Mashindano ya Kushindania Ukuu
Mwokozi aliwaambia, “Mtu yeyote atakaye kuwa wa kwanza kwenu, na awe mdogo kuliko wote, na kuwa miumishi wa wote.” Hawakufahamu aina ya ufalme wa Kristo, bila shaka hili ndilo lililokuwa asili ya mabishano yao. Lakini sababu hasa ilikuwa kubwa zaidi kuliko hilo. Hata walipokwisha kufahamu kabisa, swali lolote la mambo yaliyotangulia lingeweza kuamsha matatizo. Hivyo msukosuko ungeweza kuletwa kanisani, baada ya Kristo kuondoka. Kushindania ukuu, ulikuwa kazi ya juu juu ya nia ile ya ushindani mkuu ulioanzia mbinguni, uliosababisha Yesu kuja na kufa. Mbele yake ilitokea njozi ya Shetani aliyesema, “Nitafanana naye aliye juu.” Isaya 14:14. Tamaa ya ukuu ilileta mashindano katika baraza la mbinguni. Lusifa alitamani kupata uwezo wa Mungu, sio tabia ya Mungu. Alitafuta kupata ukuu, na kila mtu au kila kiumbe chenye nia hiyo, hutenda mambo kama hayo. Utawala wa Shetani ni wa mabavu. Kila mtu humhesabu mwingine kuwa ni ngazi yake ya kupandia kwenda kwenye ukuu.
TVV 247.6
Wakati Lusifa alipotafuta kulingana na Mungu, “kristo alijifanya kuwa hana utukufu, akajitwalia namna ya mtumwa, akawa mfano wa mwanadamu, na alipokuwa na umbo la mwanadamu akajinyenyekeza, akawa mtii mpaka mauti, nayo mauti ya msalaba.” Wafilipi 2:7, 8. Sasa msalaba ulikuwa mbele yake, na wanafunzi wake walikuwa wakijitafutia ukuu, wala hawakushughulikia na hali ya unyenyekevu aliokuwa nayo Bwana wao, wala hawakuelewa na maneno yake kuhusu unyenyekevu kwa ajili yao.
TVV 248.1
Yesu alijaribu kusahihisha maovu haya. Aliwaonyesha ni kanuni gani inayotakiwa katika ufalme wa mbinguni, na ukuu wa kweli ni upi. Wale waliojawa na kiburi na kujiona walikuwa wakijifikiria na zawadi watakayopata. Watu kama hao hawakufaa katika ufalme wa mbinguni, maana walionekana kuwa katika jamii ya Shetani. Kabla ya kupata heshima, kwanza kunyenyekea. Kupata cheo mbele ya wanadamu, mbingu huchagua watendakazi walio katika sehemu ya chini machoni pa Mungu. Mwanafunzi wafananaye na mtoto, ndiye afaaye zaidi katika kazi ya Mungu. Anayehitaji msaada wa mbinguni, atauomba kutoka katika kuongea na Kristo, ataondoka kwenda katika kazi yake, akiwa na msaada alioomba naye hufaulu pale watu wenye elimu zaidi wanaposhindwa.
TVV 248.2
Lakini watu wanaojitukuza wenyewe, wakijiona kuwa wanatosha kufaulu kazini na kuendesha mpango wa Mungu, Bwana huwaweka kando tu, wala hana haja nao. Kazi ya Mungu haisimami, bali huendelea kwa nguvu zaidi.
TVV 248.3
Haikutosha kuwafundisha wanafunzi wa Kristo namna ufalme wa Mungu ulivyo. Jambo kubwa walilohitaji ni kuongoka, na kubadilika mioyo yao. Yesu akimwita mtoto, alimweka kati yao, akamkumbatia mikononi mwake, akasema, “Msipoongoka, mkawa kama’ mtoto mdogo, hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.” Hali isiyokuwa ya kutaka makuu, kujisahau nafsi, na kuwa na upendo kama mtoto mdogo, ndiyo hali yenye thamani machoni pa mbingu, nayo ndiyo inayoonyesha ukuu wa kweli. Katika miguu ya Yesu, fahari ya ulimwengu na ukuu wake husahauliwa. Matajiri na maskini, wasomi na wasio wasomi, hukutana pamoja kama watu walionunuliwa kwa damu ya thamani bila ubaguzi wa aina yoyote.
