Tumaini la Vizazi Vyote

236/307

Ishara katika Mbingu

Mwokozi anatoa dalili za kurudi kwake, na kutaja wakati ambapo dalili za kwanza kati ya hizo zilakapoanza kutokea; “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu walakapoombeleza; nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu”. TVV 356.1

Mwisho wa mateso makuu yaliyoendeshwa na upapa, Kristo alitamka, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake. Kukifuata nyota kuanguka mbinguni. Na anasema; “Nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.” Mathayo 24:33. Kristo anasema kwa wale watakaoziona dalili hizi: “Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.” Dalili hizi zilikwisha kutokea. Sasa tunajua kuwa kurudi kwa Bwana kuko, karibu mlangoni. TVV 356.2

Kristo anakuja na utukufu mwingi. Majeshi ya Malaika wenye utukufu watafuatana naye. Atakuja kuwafufua wafu na kuwabadilisha watakatifu walio hai; ili kuwatukuza watu wake waliompenda na kuzishika amri zake na kisha kuwapeleka kwake. Tunapowaangalia wafu wetu na tukumbuke asubuhi ile ambayo’”wafu waafufuliwa, wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika.” 1 Wakorintho 15.52. Mfalme atayafuta machozi yote kutoka katika macho yetu, na kutusimamisha “mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu” (Yuda 1:24). “Basi: mambo hayo yaanzapo kutokea changamkeni mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.” Lakini Kristo alisema wazi kuwa yeye mwenyewe hawezi kusema siku au saa ya kurudi kwake. Siku: hasa ya kurudi kwake Yesu ni siri ya Mungu. TVV 356.3