; “kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu wala hana kitu kwangu.” “Yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.” Sasa . . . atatupwa nje. (Yohana 14:30; 16:11; 12:31.)
TVV 385.1
Knsto alijua kuwa, atakaposema “Imekwisha”. mbingu yote itashangilia. Sikio lake lilisikia kwa mbali nyimbo na shangwe kuu iliyokuwa ikifanywa huko mbinguni kushangilia ushindi. Alijua kuwa jina la Kristo litatangazwa katika sayari zote na kutukuzwa. Alijua kuwa ukweli ulioimarishwa na Roho Mtakatifu utashinda katika vita dhidi ya uovu. Alijua kuwa maisha ya wanafunzi. wake waaminifu yatafanana na maisha yake, mfulululizo wa ushindi ambao haujapata kuonekana hapa lakini utakaotambulikana, hivyo katika siku ile kuu. Kristo hakushindwa wala kukata tamaa, na wafuasi wake wanapaswa kudhihirisha imani stahimilifu. vivyo hivyo. Waishi kama alivyoishi yeye na kufanya kazi kama alivyofanya. Badala ya kusikitikia matatizo, wakabiliane nayo na kushinda kukata tamaa.
TVV 385.2
Kristo alikusudia kuwa utaratibu wa mbinguni na ushirikiano wa Uungu mbinguni vionekane katika kanisa lake hapa duniani. Ili kwa njia ya watu wake apokee utukufu mwingi. Kanisa lililojaliwa na haki ya Kristo, ndiyo ghala yake ambao utajiri wa neema yake na, upendo wake vitaonekana kwa dhahiri. Kristo huwaangalia watu wake katika usafi na utimilifu wao kama tunu ya unyenyekevu wake na nyongeza ya utukufu wake.
TVV 385.3
Kwa maneno mazito na ya tumaini Mwokozi alimalizia mafundisho yake. Alikuwa amekamilisha kazi aliyopewa kufanya. Alikuwa amelidhihirisha jina la Baba na kujikusanyia wale ambao wangeendeleza kazi yake miongoni mwa wanadamu.
TVV 385.4
Knsto sasa kama Kuhani Mkuu Aliyewekwa wakfu aliwaombea watu wake, “Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.” “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.. Wote wawe na umoja; “ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.”
TVV 385.5
Knsto aliliweka kanisa lake teule mikononi mwa Baba. Kwake kulibakia vita ya mwisho na Shetani, naye alitoka kwenda kukabiliana navyo.
TVV 385.6
13871
TVV
Tumaini la Vizazi Vyote
[{"para_id":"13871.97","title":"4 \u2014 Kuzaliwa Zizini","mp3":"\/mp3\/13871\/0014_swa_f_4_kuzaliwa_zizini_13871_97.mp3#duration=342&size=5577659"},{"para_id":"13871.145","title":"6 \u2014 Tumeiona Nyota Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0020_swa_f_6_tumeiona_nyota_yake_13871_145.mp3#duration=699&size=11277784"},{"para_id":"13871.184","title":"7 \u2014 Mtoto Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0025_swa_f_7_mtoto_yesu_13871_184.mp3#duration=598&size=6083499"},{"para_id":"13871.216","title":"8 \u2014 Kuhudhuria Katika Pasaka","mp3":"\/mp3\/13871\/0029_swa_f_8_kuhudhuria_katika_pasaka_13871_216.mp3#duration=664&size=6739433"},{"para_id":"13871.248","title":"9 \u2014 Matatizo ya Kristo Wakati wa Utoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0032_swa_f_9_matatizo_ya_kristo_wakati_wa_utoto_13871_248.mp3#duration=834&size=8439843"},{"para_id":"13871.282","title":"10 \u2014 Sauti Nyikani","mp3":"\/mp3\/13871\/0036_swa_f_10_sauti_nyikani_13871_282.mp3#duration=1057&size=10667758"},{"para_id":"13871.336","title":"11 \u2014 Ubatizo wa Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0042_swa_f_11_ubatizo_wa_yesu_13871_336.mp3#duration=478&size=4879322"},{"para_id":"13871.360","title":"12 \u2014 Majaribu","mp3":"\/mp3\/13871\/0045_swa_f_12_majaribu_13871_360.mp3#duration=977&size=9870882"},{"para_id":"13871.401","title":"13 \u2014 Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0050_swa_f_13_ushindi_13871_401.mp3#duration=623&size=6329203"},{"para_id":"13871.428","title":"14 \u2014 Tumemwona Masihi","mp3":"\/mp3\/13871\/0054_swa_f_14_tumemwona_masihi_13871_428.mp3#duration=1307&size=13172069"},{"para_id":"13871.485","title":"15 \u2014 Yesu Ahudhuria Harusi","mp3":"\/mp3\/13871\/0060_swa_f_15_yesu_ahudhuria_harusi_13871_485.mp3#duration=932&size=9423837"},{"para_id":"13871.527","title":"16 \u2014 Kristo Akabili Machafuko Hekaluni","mp3":"\/mp3\/13871\/0063_swa_f_16_kristo_akabili_machafuko_hekaluni_13871_527.mp3#duration=1374&size=13844801"},{"para_id":"13871.579","title":"17 \u2014 Nikodemo Amwendea Yesu Wakati wa Usiku","mp3":"\/mp3\/13871\/0068_swa_f_17_nikodemo_amwendea_yesu_wakati_wa_usiku_13871_579.mp3#duration=1110&size=11198316"},{"para_id":"13871.619","title":"18 \u2014 Yeye Hana Budi Kuzidi Bali Mimi Kupungua\u2019","mp3":"\/mp3\/13871\/0071_swa_f_18_yeye_hana_budi_kuzidi_bali_mimi_kupungua_13871_619.mp3#duration=392&size=4024084"},{"para_id":"13871.640","title":"19 \u2014 Yesu na Mwanawke Mwenye Waume Watano","mp3":"\/mp3\/13871\/0073_swa_f_19_yesu_na_mwanawke_mwenye_waume_watano_13871_640.mp3#duration=1095&size=11052730"},{"para_id":"13871.695","title":"20 \u2014 \u201cMsipoona Ishara na Maajabu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0078_swa_f_20_msipoona_ishara_na_maajabu_13871_695.mp3#duration=404&size=4140487"},{"para_id":"13871.715","title":"21 \u2014 Bethzatha na Sanhedrin","mp3":"\/mp3\/13871\/0079_swa_f_21_bethzatha_na_sanhedrin_13871_715.mp3#duration=1404&size=22570477"},{"para_id":"13871.777","title":"22 \u2014 Kifungo na Kifo cha Yohana","mp3":"\/mp3\/13871\/0086_swa_f_22_kifungo_na_kifo_cha_yohana_13871_777.mp3#duration=1163&size=11730972"},{"para_id":"13871.830","title":"23 \u2014 Jinsi Danieli Alivyomtambua Yesu kuwa ni Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0092_swa_f_23_jinsi_danieli_alivyomtambua_yesu_kuwa_ni_kristo_13871_830.mp3#duration=543&size=5530218"},{"para_id":"13871.851","title":"24 \u2014 \u201cJe, Huyu Siye Mwana wa Seremala?