TVV 248.4
Mungu huweka muhuri wake kwa watu, sio kwa ajili ya vyeo walivyo navyo, ila kwa ajili ya ungano waliloungana na Kristo. “Nawe umenipa ngao ya wokovu . . . wako.” Kama mafao ya tabia ya mwanadamu, “Umenikuza.” Zaburi 18:35.
TVV 249.1
Maneno ya Mwokozi yaliwafanya wanafunzi wake wasijitumainie. Yohana aliamshwa aulize, kama matendo yake ni ya sawa, au namna gani. Alisema: “Bwana, tulimwona mtu mmoja akifukuza pepo kwa jina lako . . . sisi tulimkataza kwa sababu hafuatani na sisi.” Yakobo na Yohana walidhani kuwa kumkataza mtu huyo walikuwa wakimtetea Bwana wao; kumbe sivyo.
TVV 249.2
Walianza kufahamu kuwa kufanya hivyo walikuwa wakiona wivu kwa ajili yao wenyewe. Walikubali kosa lao, na kukubaliana na makemeo ya Yesu. Bwana aliwaambia: “Msimkataze, maana hakuna awezaye kufanya miujiza kwa jina langu, kisha akawa kinyume changu.” Watu wengi walivutiwa na tabia pamoja na kazi ya Kristo, ambao walimwamini. Wanafunzi inawapasa kuwa waangalifu sana ili wasiwakatishe tamaa hawa watu. Lazima waonyeshe fadhili kama zile walizoona Bwana wao.
TVV 249.3
Kristo ni Mwalimu Mkuu; nasi twapaswa kukaa miguuni mwake na kujifunza kwake. Kila mtu aliyevutwa na Mungu ni mfereji wa kupitishia upendo wa Yesu na kuwafikia wengine. Ingelupasa kuwa waangalifu kadiri gani ili kusudi tusije tukawakatisha wachukuzi nuru wa Mungu na kuvuruga nuru ambayo wangeangaza ulimwenguni!
TVV 249.4
Kitendo kama cha Yohana cha kumkataza afanyaye miujiza kwa jina la Yesu, kingeweza kupoteza mtu. Yesu alisema kuhusu jambo hili. “Ni heri kama angefungiwa jiwe, shingoni mwake na kutupwa kilindini mwa bahari.”
TVV 249.5
Mbona kusema maneno haya magumu? Kwa sababu “Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilicopotea.” Luka 19:10. Je, wanafunzi wake wataonyesha roho ya ubinafsi kwa wenzao, kuliko Bwana wa mbinguni alivyoonyesha roho ya fadhili kwa watu? Dhambi ya kumkosesha mtu ni kubwa kadiri gani? Kwa mtu huyu kilio na masumbuko ya Mwokozi yalikuwa bure. Ni dhambi kubwa mno!
TVV 249.6
Ole ni wa ulimwengu kwa ajili ya mambo ya kukosesha. Mambo ya kukosesha hayana budi kuja. Ulimwengu utawapinga wafuasi wa Kristo kwa hakika. Lakini ole wa mkristo afanyaye mambo haya. Watu wengi hudanganywa na kupotoshwa na wale wanaojidai kuwa ni wafuasi wa Kristo, hali wakipotosha tabia yake.
