Maranatha

36/183

Mwongozo Usio Weza Kukosea, Sura ya 36

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Yakobo 1:22 Mar 44.1

Mungu anawaita wale wajuao mapenzi yake kuwa watendaji wa neno lake. Udhaifu, kutojitoa mioyo kikamilifu, na kusitasita kunakaribisha mashambulio ya Shetani; na wale wanaoruhusu tabia hizi kukua hawataweza kujiepusha na maanguko kutokana na mawimbi makali ya majaribu. Kila ajiitaye ‘Mkristo’ anapaswa kukua na kufikia kiwango kamili cha Kristo, ambaye kwa Mkristo ndiye kiongozi wa juu aliye hai. Mar 44.2

Sisi sote tunahitaji mwongozo tupitiapo nyakati za dhiki maishani kama jinsi baharia anavyomhitaji rubani katika maeneo yenye mchanga mwingi au katika mto wenye miamba mingi, na je, mwongozo huu linapatikana wapi? Tunakuelekeza katika Biblia. Hii ilivuviwa na Mungu, ikaandikwa na watakatifu, kwa uwazi na uangalifu kabisa ikielekeza wadogo kwa wakubwa kwenye wajibu wao. Hii inainua mawazo, inalainisha mioyo, na kuleta furaha yenye utukufu rohoni. Biblia inawakilisha kiwango cha tabia kisicho na kasoro; ni mwongozo usio na makosa katika hali zote, hadi mwishoni kabisa mwa safari ya maisha. Hebu ichukue kama mshauri wako, kama kanuni kwa ajili ya kila siku ya maisha yako... Mar 44.3

Katika maandiko maelfu ya johari za ukweli zimejificha machoni pa mtafutaji aangaliaye juu juu. Mgodi wa ukweli kamwe haumaliziki. Kadiri Maandiko yanavyochunguzwa kwa mioyo minyenyekevu, ndivyo shauku itakavyoongezeka, na ndivyo utakajisikia kusema kama Paulo: “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!” Mar 44.4

Kila siku unapaswa kujifunza jambo jipya kutoka katika Maandiko. Fanya kama utafutaye hazina iliyofichwa, kwani humo ndimo yapatikanapo maneno ya uzima wa milele. Omba kwa ajili ya hekima na ufahamu ili kuelewa maandiko haya matakatifu. Kama utafanya hivi, utaona utukufu mpya katika neno la Mungu; utahisi kupokea nuru mpya na yenye thamani katika masomo yalivounganika na kweli, na Maandiko kwa ujumla yatadumu kuonekana ya thamani zaidi katika tathmini yako. Mar 44.5

Hebu uwe na bidii ya kutumia kila njia ipatikanayo katika neema, ili ubadilishwe tabia yako na ukue kufikia kiwango kamili kifaacho kwa watu wa Kristo Yesu. Mar 44.6