\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0094_swa_f_24_je_huyu_siye_mwana_wa_seremala_13871_851.mp3#duration=718&size=7276333"},{"para_id":"13871.885","title":"25 \u2014 Mwito Kando ya Bahari","mp3":"\/mp3\/13871\/0096_swa_f_25_mwito_kando_ya_bahari_13871_885.mp3#duration=618&size=6283618"},{"para_id":"13871.911","title":"26 \u2014 Siku za Shughuli na Raha katika Kapernaumu","mp3":"\/mp3\/13871\/0100_swa_f_26_siku_za_shughuli_na_raha_katika_kapernaumu_13871_911.mp3#duration=1004&size=10145925"},{"para_id":"13871.955","title":"27 \u2014 Mwenye Ukoma wa Kwanza Kuponywa na Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0103_swa_f_27_mwenye_ukoma_wa_kwanza_kuponywa_na_kristo_13871_955.mp3#duration=999&size=10093329"},{"para_id":"13871.1004","title":"28 \u2014 Mathayo: Kutoka Kutoza Ushuru Mpaka Mwanafunzi","mp3":"\/mp3\/13871\/0107_swa_f_28_mathayo_kutoka_kutoza_ushuru_mpaka_mwanafunzi_13871_1004.mp3#duration=830&size=8399583"},{"para_id":"13871.1042","title":"29 \u2014 Yesu Aiokoa Sabato","mp3":"\/mp3\/13871\/0112_swa_f_29_yesu_aiokoa_sabato_13871_1042.mp3#duration=933&size=9434863"},{"para_id":"13871.1081","title":"30 \u2014 Awekea Mikono Mitume Kumi na Wawili","mp3":"\/mp3\/13871\/0117_swa_f_30_awekea_mikono_mitume_kumi_na_wawili_13871_1081.mp3#duration=405&size=4147140"},{"para_id":"13871.1100","title":"31 \u2014 Mahubiri Mlimani","mp3":"\/mp3\/13871\/0119_swa_f_31_mahubiri_mlimani_13871_1100.mp3#duration=1556&size=25001595"},{"para_id":"13871.1172","title":"32 \u2014 Afisa wa Jeshi Aomba Msaada Kwa Ajili Mtumishi Wake","mp3":"\/mp3\/13871\/0125_swa_f_32_afisa_wa_jeshi_aomba_msaada_kwa_ajili_mtumishi_wake_13871_1172.mp3#duration=533&size=8636236"},{"para_id":"13871.1199","title":"33 \u2014 Jinsi Yesu Alivyojihusisha na Matatizo ya Jamaa","mp3":"\/mp3\/13871\/0127_swa_f_33_jinsi_yesu_alivyojihusisha_na_matatizo_ya_jamaa_13871_1199.mp3#duration=744&size=11999844"},{"para_id":"13871.1229","title":"34 \u2014 Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi","mp3":"\/mp3\/13871\/0130_swa_f_34_nira_yake_ni_laini_na_mzigo_wake_ni_mwepesi_13871_1229.mp3#duration=511&size=8279056"},{"para_id":"13871.1255","title":"35 \u2014 Kutuliza Dhoruba","mp3":"\/mp3\/13871\/0133_swa_f_35_kutuliza_dhoruba_13871_1255.mp3#duration=953&size=15344257"},{"para_id":"13871.1299","title":"36 \u2014 Mguso wa Imani","mp3":"\/mp3\/13871\/0136_swa_f_36_mguso_wa_imani_13871_1299.mp3#duration=457&size=7409111"},{"para_id":"13871.1320","title":"37 \u2014 Wainjilisti wa Kwanza","mp3":"\/mp3\/13871\/0138_swa_f_37_wainjilisti_wa_kwanza_13871_1320.mp3#duration=804&size=12970024"},{"para_id":"13871.1358","title":"38 \u2014 Kristo na Wanafunzi Wapumzika","mp3":"\/mp3\/13871\/0141_swa_f_38_kristo_na_wanafunzi_wapumzika_13871_1358.mp3#duration=504&size=8168554"},{"para_id":"13871.1385","title":"39 \u2014 \u201cWapeni Ninyi Chakula\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0144_swa_f_39_wapeni_ninyi_chakula_13871_1385.mp3#duration=299&size=4886983"},{"para_id":"13871.1413","title":"40 \u2014 Usiku Ziwani","mp3":"\/mp3\/13871\/0147_swa_f_40_usiku_ziwani_13871_1413.mp3#duration=639&size=10325621"},{"para_id":"13871.1445","title":"41 \u2014 Hatari