TVV 250.1
13871
TVV
Tumaini la Vizazi Vyote
[{"para_id":"13871.97","title":"4 \u2014 Kuzaliwa Zizini","mp3":"\/mp3\/13871\/0014_swa_f_4_kuzaliwa_zizini_13871_97.mp3#duration=342&size=5577659"},{"para_id":"13871.145","title":"6 \u2014 Tumeiona Nyota Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0020_swa_f_6_tumeiona_nyota_yake_13871_145.mp3#duration=699&size=11277784"},{"para_id":"13871.184","title":"7 \u2014 Mtoto Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0025_swa_f_7_mtoto_yesu_13871_184.mp3#duration=598&size=6083499"},{"para_id":"13871.216","title":"8 \u2014 Kuhudhuria Katika Pasaka","mp3":"\/mp3\/13871\/0029_swa_f_8_kuhudhuria_katika_pasaka_13871_216.mp3#duration=664&size=6739433"},{"para_id":"13871.248","title":"9 \u2014 Matatizo ya Kristo Wakati wa Utoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0032_swa_f_9_matatizo_ya_kristo_wakati_wa_utoto_13871_248.mp3#duration=834&size=8439843"},{"para_id":"13871.282","title":"10 \u2014 Sauti Nyikani","mp3":"\/mp3\/13871\/0036_swa_f_10_sauti_nyikani_13871_282.mp3#duration=1057&size=10667758"},{"para_id":"13871.336","title":"11 \u2014 Ubatizo wa Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0042_swa_f_11_ubatizo_wa_yesu_13871_336.mp3#duration=478&size=4879322"},{"para_id":"13871.360","title":"12 \u2014 Majaribu","mp3":"\/mp3\/13871\/0045_swa_f_12_majaribu_13871_360.mp3#duration=977&size=9870882"},{"para_id":"13871.401","title":"13 \u2014 Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0050_swa_f_13_ushindi_13871_401.mp3#duration=623&size=6329203"},{"para_id":"13871.428","title":"14 \u2014 Tumemwona Masihi","mp3":"\/mp3\/13871\/0054_swa_f_14_tumemwona_masihi_13871_428.mp3#duration=1307&size=13172069"},{"para_id":"13871.485","title":"15 \u2014 Yesu Ahudhuria Harusi","mp3":"\/mp3\/13871\/0060_swa_f_15_yesu_ahudhuria_harusi_13871_485.mp3#duration=932&size=9423837"},{"para_id":"13871.527","title":"16 \u2014 Kristo Akabili Machafuko Hekaluni","mp3":"\/mp3\/13871\/0063_swa_f_16_kristo_akabili_machafuko_hekaluni_13871_527.mp3#duration=1374&size=13844801"},{"para_id":"13871.579","title":"17 \u2014 Nikodemo Amwendea Yesu Wakati wa Usiku","mp3":"\/mp3\/13871\/0068_swa_f_17_nikodemo_amwendea_yesu_wakati_wa_usiku_13871_579.mp3#duration=1110&size=11198316"},{"para_id":"13871.619","title":"18 \u2014 Yeye Hana Budi Kuzidi Bali Mimi Kupungua\u2019","mp3":"\/mp3\/13871\/0071_swa_f_18_yeye_hana_budi_kuzidi_bali_mimi_kupungua_13871_619.mp3#duration=392&size=4024084"},{"para_id":"13871.640","title":"19 \u2014 Yesu na Mwanawke Mwenye Waume Watano","mp3":"\/mp3\/13871\/0073_swa_f_19_yesu_na_mwanawke_mwenye_waume_watano_13871_640.mp3#duration=1095&size=11052730"},{"para_id":"13871.695","title":"20 \u2014 \u201cMsipoona Ishara na Maajabu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0078_swa_f_20_msipoona_ishara_na_maajabu_13871_695.mp3#duration=404&size=4140487"},{"para_id":"13871.715","title":"21 \u2014 Bethzatha na Sanhedrin","mp3":"\/mp3\/13871\/0079_swa_f_21_bethzatha_na_sanhedrin_13871_715.mp3#duration=1404&size=22570477"},{"para_id":"13871.777","title":"22 \u2014 Kifungo na Kifo cha Yohana","mp3":"\/mp3\/13871\/0086_swa_f_22_kifungo_na_kifo_cha_yohana_13871_777.mp3#duration=1163&size=11730972"},{"para_id":"13871.830","title":"23 \u2014 Jinsi Danieli Alivyomtambua Yesu kuwa ni Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0092_swa_f_23_jinsi_danieli_alivyomtambua_yesu_kuwa_ni_kristo_13871_830.mp3#duration=543&size=5530218"},{"para_id":"13871.851","title":"24 \u2014 \u201cJe, Huyu Siye Mwana wa Seremala?\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0094_swa_f_24_je_huyu_siye_mwana_wa_seremala_13871_851.mp3#duration=718&size=7276333"},{"para_id":"13871.885","title":"25 \u2014 Mwito Kando ya Bahari","mp3":"\/mp3\/13871\/0096_swa_f_25_mwito_kando_ya_bahari_13871_885.mp3#duration=618&size=6283618"},{"para_id":"13871.911","title":"26 \u2014 Siku za Shughuli na Raha katika Kapernaumu","mp3":"\/mp3\/13871\/0100_swa_f_26_siku_za_shughuli_na_raha_katika_kapernaumu_13871_911.mp3#duration=1004&size=10145925"},{"para_id":"13871.955","title":"27 \u2014 Mwenye Ukoma wa Kwanza Kuponywa na Kristo","mp3":"\/mp3\/13871\/0103_swa_f_27_mwenye_ukoma_wa_kwanza_kuponywa_na_kristo_13871_955.mp3#duration=999&size=10093329"},{"para_id":"13871.1004","title":"28 \u2014 Mathayo: Kutoka Kutoza Ushuru Mpaka Mwanafunzi","mp3":"\/mp3\/13871\/0107_swa_f_28_mathayo_kutoka_kutoza_ushuru_mpaka_mwanafunzi_13871_1004.mp3#duration=830&size=8399583"},{"para_id":"13871.1042","title":"29 \u2014 Yesu Aiokoa Sabato","mp3":"\/mp3\/13871\/0112_swa_f_29_yesu_aiokoa_sabato_13871_1042.mp3#duration=933&size=9434863"},{"para_id":"13871.1081","title":"30 \u2014 Awekea Mikono Mitume Kumi na Wawili","mp3":"\/mp3\/13871\/0117_swa_f_30_awekea_mikono_mitume_kumi_na_wawili_13871_1081.mp3#duration=405&size=4147140"},{"para_id":"13871.1100","title":"31 \u2014 Mahubiri Mlimani","mp3":"\/mp3\/13871\/0119_swa_f_31_mahubiri_mlimani_13871_1100.mp3#duration=1556&size=25001595"},{"para_id":"13871.1172","title":"32 \u2014 Afisa wa Jeshi Aomba Msaada Kwa Ajili Mtumishi Wake","mp3":"\/mp3\/13871\/0125_swa_f_32_afisa_wa_jeshi_aomba_msaada_kwa_ajili_mtumishi_wake_13871_1172.mp3#duration=533&size=8636236"},{"para_id":"13871.1199","title":"33 \u2014 Jinsi Yesu Alivyojihusisha na Matatizo ya Jamaa","mp3":"\/mp3\/13871\/0127_swa_f_33_jinsi_yesu_alivyojihusisha_na_matatizo_ya_jamaa_13871_1199.mp3#duration=744&size=11999844"},{"para_id":"13871.1229","title":"34 \u2014 Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi","mp3":"\/mp3\/13871\/0130_swa_f_34_nira_yake_ni_laini_na_mzigo_wake_ni_mwepesi_13871_1229.mp3#duration=511&size=8279056"},{"para_id":"13871.1255","title":"35 \u2014 Kutuliza Dhoruba","mp3":"\/mp3\/13871\/0133_swa_f_35_kutuliza_dhoruba_13871_1255.mp3#duration=953&size=15344257"},{"para_id":"13871.1299","title":"36 \u2014 Mguso wa Imani","mp3":"\/mp3\/13871\/0136_swa_f_36_mguso_wa_imani_13871_1299.mp3#duration=457&size=7409111"},{"para_id":"13871.1320","title":"37 \u2014 Wainjilisti wa Kwanza","mp3":"\/mp3\/13871\/0138_swa_f_37_wainjilisti_wa_kwanza_13871_1320.mp3#duration=804&size=12970024"},{"para_id":"13871.1358","title":"38 \u2014 Kristo na Wanafunzi Wapumzika","mp3":"\/mp3\/13871\/0141_swa_f_38_kristo_na_wanafunzi_wapumzika_13871_1358.mp3#duration=504&size=8168554"},{"para_id":"13871.1385","title":"39 \u2014 \u201cWapeni Ninyi Chakula\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0144_swa_f_39_wapeni_ninyi_chakula_13871_1385.mp3#duration=299&size=4886983"},{"para_id":"13871.1413","title":"40 \u2014 Usiku Ziwani","mp3":"\/mp3\/13871\/0147_swa_f_40_usiku_ziwani_13871_1413.mp3#duration=639&size=10325621"},{"para_id":"13871.1445","title":"41 \u2014 Hatari Katika Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0150_swa_f_41_hatari_katika_galilaya_13871_1445.mp3#duration=1322&size=21255291"},{"para_id":"13871.1509","title":"42 \u2014 Kristo Atabiri Juu ya Maanguko","mp3":"\/mp3\/13871\/0157_swa_f_42_kristo_atabiri_juu_ya_maanguko_13871_1509.mp3#duration=310&size=3197643"},{"para_id":"13871.1527","title":"43 \u2014 Kristo Avunja Ubaguzi wa Mataifa","mp3":"\/mp3\/13871\/0159_swa_f_43_kristo_avunja_ubaguzi_wa_mataifa_13871_1527.mp3#duration=551&size=5609425"},{"para_id":"13871.1551","title":"44 \u2014 Ishara ya Kweli","mp3":"\/mp3\/13871\/0161_swa_f_44_ishara_ya_kweli_13871_1551.mp3#duration=684&size=6941240"},{"para_id":"13871.1582","title":"45 \u2014 Kuonyeshwa Mbele Fumbo la Msalaba","mp3":"\/mp3\/13871\/0165_swa_f_45_kuonyeshwa_mbele_fumbo_la_msalaba_13871_1582.mp3#duration=1145&size=11549078"},{"para_id":"13871.1631","title":"46 \u2014 Yesu Ageuka Sura","mp3":"\/mp3\/13871\/0169_swa_f_46_yesu_ageuka_sura_13871_1631.mp3#duration=510&size=5201013"},{"para_id":"13871.1653","title":"47 \u2014 Kupingana na Roho za Mashetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0171_swa_f_47_kupingana_na_roho_za_mashetani_13871_1653.mp3#duration=530&size=5405611"},{"para_id":"13871.1675","title":"48 \u2014 Nani Aliye Mkubwa Zaidi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0173_swa_f_48_nani_aliye_mkubwa_zaidi_13871_1675.mp3#duration=1120&size=11299793"},{"para_id":"13871.1724","title":"49 \u2014 \u201cMtu Akiwa na Kiu, na Aje\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0177_swa_f_49_mtu_akiwa_na_kiu_na_aje_13871_1724.mp3#duration=703&size=7128511"},{"para_id":"13871.1758","title":"50 \u2014 Katikati ya Mitego","mp3":"\/mp3\/13871\/0180_swa_f_50_katikati_ya_mitego_13871_1758.mp3#duration=856&size=8662407"},{"para_id":"13871.1798","title":"51 \u2014 Nuru ya Uzima","mp3":"\/mp3\/13871\/0184_swa_f_51_nuru_ya_uzima_13871_1798.mp3#duration=1310&size=13204222"},{"para_id":"13871.1859","title":"52 \u2014 Mchungaji, Mungu","mp3":"\/mp3\/13871\/0190_swa_f_52_mchungaji_mungu_13871_1859.mp3#duration=580&size=5898525"},{"para_id":"13871.1886","title":"53 \u2014 Safari ya Mwisho Kutoka Galilaya","mp3":"\/mp3\/13871\/0194_swa_f_53_safari_ya_mwisho_kutoka_galilaya_13871_1886.mp3#duration=863&size=8730237"},{"para_id":"13871.1925","title":"54 \u2014 Msamaria Mwema","mp3":"\/mp3\/13871\/0198_swa_f_54_msamaria_mwema_13871_1925.mp3#duration=616&size=6260151"},{"para_id":"13871.1952","title":"55 \u2014 Si Kujionyesha kwa Nje","mp3":"\/mp3\/13871\/0200_swa_f_55_si_kujionyesha_kwa_nje_13871_1952.mp3#duration=433&size=4434757"},{"para_id":"13871.1971","title":"56 \u2014 Upendo wa Yesu kwa Watoto","mp3":"\/mp3\/13871\/0201_swa_f_56_upendo_wa_yesu_kwa_watoto_13871_1971.mp3#duration=543&size=5526138"},{"para_id":"13871.1996","title":"57 \u2014 Kijana Tajiri Mtawala Amepungukiwa na jambo Moja","mp3":"\/mp3\/13871\/0203_swa_f_57_kijana_tajiri_mtawala_amepungukiwa_na_jambo_moja_13871_1996.mp3#duration=478&size=4879601"},{"para_id":"13871.2019","title":"58 \u2014 Kufufuliwa kwa Lazaro","mp3":"\/mp3\/13871\/0205_swa_f_58_kufufuliwa_kwa_lazaro_13871_2019.mp3#duration=1099&size=11092144"},{"para_id":"13871.2066","title":"59 \u2014 Makuhani na Wakuu Wanaendelea na Njama Yao","mp3":"\/mp3\/13871\/0206_swa_f_59_makuhani_na_wakuu_wanaendelea_na_njama_yao_13871_2066.mp3#duration=454&size=4641463"},{"para_id":"13871.2088","title":"60 \u2014 Cheo Kikuu Ni Kipi?","mp3":"\/mp3\/13871\/0208_swa_f_60_cheo_kikuu_ni_kipi_13871_2088.mp3#duration=406&size=4158184"},{"para_id":"13871.2112","title":"61 \u2014 Mtu Mfupi Aliyekuwa Mashuhuri","mp3":"\/mp3\/13871\/0210_swa_f_61_mtu_mfupi_aliyekuwa_mashuhuri_13871_2112.mp3#duration=401&size=4111640"},{"para_id":"13871.2133","title":"62 \u2014 Mariamu Ampaka Yesu Mafuta","mp3":"\/mp3\/13871\/0211_swa_f_62_mariamu_ampaka_yesu_mafuta_13871_2133.mp3#duration=1307&size=13170907"},{"para_id":"13871.2190","title":"63 \u2014 Yesu Atangazwa Kuwa Mfalme wa Israeli","mp3":"\/mp3\/13871\/0218_swa_f_63_yesu_atangazwa_kuwa_mfalme_wa_israeli_13871_2190.mp3#duration=707&size=7169996"},{"para_id":"13871.2232","title":"64 \u2014 Watu wa Kuangamia","mp3":"\/mp3\/13871\/0222_swa_f_64_watu_wa_kuangamia_13871_2232.mp3#duration=693&size=7031722"},{"para_id":"13871.2263","title":"65 \u2014 Hekalu Latakaswa Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0224_swa_f_65_hekalu_latakaswa_tena_13871_2263.mp3#duration=1329&size=13390450"},{"para_id":"13871.2316","title":"66 \u2014 Kristo Akabiliana na Adui Zake","mp3":"\/mp3\/13871\/0228_swa_f_66_kristo_akabiliana_na_adui_zake_13871_2316.mp3#duration=740&size=7505171"},{"para_id":"13871.2352","title":"67 \u2014 Yesu Azuru Hekalu Mara ya Mwisho","mp3":"\/mp3\/13871\/0231_swa_f_67_yesu_azuru_hekalu_mara_ya_mwisho_13871_2352.mp3#duration=1219&size=12295749"},{"para_id":"13871.2400","title":"68 \u2014 Wayunani Walipotaka \u201cKumwona Yesu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0233_swa_f_68_wayunani_walipotaka_kumwona_yesu_13871_2400.mp3#duration=666&size=6756313"},{"para_id":"13871.2430","title":"69 \u2014 Dalili za Kuja Kwa Kristo Mara ya Pili","mp3":"\/mp3\/13871\/0235_swa_f_69_dalili_za_kuja_kwa_kristo_mara_ya_pili_13871_2430.mp3#duration=1155&size=11655117"},{"para_id":"13871.2473","title":"70 \u2014 Kristo Ashirikiana na Wenye Dhiki na Masikini","mp3":"\/mp3\/13871\/0239_swa_f_70_kristo_ashirikiana_na_wenye_dhiki_na_masikini_13871_2473.mp3#duration=566&size=5758478"},{"para_id":"13871.2498","title":"71 \u2014 Mtumishi wa