Katika Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0150_swa_f_41_hatari_katika_galilaya_13871_1445.mp3#duration=1322&size=21255291"},{"para_id":"13871.1509","title":"42 \u2014 Kristo Atabiri Juu ya Maanguko","mp3":"\/mp3\/13871\/0157_swa_f_42_kristo_atabiri_juu_ya_maanguko_13871_1509.mp3#duration=310&size=3197643"},{"para_id":"13871.1527","title":"43 \u2014 Kristo Avunja Ubaguzi wa Mataifa","mp3":"\/mp3\/13871\/0159_swa_f_43_kristo_avunja_ubaguzi_wa_mataifa_13871_1527.mp3#duration=551&size=5609425"},{"para_id":"13871.1551","title":"44 \u2014 Ishara ya Kweli","mp3":"\/mp3\/13871\/0161_swa_f_44_ishara_ya_kweli_13871_1551.mp3#duration=684&size=6941240"},{"para_id":"13871.1582","title":"45 \u2014 Kuonyeshwa Mbele Fumbo la Msalaba","mp3":"\/mp3\/13871\/0165_swa_f_45_kuonyeshwa_mbele_fumbo_la_msalaba_13871_1582.mp3#duration=1145&size=11549078"},{"para_id":"13871.1631","title":"46 \u2014 Yesu Ageuka Sura","mp3":"\/mp3\/13871\/0169_swa_f_46_yesu_ageuka_sura_13871_1631.mp3#duration=510&size=5201013"},{"para_id":"13871.1653","title":"47 \u2014 Kupingana na Roho za Mashetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0171_swa_f_47_kupingana_na_roho_za_mashetani_13871_1653.mp3#duration=530&size=5405611"},{"para_id":"13871.1675","title":"48 \u2014 Nani Aliye Mkubwa Zaidi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0173_swa_f_48_nani_aliye_mkubwa_zaidi_13871_1675.mp3#duration=1120&size=11299793"},{"para_id":"13871.1724","title":"49 \u2014 \u201cMtu Akiwa na Kiu, na Aje\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0177_swa_f_49_mtu_akiwa_na_kiu_na_aje_13871_1724.mp3#duration=703&size=7128511"},{"para_id":"13871.1758","title":"50 \u2014 Katikati ya Mitego","mp3":"\/mp3\/13871\/0180_swa_f_50_katikati_ya_mitego_13871_1758.mp3#duration=856&size=8662407"},{"para_id":"13871.1798","title":"51 \u2014 Nuru ya Uzima","mp3":"\/mp3\/13871\/0184_swa_f_51_nuru_ya_uzima_13871_1798.mp3#duration=1310&size=13204222"},{"para_id":"13871.1859","title":"52 \u2014 Mchungaji, Mungu","mp3":"\/mp3\/13871\/0190_swa_f_52_mchungaji_mungu_13871_1859.mp3#duration=580&size=5898525"},{"para_id":"13871.1886","title":"53 \u2014 Safari ya Mwisho Kutoka Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0194_swa_f_53_safari_ya_mwisho_kutoka_galilaya_13871_1886.mp3#duration=863&size=8730237"},{"para_id":"13871.1925","title":"54 \u2014 Msamaria Mwema","mp3":"\/mp3\/13871\/0198_swa_f_54_msamaria_mwema_13871_1925.mp3#duration=616&size=6260151"},{"para_id":"13871.1952","title":"55 \u2014 Si Kujionyesha kwa Nje","mp3":"\/mp3\/13871\/0200_swa_f_55_si_kujionyesha_kwa_nje_13871_1952.mp3#duration=433&size=4434757"},{"para_id":"13871.1971","title":"56 \u2014 Upendo wa Yesu kwa Watoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0201_swa_f_56_upendo_wa_yesu_kwa_watoto_13871_1971.mp3#duration=543&size=5526138"},{"para_id":"13871.1996","title":"57 \u2014 Kijana Tajiri Mtawala Amepungukiwa na jambo Moja","mp3":"\/mp3\/13871\/0203_swa_f_57_kijana_tajiri_mtawala_amepungukiwa_na_jambo_moja_13871_1996.mp3#duration=478&size=4879601"},{"para_id":"13871.2019","title":"58 \u2014 Kufufuliwa kwa Lazaro","mp3":"\/mp3\/13871\/0205_swa_f_58_kufufuliwa_kwa_lazaro_13871_2019.mp3#duration=1099&size=11092144"},{"para_id":"13871.2066","title":"59 \u2014 Makuhani na Wakuu Wanaendelea na Njama Yao","mp3":"\/mp3\/13871\/0206_swa_f_59_makuhani_na_wakuu_wanaendelea_na_njama_yao_13871_2066.mp3#duration=454&size=4641463"},{"para_id":"13871.2088","title":"60 \u2014 Cheo Kikuu Ni Kipi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0208_swa_f_60_cheo_kikuu_ni_kipi_13871_2088.mp3#duration=406&size=4158184"},{"para_id":"13871.2112","title":"61 \u2014 Mtu Mfupi Aliyekuwa Mashuhuri","mp3":"\/mp3\/13871\/0210_swa_f_61_mtu_mfupi_aliyekuwa_mashuhuri_13871_2112.mp3#duration=401&size=4111640"},{"para_id":"13871.2133","title":"62 \u2014 Mariamu Ampaka Yesu Mafuta","mp3":"\/mp3\/13871\/0211_swa_f_62_mariamu_ampaka_yesu_mafuta_13871_2133.mp3#duration=1307&size=13170907"},{"para_id":"13871.2190","title":"63 \u2014 Yesu Atangazwa Kuwa Mfalme wa Israeli","mp3":"\/mp3\/13871\/0218_swa_f_63_yesu_atangazwa_kuwa_mfalme_wa_israeli_13871_2190.mp3#duration=707&size=7169996"},{"para_id":"13871.2232","title":"64 \u2014 Watu wa Kuangamia","mp3":"\/mp3\/13871\/0222_swa_f_64_watu_wa_kuangamia_13871_2232.mp3#duration=693&size=7031722"},{"para_id":"13871.2263","title":"65 \u2014 Hekalu Latakaswa Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0224_swa_f_65_hekalu_latakaswa_tena_13871_2263.mp3#duration=1329&size=13390450"},{"para_id":"13871.2316","title":"66 \u2014 Kristo Akabiliana na Adui Zake","mp3":"\/mp3\/13871\/0228_swa_f_66_kristo_akabiliana_na_adui_zake_13871_2316.mp3#duration=740&size=7505171"},{"para_id":"13871.2352","title":"67 \u2014 Yesu Azuru Hekalu Mara ya Mwisho","mp3":"\/mp3\/13871\/0231_swa_f_67_yesu_azuru_hekalu_mara_ya_mwisho_13871_2352.mp3#duration=1219&size=12295749"},{"para_id":"13871.2400","title":"68 \u2014 Wayunani Walipotaka \u201cKumwona Yesu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0233_swa_f_68_wayunani_walipotaka_kumwona_yesu_13871_2400.mp3#duration=666&size=6756313"},{"para_id":"13871.2430","title":"69 \u2014 Dalili za Kuja Kwa Kristo Mara ya Pili","mp3":"\/mp3\/13871\/0235_swa_f_69_dalili_za_kuja_kwa_kristo_mara_ya_pili_13871_2430.mp3#duration=1155&size=11655117"},{"para_id":"13871.2473","title":"70 \u2014 Kristo Ashirikiana na Wenye Dhiki na Masikini","mp3":"\/mp3\/13871\/0239_swa_f_70_kristo_ashirikiana_na_wenye_dhiki_na_masikini_13871_2473.mp3#duration=566&size=5758478"},{"para_id":"13871.2498","title":"71 \u2014 Mtumishi wa Watumishi","mp3":"\/mp3\/13871\/0241_swa_f_71_mtumishi_wa_watumishi_13871_2498.mp3#duration=943&size=9526890"},{"para_id":"13871.2539","title":"72 \u2014 Meza ya Bwana Yaanzishwa","mp3":"\/mp3\/13871\/0243_swa_f_72_meza_ya_bwana_yaanzishwa_13871_2539.mp3#duration=958&size=9677405"},{"para_id":"13871.2576","title":"73 \u2014 \u201cMsifadhaike Mioyoni Mwenu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0246_swa_f_73_msifadhaike_mioyoni_mwenu_13871_2576.mp3#duration=1908&size=19179012"},{"para_id":"13871.2641","title":"74 \u2014 Pambano la Kutisha Katika Gethsemane","mp3":"\/mp3\/13871\/0251_swa_f_74_pambano_la_kutisha_katika_gethsemane_13871_2641.mp3#duration=1080&size=10900601"},{"para_id":"13871.2688","title":"75 \u2014 Kesi Batili Dhidi ya Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0256_swa_f_75_kesi_batili_dhidi_ya_yesu_13871_2688.mp3#duration=1590&size=25543110"},{"para_id":"13871.2752","title":"76 \u2014 Jinsi Yuda Alivyopoteza Roho Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0262_swa_f_76_jinsi_yuda_alivyopoteza_roho_yake_13871_2752.mp3#duration=692&size=7020406"},{"para_id":"13871.2784","title":"77 \u2014 Kristo Ashtakiwa Mbele Ya Gavana Wa Kirumi","mp3":"\/mp3\/13871\/0266_swa_f_77_kristo_ashtakiwa_mbele_ya_gavana_wa_kirumi_13871_2784.mp3#duration=1936&size=19458815"},{"para_id":"13871.2868","title":"78 \u2014 Yesu Afa Juu Ya Kalwari","mp3":"\/mp3\/13871\/0274_swa_f_78_yesu_afa_juu_ya_kalwari_13871_2868.mp3#duration=1671&size=16811964"},{"para_id":"13871.2932","title":"79 \u2014 Jinsi Kifo Cha Kristo Kilivyomshinda Shetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0281_swa_f_79_jinsi_kifo_cha_kristo_kilivyomshinda_shetani_13871_2932.mp3#duration=884&size=8938225"},{"para_id":"13871.2968","title":"80 \u2014 Yesu Apumzika Katika Kaburi La Yusufu","mp3":"\/mp3\/13871\/0285_swa_f_80_yesu_apumzika_katika_kaburi_la_yusufu_13871_2968.mp3#duration=708&size=7178978"},{"para_id":"13871.2994","title":"81 \u2014 \u201cBwana Amefufuka\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0288_swa_f_81_bwana_amefufuka_13871_2994.mp3#duration=562&size=5718538"},{"para_id":"13871.3022","title":"82 \u2014 \u201cMama Unalilia Nini?","mp3":"\/mp3\/13871\/0292_swa_f_82_mama_unalilia_nini_13871_3022.mp3#duration=578&size=5878775"},{"para_id":"13871.3051","title":"83 \u2014 Kutembea Kwenda Emau","mp3":"\/mp3\/13871\/0293_swa_f_83_kutembea_kwenda_emau_13871_3051.mp3#duration=498&size=5083897"},{"para_id":"13871.3073","title":"84 \u2014 Kristo Aliyefufuka Atokea","mp3":"\/mp3\/13871\/0296_swa_f_84_kristo_aliyefufuka_atokea_13871_3073.mp3#duration=595&size=6053282"},{"para_id":"13871.3100","title":"85 \u2014 Kando Ya Bahari Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0299_swa_f_85_kando_ya_bahari_tena_13871_3100.mp3#duration=789&size=12730367"},{"para_id":"13871.3133","title":"86 \u2014 \u201cEnendeni . . . Mkawafanye Mataifa Yote\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0302_swa_f_86_enendeni_mkawafanye_mataifa_yote_13871_3133.mp3#duration=936&size=15074513"},{"para_id":"13871.3172","title":"87 \u2014 Kristo Aingia Mbinguni Kwa Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0306_swa_f_87_kristo_aingia_mbinguni_kwa_ushindi_13871_3172.mp3#duration=691&size=11154751"}]