Watumishi","mp3":"\/mp3\/13871\/0241_swa_f_71_mtumishi_wa_watumishi_13871_2498.mp3#duration=943&size=9526890"},{"para_id":"13871.2539","title":"72 \u2014 Meza ya Bwana Yaanzishwa","mp3":"\/mp3\/13871\/0243_swa_f_72_meza_ya_bwana_yaanzishwa_13871_2539.mp3#duration=958&size=9677405"},{"para_id":"13871.2576","title":"73 \u2014 \u201cMsifadhaike Mioyoni Mwenu\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0246_swa_f_73_msifadhaike_mioyoni_mwenu_13871_2576.mp3#duration=1908&size=19179012"},{"para_id":"13871.2641","title":"74 \u2014 Pambano la Kutisha Katika Gethsemane","mp3":"\/mp3\/13871\/0251_swa_f_74_pambano_la_kutisha_katika_gethsemane_13871_2641.mp3#duration=1080&size=10900601"},{"para_id":"13871.2688","title":"75 \u2014 Kesi Batili Dhidi ya Yesu","mp3":"\/mp3\/13871\/0256_swa_f_75_kesi_batili_dhidi_ya_yesu_13871_2688.mp3#duration=1590&size=25543110"},{"para_id":"13871.2752","title":"76 \u2014 Jinsi Yuda Alivyopoteza Roho Yake","mp3":"\/mp3\/13871\/0262_swa_f_76_jinsi_yuda_alivyopoteza_roho_yake_13871_2752.mp3#duration=692&size=7020406"},{"para_id":"13871.2784","title":"77 \u2014 Kristo Ashtakiwa Mbele Ya Gavana Wa Kirumi","mp3":"\/mp3\/13871\/0266_swa_f_77_kristo_ashtakiwa_mbele_ya_gavana_wa_kirumi_13871_2784.mp3#duration=1936&size=19458815"},{"para_id":"13871.2868","title":"78 \u2014 Yesu Afa Juu Ya Kalwari","mp3":"\/mp3\/13871\/0274_swa_f_78_yesu_afa_juu_ya_kalwari_13871_2868.mp3#duration=1671&size=16811964"},{"para_id":"13871.2932","title":"79 \u2014 Jinsi Kifo Cha Kristo Kilivyomshinda Shetani","mp3":"\/mp3\/13871\/0281_swa_f_79_jinsi_kifo_cha_kristo_kilivyomshinda_shetani_13871_2932.mp3#duration=884&size=8938225"},{"para_id":"13871.2968","title":"80 \u2014 Yesu Apumzika Katika Kaburi La Yusufu","mp3":"\/mp3\/13871\/0285_swa_f_80_yesu_apumzika_katika_kaburi_la_yusufu_13871_2968.mp3#duration=708&size=7178978"},{"para_id":"13871.2994","title":"81 \u2014 \u201cBwana Amefufuka\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0288_swa_f_81_bwana_amefufuka_13871_2994.mp3#duration=562&size=5718538"},{"para_id":"13871.3022","title":"82 \u2014 \u201cMama Unalilia Nini?","mp3":"\/mp3\/13871\/0292_swa_f_82_mama_unalilia_nini_13871_3022.mp3#duration=578&size=5878775"},{"para_id":"13871.3051","title":"83 \u2014 Kutembea Kwenda Emau","mp3":"\/mp3\/13871\/0293_swa_f_83_kutembea_kwenda_emau_13871_3051.mp3#duration=498&size=5083897"},{"para_id":"13871.3073","title":"84 \u2014 Kristo Aliyefufuka Atokea","mp3":"\/mp3\/13871\/0296_swa_f_84_kristo_aliyefufuka_atokea_13871_3073.mp3#duration=595&size=6053282"},{"para_id":"13871.3100","title":"85 \u2014 Kando Ya Bahari Tena","mp3":"\/mp3\/13871\/0299_swa_f_85_kando_ya_bahari_tena_13871_3100.mp3#duration=789&size=12730367"},{"para_id":"13871.3133","title":"86 \u2014 \u201cEnendeni . . . Mkawafanye Mataifa Yote\u201d","mp3":"\/mp3\/13871\/0302_swa_f_86_enendeni_mkawafanye_mataifa_yote_13871_3133.mp3#duration=936&size=15074513"},{"para_id":"13871.3172","title":"87 \u2014 Kristo Aingia Mbinguni Kwa Ushindi","mp3":"\/mp3\/13871\/0306_swa_f_87_kristo_aingia_mbinguni_kwa_ushindi_13871_3172.mp3#duration=691&size=11154751"}]